YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 13 October 2012

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU MSIBANI MWANZA NYUMBANI KWA MAREHEMU (SACP) LIBERATUS BURLOW



 Watu wanajongea polepole nyumbani kwa Marehemu Liberatu Burlow huku wakiwa hawaamini kilichotokea.
 Nyumbani  kwa Marehemu Liberatus Burlow aliyekuwa Kamanda wa Police Mkoa wa Mwanza
aliyeuwawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.
 Ni huzuni tupu,bado ni mapema sana kamati zinaundwa na mikakati inapangwa juu ya kukabiriana na Msiba huu Mkubwa.
Marehemu Liberatus Barlow
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Liberatus Barlow.

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HUKO MBAGALA BAADA YA Mtoto MMOJA KUKOJOLEA MSAHAFU NA KUZUA TAFRANI KUBWA KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM



 Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate. Picha na Happy Mnale
 Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo
 Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
 Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam leo
HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR LEO

DAR ES SALAAM, Tanzania

VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.

Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.

Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.

Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.

Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa   

Friday, 12 October 2012

JOKATE MWEGELO AKIWA KWENYE ALA ZA ROHO CLOUDS FM



Jokate Mwegelo akiwa studio kuongelea uzinduzi wa Kampuni yake ya Kidoti ambayo jana imezindua product ya nywele bandia za kina dada.
.

ENEO DOGO ASLAY ANAPOWASAIDIA WAZAZI WAKE KUJENGA NYUMBA.


3
Staaa wa bongofleva ambae wengi tulimfahamu kupitia single ya ‘naenda kusema kwa mama’ dogo Aslay ndio anasaidia kuwajengea wazazi nyumba hapa Gongo la mboto Dar es salaam.
.
Pesa aliyoitoa Aslay ndio imenunulia haya matofali ambapo mara ya mwisho kuongea na Aslay aliniambia alikua ametoa zaidi ya shilingi laki nane kwa ajili ya huo ujenzi, yani kila anapopata pesa za show kidogo anakimbiza nyumbani kwao huku yeye akiendelea na masomo.
Interview na mama Aslay.
Hii ndio nyumba wanayoishi wazazi wake Aslay Gongo la mboto Dar es salaam, wamepanga na ina chumba kidogo na sebule na wanailipia elfu 20 kwa mwezi.
Aslay.

NDUGU WAKRISTO WENZANGU NAOMBA MUONE KAVA LA MOVIE HII...TUNADHALILISHWAAA



Official cover ya filamu mpya ya ‘Sister Mary’

MSANII nguli wa filamu Tanzania, Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Sister Mary’, iliyofanyika chini ya RJ Company ambayo itakuwa na nyota wengine kama Irene Uwoya,Johari na wengine kibao ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu nchini. Ndani ya mzigo huoUwoya amecheza kama Sister Mary na Rayamecheza kama Father Criss.

Ray alizungumza na mtandao wa DarTalk na kusema kuwa zipo filamu nyingine ambazo zinakuja lakini hiyo imeshakamilika na mashabiki wake wataanza kuitazama pia imetengezwa katika kiwango cha hali ya juu.

“Hiyo ndiyo filamu ambayo inakuja kwa sasa na nipo na wasanii wengi wazuri ambao wanafanya vizuri na kila msanii amecheza vizuri kulikana na nafasi yake, hata hivyo nawaomba mashabiki wangu wanipe sapoti yao kwani bila wao mimi siwezi kusimama na kufanya filamu,” alisema,

WANACHUO WANNE WALIVYOUWAWA KIKATILI KIMAKOSA WAKISHUTUMIWA KWA WIZI.



Wanafunzi wanne wa chuo wameuwawa kikatili kwa kupigwa na kuchomwa moto hadharani kwenye kijiji cha Aluu Nigeria kilichokaribu na chuo chao kwa tuhuma za wizi wa laptops na simu kitu ambacho inaaminika hawakukifanya.

Waliamua kuungana na kuanza kuishi kwenye kijiji hicho kutokana na kutoridhishwa na mazingira ya hostel za chuo, wakiwa marafiki wanne walimsindikiza mmoja wao kwa jamaa mmoja anaemdai aliekua anaeishi kwenye hicho kijiji ambacho kimekua kikikumbwa na matukio ya unyang’anyi na wizi wa vitu mbalimbali.

Daily post wameandika kwamba walipofika kwa mdaiwa kutokana na malumbano jirani yake ambae ni mama alianza kupiga kelele kwamba hawa wanafunzi ni wezi na ghafla ndio kikundi cha wananchi wenye hasira wakakusanyika na kuanza kuwapiga mpaka kuwachoma moto.


Taarifa nyingine kutoka mitandao mbalimbali ya Nigeria zinasema wanafunzi hawa wanne walimchukua mwenzao mmoja ambae anajulikana kwa ubabe ili wamtumie kumtisha huyu anaedaiwa atoe pesa haraka, huyu jamaa waliemuongeza akawa watano inasemekana alikua na bastola.

Wakati wa purukushani na mdaiwa aliionyesha hiyo bastola na wakati wananchi walipokusanyika baada ya kupigwa kelele za wezi jamaa mwenye bastola kwa uoga aliamua kuisalimisha ile bastola ambayo ndio wananchi walipata uthibitisho kwamba jamaa ni wezi, wakaanza kuwapiga lakini aliesalimisha bastola akafanikiwa kukimbia wkaabaki hawa wanne ambao ndio wameuwawa.
Taarifa zote nilizozisoma zinasema wanafunzi hawa hawakuwa wezi na wametoka kwenye familia zenye uwezo, hata mmoja wao miezi kadhaa iliyopita alikua nchini Marekani kwa mapumziko, ndio huyo hapo chini kwenye picha akiwa shopping Marekani.

Wednesday, 10 October 2012

MSANII WA FILAMU BONGO AONYEZA TATTOO ZAKE KWENYE MAKALIO:


Msanii Rayuu wa Bongo movie.


Wasanii wa Bongo sasa mmezidi na nyie. kila siku mipicha yenu mpo Uchu tu au ndio imekuwa Fashion ya siku hizi?

HUU NDIO UNYAMA ALIONIFANYIA MKE WANGU:


“Mimi ni dereva wa daladala linalofanya safari Mwenge na Temeka, Septemba 28, mwaka huu sikuweza kurudi nyumbani baada ya basi hilo kuharibika. Kutokana na tatizo hilo, nilishindwa kuliacha barabarani ndipo nilimtumia ujumbe mke wangu kumuarifu.

“Niliporudi  nyumbani asubuhi nilikumbana na maswali mengi kutoka kwa mke wangu, kisha akaingia jikoni na kunyanyua surufia iliyokuwa na uji akanimwagia usoni, ukaniunguza vibaya sana.

“Baada kufanyiwa unyama huo nilipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo wasamaria walikuja na kunipeleka Hospitali ya Temeke ambako nililazwa.

“Kabla ya tukio hilo tumekuwa tukizozana mara kwa mara na hata kutishia maisha yangu lakini nashindwa kuachana naye kwa kuwa nimezaanaye,” alilalamika Mlewa.
 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,  ACP David Misiime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mama huyo ameshakamatwa na upelelezi unaendelea.

HUU NI UZALENDO ATOA KALI NYINGINE! AMWAGA CHOZI BAADA YA YANGA KUTOKA SARE NA SIMBA.


Tuesday, 9 October 2012

SOMA JINSI BINTI WA MIAKA 16 ZIMBABWE ALIVYOTIRIRIKA KUHUSISHWA KWENYE DINI YA KISHETANI.


0
Bulawayo.
Mtandao maarufu wa Naija Gists umeripoti kwamba binti mmoja wa miaka 16 Zimbabwe ameshtua nchi baada ya kujitokeza na kusema yuko kwenye dini ya kishetani ambayo waumini wake hunywa damu za watu.
Kilichowashtua wengi zaidi ni kwamba amewataja watu 38 ambao wamefariki tayari ,na hiyo ni kutokana na kunyonywa damu na waumini wa dini hiyo.
Hakuishia hapo, huyu binti ametaja mpaka majina ya watu 60 anaoshirikiana nao kwenye hiyo biashara akiwemo mchungaji wa kanisa moja maarufu lililopo cawdray park Bulawayo na ametaja mpaka nyumba ilipo na kuamplfy kwamba kwenye hiyo nyumba kuna chumba cha chini ya ardhi ambacho ndio watu huwa wanawekwa huko wakisubiri kuuliwa damu ipatikane.
.
Alijiunga na hiyo dini akiwa na umri wa miaka 15 tu na ilikua ni baada ya kushawishiwa na mwanaume ambae alikua ni mpenzi wake mwenye umri wa miaka 32, siku moja akiwa kwenye kituo cha basi na boyfriend wake, alijisikia vibaya mwilini na akakaribia kuanguka ndio boyfriend wake na rafiki zake wakamnyanyua na kumpeleka kwenye nyumba iliyopo karibu na kituo cha basi.
Kwenye hiyo nyumba ndio kuna hicho chumba cha ardhini ambapo alilishwa damu ya watu, polisi wa Zimbabwe wamethibitisha kupata hizo taarifa toka wiki iliyopita ila hawajasema chochote mpaka  wakimaliza uchunguzi.

YALIOJIRI KATIKA MAGAZETI YA LEO TAREHE 10/10/2012

0
.
.
.
..
..
.
.
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.