Saturday, 18 August 2012
SAFARI ZA RAIS JAKAYA KIKWETE TANGU AINGIE MADARAKANI 2005!- 2012
President Jakaya Kikwete and his wife, Salma Kikwete and Minister for Tourism in Jamaica, Mr Edmund Bartlett (right) and Chairman of the Mystic mountains conservation, Mr Horace Clarke, touring the hills facing the tourist attractions in St. Ann region, in Jamaica. |
Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili yake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005
UPDATES
Mpaka leo tarehe 23/8/2011 tayari amesha safiri safari 315 tangu aingie magogoni octoba mwaka 2005
Hii ni rekodi ya kipekee duniani ambayo watz tunatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele maatako nyuma
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Libya, ... UPDATES
Kesho tar 9/9/2011 rais atasafiri kuelekea Kenya kwa ziara ya kikazi
Hiyo ni safari ya 316 tangu rais aingie madarakani mwaka 2005!
UPDATES:
Safari ya 317 kwa rais wangu kipenzi!
ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa
hasara.mia
UPDATES
Safari ya 318 ya rais mwenye maajabu duniani!
JK anaondoka leo kuelekea Australia kwenye mkutano wa jumuiya ya madola...
President Jakaya Mrisho Kikwete in a group picture with some top officials of Turkey Confederation of Businessmen
UPDATES
Wakuu nimepata taarifa halisi za wastani wa gharama ya NAULI ya kila safari ya nje ambayo rais kikwete na ujumbe wake hutumia! Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya kuaminika toka wizara ya fedha,hazina na magogoni ni kuwa kila msafara hugharimu kadirio la juu milioni 300 na kadilio la chini ni milioni 250. Zingatieni hii ni NAULI ya ndege iende irudi tu!
Sasa hebu chambueni wenyewe ikulu inatumia kiasi gani kwa safari za rais?
UPDATES16/12/2011
Safari ya 319, hivi sasa yupo nchi Uganda katika mkutano uitwao International Conference of Heads of State (ICGLR)
Rais wetu anazidi kujijengea heshima katika mkakati wake wa kuvunja rekodi ya dunia kwa kusafi hata ziara zenye kumtuma waziri, yeye anasafi tu ilimradi lengo litimie
Inashangaza sana kuona maraisi wenzake kwa kujali zaidi maslahi ya mataifa yao, hawakuona sababu za kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika wakabaki na wengine kutuma wawakilishi tu, lakini jk hata kicheni pati akialikwa Urusi atasafiri bila kukosa.
Rais kikwete na Wasiri wa Nje Wa Marekani Bi Cliton
UPDATES
Safari ya 320 ya Rais JK Ameenda Davos Kuikomboa Tanzania, acheni Kelele !
ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2012
Obama Na Kikwete MAREKAni
UPDATES:
SAFARI ya 321 ya Mh Rais Jakaya M. Kikwete, sasa leo anatua katika nchi ya Afrika kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili leo Jumamosi, Januari 28, 2012UPDATES: 21/2/2012
Rais kikwete na Rais Wa Marekani Obama na bibi cliton
SAFARI ya 322,
Leo mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete amesafiri kwenda Uingereza,hakuna sababu ya msingi inayompeleka huko japo kubwa ni kupangua Baraza la Mawaziri.UPDATES: 24/2/2012
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan, Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya siku mbili.
SAFARI YA 323,
Leo Rais mwenye maajabu duniani, mutu ya musoga, aka msafiri kafiri, anatua Botswana ikiwa ni mwendelezo wa safari zake za kikazi, huku nyumbani amecha mbwa wamepatwa na kichaa wanaua raia wanaomba haki yao ya kulindwa!
Inasikitisha, inashangaza aminini haya ndiyo ya FILAUNI.
Rais Jakaya Kikwete akipokewa rasmi na Mfalme Abdullah II ibn Al Hussein wa Jordan katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi nchini Jordan tarehe 22.02.2010.
UPDATES:
Safari ya 324!
15/04/2012 Rais Jakaya Kikwete ametua Brazili kwa ziara ya kikazi!
UPDATES:
SAFARI YA 325
Leo tarehe 22 rais Jakaya Kikwete amewasili Malawi kushiriki mazishi ya aliyekuwa rais wa Malawi Bingu wa Mtharika!
Raitba inasema atarudi tz tarehe 24
KIKWETE hUKO chNA
UPDATES:
Leo tarehe 9/5/2012
Safari ya 326 tangu mkuu wa nchi aingie madarakani!
Rais amewasili Addis Ababa Ethiopia KWA KONGAMANO LA UCHUMI LA KIMATAIFA KWA AFRICA!
UPDATES:
Safari yake ya 327,
Rais Jakaya Kikwete yupo nchini Marekani tangu tarehe 16/5/2012 akisubiri kuhudhuria mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 19/5/2012,
UPDATES
SAFARI YA 328:
Leo tarehe 1/7/2012
Rais wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwete na ujumbe wake wamesafiri mpaka Kigali Rwanda kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo!
Mungu ibariki Tanzania!
UPDATES:
SAFARI YA 329
Tarehe 2/7/2012
Rais Jakaya baada ya kutoka kuhudhuria sherehe za uhuru nchini Rwanda, ameunganisha kwenda nchini Burundi kuhudhurua sherehe za Uhuru wa nchi hiyo!UPDATES
Tarehe 10/7/2012
Safari ya 330:
Hivi punde tumewasili nchini Uingereza,
Msafara wa mh rais Jakaya Kikwete umewasili Hyatt Regency London-The Churchill
rais wa Tanzania na rais wa Burundi
Ziara hii imetufikisha hapa kwaajili ya mh rais kuhudhuria mkuta unaohusu mambo ya Family Plan!
UPDATES:
SAFARI YA 331
Tarehe 14, rais Jakaya Kikwete amewasili Mjini Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU),UPDATES:
SAFARI YA 332.
Rais Jakaya Kikwete amewasili Kampala, Uganda,*kuhudhuria mkutano wa*nchi*za Maziwa Makuu asubuhi Agosti*8, 2012
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho kikwete
UPDATES
SAFARI YA 333 .
Rais Jakaya Kikwete yupo nchni Ghana kuhudhuria msiba wa rais wa nchi hiyo.
UGONJWA UNAOITESA AFRICA YA MASHARIKI NA KATI; EBOLA
Ebola: Ugonjwa hatari unaoitesa jamii Afrika | Send to a friend |
Friday, 17 August 2012 09:37 |
Na Florence Majani KATIKA siku za hivi karibuni ugonjwa wa Ukimwi umetajwa kuwa si janga tena hasa baada ya mwanga wa tiba yake kuanza kuonekana- njia za kuzuia na dawa za kufubaza makali ya virusi vyake kupatikana. Lakini, Afrika inaendelea kusumbuliwa na maradhi mengi mno, kiasi cha kutatiza afya za wakazi wake. Miongoni mwa magonjwa hayo ni malaria, ambao unasemekana kuua watu wengi zaidi barani humo. Lakini, ugonjwa wa ebola ambao umeikumba nchi jirani ya Uganda hivi karibuni baada ya miaka ya karibuni kutesa wengi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unatajwa kuwa ni ugonjwa hatari zaidi pengine kuliko Ukimwi kwa namna unavyomtesa mgonjwa, unavyoua kwa haraka na unavyoambukiza kwa wepesi. Mwananchi lilifunga safari na kuzungumza na daktari Henry Mwakyoma, Mkuu wa Kitengo cha Patholojia wa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili (MNH). Dk Mwakyoma anaulezea ugonjwa huu kama ugonjwa wa hatari zaidi ambao wanasayansi wameshindwa kupata tiba yake hadi sasa. Daktari huyu anasema ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya ‘ebola’ ambavyo hupatikana kwa wanyama wa porini hasa waishio katika maeneo yenye joto katika nchi za Afrika. Jina la ugonjwa huo, yaani ebola, limetokana na Mto Ebola, uliopo nchini DR Congo. Dk Mwakyoma anaongeza kuwa zipo aina tano za virusi vya ugonjwa huu na majina yake yamepatikana kulingana na mazingira yake. Kwa mfano kirusi cha ebola cha nchini Uganda kinaitwa ‘Bundibugyo Virus’ na kile cha DRC kimepewa jina la ebola. Kirusi cha nchini Sudan kimepewa jina la Sudan Virus na nchini Ivory Coast kimepewa jina la Tail Virus. Anaongeza: “Aina ya tano ya kirusi cha ebola ilipatikana Amerika ya Kusini, lakini kirusi hiki hakijabainika kusababisha madhara kwa binadamu.” Ebola yaingia duniani Tukio la kwanza la ugonjwa hatari wa ebola liligundulika Agosti 29, 1976 katika eneo la nyanda za juu nchini DR Congo, liitwalo, hususan Yambuku. “Ugonjwa huu uliwapata wakazi wa Yambuku ambao inasemekana walikuwa wakila mizoga ya wanyama wa porini, hasa sokwe na popo,” anasema mtaalam huyo. Mwaka huo huo ugonjwa huo uliibuka nchini Sudan katika maeneo ya viwanda vya pamba, katika mji wa Nzara na mwaka 1994, ugonjwa huu uliibuka nchini Ivory Coast na kusababisha maafa makubwa. ‘Ugonjwa wa ebola uliibuka nchini uganda Julai 2007 katika wilaya ya Bundibugyo,” anasema Dk Mwakyoma. Binadamu hupataje ebola? Dk Mwakyoma anasema utafiti uliofanyika miaka ya nyuma uliabini kuwa virusi vya ebola huingia kwa mwanadamu kutoka kwa wanyama wa porini, hasa sokwe na popo. “Baada ya binadamu kula nyama yenye virusi hivyo, husambaa na katika mwili wake, na huo ndiyo mwanzo wa wanadamu wengine kupata maradhi hayo,” anasema. Anaongeza kuwa utafiti huo uligundua kuwa baadhi ya wanyama wanaweza kuishi na virusi vya Ebola bila kuwadhuru na wanyama wengine huweza kudhurika na kufa kama wanavyoathiriwa wanadamu. Binadamu hawezi kuambukizwa Ebola kwa njia ya upumuaji, bali hupata kwa njia ya majimaji ya mwilini mwa mwanadamu. Majimaji hayo ni pamoja na damu, jasho, kamasi, kinyesi na wakati mwingine mbegu za kiume pamoja na vifaa ambavyo mgonjwa anayeugua ebola atakuwa amevitumia. “Ndiyo maana tunasema ugonjwa huu ni hatari zaidi kwa sababu, ni kwa sekunde chache tu ukifanya mchezo umeambukiwa na kifo chake ni cha haraka sana,” anasema. Dk Mwakyoma anasema virusi vya ebola hupendelea kukimbilia katika mishipa ya damu na hivyo huenda kuathiri ogani muhimu mwilini ambazo huufanya mwili ujiendeshe. Ogani ambazo huathiriwa zaidi ni ini, figo, mishipa midogomidogo ya damu, mfumo wa chakula na mfumo wa upumuaji. Dalili za ugonjwa huu Dalili za awali za ugonjwa huu, Dk Mwakyoma anaeleza kuwa huanza kuonekana kuanzia siku ya kumi hadi wiki mbili baada ya binadamu kupata maambukizi. Anazitaja dalili za mwanzo kuwa ni mafua makali ambayo si mafua ya kawaida kama ambayo wengi wetu huugua, la hasha, bali ni mafua ya kipekee. Lakini pia, mtu aliyepata uambukizo wa virusi vya ebola huchoka mwili, hupata homa inayoambatana na vipele vidogovidogo kama vile vya kusisimkwa. “Mgonjwa hupata maumivu makali katika viungio vya mwili (joints),misuli na maumivu ya kifua. Lakini, pia kadri siku zinavyosonga mbele, mgonjwa huendelea kupata madhara mengine,” anasema Madhara hayo ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa chakula jambo linalosababisha mgonjwa kutapika , kukosa hamu ya chakula na wakati mwingine kuharisha. Virusi hivyo huendelea na kwenda mpaka katika mfumo wa njia ya hewa, virusi hivyo vinaposhambulia mfumo huo mgonjwa huanza kukohoa, kupata kwikwi kwa kiwango cha juu na kuwashwa koo. “Virusi hivi ni vya hatari zaidi kwani humfanya mgonjwa akaathirika hata katika mfumo wa neva za fahamu kwani baadhi huanza kuchanganyikiwa akili, kichwa kuuma sana, kuchoka na kupata degedege(seizures) na mwisho mgonjwa huwa mahututi (coma),” anaeleza Dk Mwakyoma Vilevile, mgonjwa wa ebola huathirika katika ngozi kwani hutokewa na vibaka vidogo sana vyenye ukubwa wa tundu la sindano, vilivyovilia damu. “Vitundu hivyo vya damu hutokana na kuathiriwa kwa mishipa ya damu mwilini na kwa kitaalamu huitwa ‘maculo paular rashes. Vitundu hivyo huonekana chini ya ngozi ya mgonjwa,” anasema. Anasema baada ya muda vitundu hivyo huwa vikubwa na huanza kuvuja damu endapo mgonjwa atachomwa na kitu chenye ncha kali kama sindano na damu huendelea kutoka kwa wingi kadri siku zinavyokwenda. “Dalili ya mgonjwa kutokwa damu ni mbaya na mara nyingi hupelekea kifo, kwa sababu damu hiyo haitoki nje peke yake, bali hutoka ndani kwa ndani mwilini mwa mgonjwa” anasema. Dk Mwakyoma anasema: “ Kifo kwa mgonjwa wa ebola husababishwa na mchanganyiko wa mambo mengi. Kwanza ni kushuka kwa mapigo ya moyo(hypertension), kufa kwa ogani za mwilini kama ini, figo, ubongo na kupoteza damu na maji mengi,” Anasema ndiyo maana mgonjwa wa ebola huteseka na hufa baada ya muda mfupi kwa sababu mwili wake hushambuliwa kwa kiasi kikubwa kwa muda mfupi. “Kingine kibaya zaidi ni kupoteza damu, kwani mgonjwa anaweza kuwa anatapika damu, anaharisha damu nyeusi, na anakohoa damu,” anasema Tiba Mtaalam huyo anasema hadi sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa ebola. Anasema asilimia 70 ya watu wanaougua ugonjwa huu hufa. Anaongeza kuwa hiyo ni sababu kubwa inayoufanya ugonjwa huu uwe hatari zaidi kwani mgonjwa awahi au asiwahi matibabu, kama ameupata ugonjwa huu, hawezi kupona. “hakuna tiba ya ugonjwa huu, bali mgonjwa hutibiwa dalili au magonjwa yanayomkumba, kwa mfano, akiishiwa damu huongezewa damu, akiishiwa maji, huwekewa maji au kumshusha homa iliyopanda,kukohoa au kutapika” anasema Lakini, anasema kwa kuwa ebola huambukizwa kwa wepesi usio wa kawaida, mgonjwa hutengwa kabisa na jamii na wanaomshughulikia kwa mfano madaktari, hutakiwa kuvaa kinga za hali ya juu. Dk Mwakyoma anaeleza kuwa asilimia 30 ya watu wanaopona ugonjwa wa ebola huweza kubaki na virusi hivyo na kuendelea kuambukiza kama VVU vinavyobaki kwa watu wanaotumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi (ARVs). Anasema wengi wanaopona hubaki na madhara kama nywele kunyonyoka, macho kuathiriwa kwa kutokwa machozi, au kudhuriwa na mwanga, na kwa wengine virusi vya ebola hubaki katika mbegu za kiume na kike. “Virusi vya ebola ambavyo vinatajwa kubaki katika mwili wa mwanadamu na kuendelea kudhuru wengine ni virusi vya Sudan. Kwa mfano, mwanaume ambaye aliugua ebola akapona, huweza kumwambukiza mke wake kwa njia ya kujamiiana na kusababisha ugonjwa huo kulipuka kwa mwanamke,” anafafanua Dk Mwakyoma anasema ugonjwa wa ebola ni wa hatari zaidi na kuwa ni vyema kama maeneo ya mipakani yakaongezewa ulinzi lakini pia alishauri watu kuacha kula baadhi ya wanyama wa porini wanaotajwa kuwa na virusi hivyo. |
BILLY GRAHAM; MUNGU ASIPOIPIGA MAREKANI AWAOMBE RADHI SODOMA NA GOMORA, ASEMA WAMEKITHIRI KWA UOVU
“If God doesn’t punish America, He’ll have to apologize to Sodom and Gomorrah.”
Mwinjilisti wa kimataifa, Billy Graham (95), amesema ikiwa Mungu hatashuka kuihukumu Marekani kutokana na kufanya uasi wa kila namna bila ya kuwa na hofu, basi itampasa aiombe radhi Sodoma na Gomora miji ambayo aliangamizwa kwa moto.
Rai hiyo aliitoa wiki chache zilizopita katika sherehe ya kuzaliwa, kwake ‘birthday’ iliyofanyika wiki iliyopita na kushuhudiwa na maelfu ya watu ambapo alisema kuwa wamarekani wamekuwa wakifanya dhambi kwa namna ya kutisha na sasa imefikia hatua mbaya, hawana tena hofu ya Mungu.
Billy Graham Mwinjilisti wa Kimataifa |
Alibainisha kwamba Mungu ni mwingi wa rehema, na kuwa ikiwa watamaanisha kutubu na kuziacha dhambi zao ni dhahiri kwamba atawasamehe na kuwarehemu, lakini wakishupaza shingo wataangamia kabisa.
Mwinjilisti huyo alisema ili kuikimbia ghadhabu ya Mungu, Wakristo wote nchini humo na mataifa jirani kama Kanada,wanapaswa kukusanyika kwenye majumba yao na marafiki, majirani na ndugu zao ili kushiriki ibada kwa pamoja kupitia Luninga zao aliyoiita “Living Room Crusade” kwa muda wa siku 40 kuanzia September 28 hadi November 6 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.
Mwinjilisti huyo wa kimataifa ambaye amekuwa akimtumikia Mungu kwa miongo kadhaa sasa, alibainisha kuwa, katika kukusanyika pamoja kwenye majumba ya Wakristo, kila mmoja atapata wasaa wa kueleza uovu wake mbele za Mungu, huku akichanganua kuwa suala la utoaji wa mimba limekuwa kubwa.
Mbali na hilo, mtumishi huyo ambaye amekuwa akiwapa ushauri wa kiroho marais mbalimbali waliowahi kuitawala Marekani, akisisitiza juu ya hilo; alitolea mfano wa mji wa Ninawi ambao ulikithiri kwa dhambi, lakini Yona alipoingia na kuwaambia kutangaza kuwa utaangamia baada ya siku 40 walisikia na kutubu.
“Ninaamini msamaha walioupata wana wa Ninawi, unaweza kutokea na kwetu, Yona alipopita na kutangaza, waliitana na kutubu,” alisema Mwinjilisti Graham.
Miongoni mwa watumishi nchini humo waliounga mkono kauli hiyo ya Graham, ni pamoja na Mwenyekiti wa ‘American for Jesus’ Anne Gimenez ambaye siku hiyo ya kutubu atakusanya watu zaidi ya laki moja huko Philadelphia, alieleza kwamba, jambo kama hilo liliwahi kutokea kipindi cha nyuma Marekani na mataifa ya Ulaya baada ya kuibuka kwa mmomonyoko wa maadili na mambo ya kiroho.
“Nadhani wazo la Billy Graham ni sahihi, taifa hili linakuwa na watu wengi wasioamini, na jambo hilo linavyokuwa kwa kiasi hichi giza huingia, lakini kama tukiomba, basi nuru itaingia,” alisema.
Mwingine ni Mwandishi wa vitabu nchini humo, Rabbi Jonathan Cahn, kwa upande wake alieleza kwamba Mwinjilisti huyo wa kimataifa amekuwa Mchungaji kwa marais na watu maarufu kwa miaka mingi, na hilo analolisema sasa ni onyo linalopaswa kuangaliwa na kutendewa kazi.
“Haijalishi ni giza la namna gani lililopo, bado lipo tumaini na wokovu pia, lakini ni pale tutakapotubu na maombi ya watu wa Mungu, unajua akisema Marekani ina shida tunatakiwa kutubu,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Awakening America Alliance, Billy Wilson, alisema kwa upande wake atakusanya makanisa ya kipendekoste na Charismatic zaidi ya 300 na kwamba wamefurahia jambo hilo lililoletwa na Billy Graham.
Tangu mwaka 2002 mtoto wa Billy Graham, na mjukuu wake Will Graham, wamekuwa wakifanya uinjilisti katika mataifa kama 50 ya Ulaya, Afrika, Asia, Latini na Mashariki ya Kati na miongoni mwa makanisa yanayoshiriki ni zaidi ya 305,000 na kwa msingi huo watu wapatao milioni 10 wameweza kumgeukia Kristo.
Imeelezwa kwamba makusanyiko ya kusikiliza ujumbe wa Graham, yatayofanyika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye majumba ya kupata kahawa, na maduka yanafananishwa na mtoza ushuri nyakati za Biblia, kuwa baada ya kutubu dhambi aliamua kuita watu na kuwarudishia kile alichokuwa akitwaa kinyume na taratibu.
Wakati huo huo Askofu E. W. Jackson, mtaalamu wa mambo ya Maji na sheria kutoka chuo cha Harvard, nchini Marekani, amewataka Wakristo nchini humo, kutokichagua chama cha Democratic, katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika November, 2012 kwa kuwa kina imani potofu.
Mwandishi Paul Stanley, wa gazeti la Kikristo nchini humo anaripoti kuwa, hivi karibuni Askofu huyo alieleza kwamba chama cha Demokratic kinawaingiza utumwani baadhi ya waamerika.
“Waachieni watu wa Mungu waende,” alisema Jackson akiwaambia Wakristo kupitia mawasiliano ya simu ni wazi kuwa Democratic ni chama cha Mpinga Kristo katika nchi hii.Wameikataa Biblia na kile Wakristo wanachokiamini, na kuhamasisha kile watakacho wao kinyume na maadili ya familia. Hii ni mbaya kwakuwa wanalimomonyoa taifa na Mungu wetu,” alisema.
Askofu Jackson alinyooshea kidole habari za hivi karibuni kutoka kwa Waliberali waliomshambulia kwa maneno mwanamichezo wa Olympic, Gabrielle Douglas, mwenye umri wa miaka 16, aliyeshinda medali ya dhahabu huko London 2012 na kusoma Biblia, lakini wapenzi wa chama hicho wakamjia juu ya kuwa haikuwa sahihi.
Baada ya ushindi wa mwanariadha huyo alisoma maandiko kwenye Warumi 12:19, yasemayo: “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana.” Mwanadada huyo mahiri aliazimia kumpa Mungu utukufu kwa ushindi wake,” alisema katika taarifa yake ya kimaandishi.
MWANAMKE TAJIRI NA MREMBO KULIKO WOTE UGANDA
JARIDA maarufu la Times nchini Uganda limemtaja mama wa watoto wawili Zari Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo kwa wakati huu.
Kwa mujibu wa jarida hilo Zari (30) ambaye ni Mwanamuziki,Mfanyabiashara na Mtangazaji wa runinga amepata mafanikio makubwa kwenye muziki na pia kipindi chake cha runinga kinachofananishwa na kipindi cha ‘Keeping up with the Kardashians’ kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.
Huku likiambatanisha picha za magari na nyumba anazomiliki mwanadada huyo, jarida hilo limeandika kuwa huenda akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho endapo ataendelea na mwenendo wake wa sasa kibiashara.
hata hivyo jarida hilo pia limetaja zari kuwa mmoja wa mstaa wapenda starehe na amekuwa akitumia mkwanja alionao kumnasa mwanaume wa aina yoyote anahisi kuwa anahitaji kumliza kwa wakati huo ingwa tuhuma hizo hazikusibitishwa moja kwa moja.
katika hatua nyingine jarida hilo limesema kuwa Zari mwenye maskani yake pia nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa uganda kuzaliwa ispokuwa ni wahamiji kwani baba yake ni raia wa Buurundi mwenye asili ya Somalia na mama yake ni raia wa India kutoka kabila la Mutoroo.
Aidha Times limeandika kuwa Zari anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW – 2006, Black Chrysler – 2008, – Audi Q7 2010 Silver Crysler – 2008, JETTA-2006, Mercedes Benz convertible -2008. Range-Rover, Lamborghin, Hummer na mengine mengi huku pia akiwanaumiliki wa maduka, hotel na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria, Cape Town na Kampala.
Subscribe to:
Posts (Atom)