YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 20 November 2014

HIVI NDIVYO MWAKYEMBE ALIVYOSULUBIWA


Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake na Shirika la Reli Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji na Uwezeshaji, Pauline Gekul alitoa madai hayo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).
Gekul alisema taratibu hazikufuatwa kwa kuwa haieleweki ni lini Serikali, wakala au Wizara ya Uchukuzi ilitangaza zabuni ya mradi wa treni kutoka Stesheni hadi Pugu kupitia JNIA.
“Pia haijulikani ni lini Serikali ilifanya upembuzi yakinifu kuhusu mradi huo wa reli kwa kufuata taratibu kama zinavyoainishwa na Sheria ya PPP ya mwaka 2010 ambayo inafanyiwa marekebisho hivi sasa,” alisema Gekul na kuongeza: “Haijulikani ni kampuni ngapi ambazo ziliomba tenda ya ukandarasi wa treni na kwamba M/s Shumoja ilishinda tenda hiyo kwa vigezo gani.”
Alisema kwa kifupi ni wazi kuwa Dk Mwakyembe na wizara yake walikiuka vifungu vya Sheria ya PPP. Alivitaja vifungu hivyo kuwa ni 4(1) na (2) vinavyomtaka waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.
Gekul alisema pia kifungu cha 5(1) kilikiukwa ambacho kinaitaka mamlaka inayohusika kufanya upembuzi yakinifu baada ya kupembua mradi ambao utafanywa kwa ubia.
“Pia kifungu cha 9 kinachotaka mzabuni kutoa nyaraka mbalimbali za miradi ikiwamo jina, mahesabu yaliyofanyiwa ukaguzi pamoja na vielelezo vya uwezo wa kifedha,” alisema Gekul.
Alihoji kulikuwa na uharaka gani wa utekelezaji wa mradi huo ambao umekiuka Sheria ya PPP bila kuwahusisha wadau wengine ambao wangeweza pia kushindana na Shumoja?
“Ingekuwa ni vyema kama Serikali ingeweka bayana undani wa mkataba wa mradi huo ambao kama Watanzania hatujawahi kusikia ukitangazwa ili kutoa fursa kwa wazabuni wenye uwezo kushindania zabuni hiyo zaidi ya kuona na kuusikia mradi siku ya utiaji saini,” alisema.
Alisema Serikali ikishabanwa kutoa majibu juu ya uvunjwaji wa sheria, huja na majibu ya kejeli, hivyo Watanzania waelewe kuwa sheria zimekuwa zikipindishwa ili kupitisha miradi ambayo baadaye hugeuka kuwa mzigo kwao kama ilivyokuwa IPTL na Escrow.
Alisema pamoja na adha ya usafiri jijini Dar es Salaam, ukweli utabaki palepale kwamba, Dk Mwakyembe alisimamia mchakato wa mradi uliokiuka sheria ambao ikiwa utashindikana katika utekelezaji na mzigo wa uvunjwaji ama usitishwaji wa mkataba, gharama zitarudi kwa Watanzania.MWANANCHI

Wednesday, 19 November 2014

HUYU NDYE BINTI ALIYESABABISHA KIFO CHA MASHAKA! MFANYABIASHARA MKUBWA ALIYEFARIKI NDANI YA GARI LAKE HUKO BUKOBA!



Inasikitisha sana kifo cha huyu bwana Leonard Mtensa kilichotokea ndani ya gari lake, mpenzi wake anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Hapa chini ni picha ya huyo dada na picha ya marehemu.
 
Jackline Hassan mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa na marehemu.
Huyu ndiye marehemu bwana Leonard Mtensa aliyekutwa na mauti ndani ya gari lake aina ya IST akiwa na mpenzi wake!

HAYA NDIO MAISHA! MADAME WEMA SEPETU ATUPIAMO AKIWA NA USAFIRI WAKE MPYA NA KUACHA FUMBO KAMA KAWAIDA!


Binti Wa Miaka 5 Abadilisha Maisha Ya Familia Yake.


Binti Mdogo Abadilisha Maisha Ya Familia Yake Kutoka Katika Hali Ya Kawaida Na Kuwa Katika Maisha Ya Hali Ya Juu,Jina Lake Anaitwa Breanna.


 Nyota Ya Mtoto Huyu Iling"ara Pindi Mama Yake Alipopost Picha Zake Katika Mtandao ambapo Alipata MashabikiZaidi Ya Milioni Moja  Waliomfolo Kupitia Page Yake Ya Instagram.

Breanna Anatokea Korea Kusini Lakini Kwa Sasa Anaishi Dubai Na Familia Yake,Amepata Mialiko Mbali,Mbali Ya Kwenda Kufanya Dili Za Uwana mitindo Na Sehemu Ambazo Ameshatembelea Bahrain Na Indonesia.

Breanna anabeba Mikoba Ya Gharama Kubwa Ikiwemo Louis Vuitton,Channel Na Kuvaa Nguo Za Wabunifu Wakubwa Duniani,Wakati Mwingine Mama Yake Anapata Hofu Kubwa  Juu Ya Binti Yake Na Kuhofia Ukuwaji Wake Kulingana Na Umaarufu Aliokuwa Nao.

Inapotokea Anaumwa Basi  Hupata   E-Mail Nyingi Kutoka Nchi MbaliMbali Kutaka Kujua Breanna.
 Kwa Sasa Ni    Gumzo Kwa Breanna Na Familia Yake Pindi Wanapopita Mitaani Kila Anae Muona anamshangaa na Kutaka Kupiga Nae Picha .