YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 10 August 2018

MAGAZETI YA LEO TAREHE 10/08/2018


JINSI DIRISHA LA USAJILI LILIVYOFUNGWA ENGLAND

Yerry Mina, Andre-Frank Anguissa, Caglar Soyuncu

Image captionYerry Mina, Andre-Frank Anguissa, Caglar Soyuncu
Dirisha kuu la uhamisho wa wachezaji England lilifungwa mnamo Alhamisi 9 Agosti saa moja saa Afrika Mashariki (ambazo ni saa kumi na moja England - 17.00BST), mwaka huu soko likifungwa mapema kuliko misimu ya awali.
Klabu zinazocheza ligi nyingine England na Wales, miongoni mwake ligi za Championship, League One na League Two bado zinaweza kuendelea kuwanunua wachezaji hadi mwisho wa mwezi huu.
Soko la kuhama wachezaji Scotland pia litafungwa 31 Agosti sawa na katika mataifa mengine Ulaya.
Siku ya mwisho, nani alihama?
Presentational grey line

9 Agosti

Ligi Kuu ya England
* saa ni wakati (kwa BST) uhamisho ulipotangazwa na klabu
20:30 Danny Ings [Liverpool - Southampton] Mkopo
20:20 Andre-Frank Zambo Anguissa [Marseille - Fulham] £22.3m
20:20 Timothy Fosu-Mensah [Manchester United - Fulham] Mkopo
20:02 Andre Gomes [Barcelona - Everton] Mkopo
20:02 Yerry Mina [Barcelona - Everton] £27.19m
19:21 Domingos Quina [West Ham - Watford] Ada Haijafichuliwa
19:01 Luciano Vietto [Atletico Madrid - Fulham] Mkopo
18:59 Martin Montoya [Valencia - Brighton] Ada Haijafichuliwa
18:35 Federico Fernandez [Swansea - Newcastle] iliripotiwa kuwa £6m
18:30 Harry Arter [Bournemouth - Cardiff] Mkopo
18:00 Caglar Soyuncu [Freiburg - Leicester] iliripotiwa kuwa £19m
18:00 Jordan Ayew [Swansea - Crystal Palace] Mkopo
17:40 Joe Bryan [Bristol City - Fulham] £6m
17:18 Sergio Rico [Sevilla - Fulham] Mkopo
17:15 Peter Gwargis [Jonkopings Sodra IF - Brighton] Ada Haijafichuliwa
17:01 Isaac Mbenza [Montpellier - Huddersfield] Mkopo
17:00 Carlos Sanchez [Fiorentina - West Ham] Ada Haijafichuliwa
16:59 Dan Burn [Wigan - Brighton] Ada Haijafichuliwa*
*Burn atarejea Wigan kwa Mkopo hadi Januari 2019
16:50 Bernard [Shakhtar Donetsk - Everton] Bila Ada
14:30 Leander Dendoncker [Anderlecht - Wolves] Mkopo
13:00 Victor Camarasa [Real Betis - Cardiff] Mkopo
10:45 Filip Benkovic [Dinamo Zagreb - Leicester] Ada Haijafichuliwa
10.31 Lucas Perez [Arsenal - West Ham] Ada Haijafichuliwa
10:02 Mateo Kovacic [Real Madrid - Chelsea] Mkopo
08:06 Daniel Arzani [Melbourne City - Manchester City] Ada Haijafichuliwa

Thursday, 9 August 2018

MH. RAISI MAGUFULI AHUZUNISHWA NA KIFO CHA NGULI "KING MAJUTO"


Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha msanii mkongwe hapa nchini Mzee Amri Athuman maarufu kwa jina la King Majuto.
Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.
“King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake” Rais Magufuli.


MH. RAISI MAGUFULI AMPOKEA MH. RAISI MUSEVENI ALIYEFANYA ZIARA YAKE TANZANIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Magufuli amempokea Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalim Nyerere ambapo amewasili nchini kwa ziara ya siku moja na kwa pamoja watafanya mazungumzo Ikulu Jijini DSM leo. 

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 70 KWA UBAKAJI WA MTOTO MDOGO


Leo August 9, 2018 Mahakama ya Wilaya Bukoba chini ya Hakimu mkazi Samweli Maweda imemuhukumu miaka 30 jela mzee wa miaka 70 kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 11 wa kata ya Maruku halmashauri ya wilaya Bukoba Mkoani Kagera.
Akiongea nje ya mahakama Wakili wa serikali mkoa wa Kagera Emmanuel Kahigi amesema kuwa tukio hilo lilitokea mwezi wa sita mwaka jana na kuongeza kuwa sambamba na mzee huyo aliyehukumiwa leo pia baba mzazi wa mtoto ameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika kosa hilo na kesi inaendelea.


KING MAJUTO HATUNAYE TENA

Alijizolea tuzo mbalimbali enzi za uhai wake

Image captionAlijizolea tuzo mbalimbali enzi za uhai wake
Msanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia wakati akipokea matibabu kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Dar es Salaam Tanzania.
Muigizaji huyo veterani alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki kwake.
Taarifa ya ikulu imesema King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Tuesday, 7 August 2018

YANAYOENDELEA MONDULI BAADA YA MBUNGE KUHAMIA CCM


Wanachama wa CCM wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka Mbunge wa CHADEMA Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.
Wakizungumza katika ofisi hizo wamesema wamesikia taarifa za kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha.

ASKOFU KILAINI ATAKA USHIRIKIANO KWA MAENDELEO YA KAGERA

Kupitia hafla iliyofanyika ya makabidhiano ya ofisi kati ya Mkuu wa mkoa mstaafu na mkuu wa mkoa mpya Kagrera wamealikwa Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa madhebu ya Dini.
Kati ya viongozi hao alikuwemo Askofu Methodius Kilaini ambaye ni Askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Bukoba na amesema kuwa kabla ya ujio wa mkuu mpya wa mkoa viongozi wa madhehebu yote mkoa wa Kagera walikaa na kujadiliana jinsi watakavyofanya kazi na mkuu huyo ili kuhakikisha mkoa unasonga mbele kimaendeleo.
Mjeshi kakabidhiwa Ofisi, mambo matatu makubwa atakayoanza nayo

Monday, 6 August 2018

CHINA NA BURUNDI WALETA BARUA KWA MH. RAISI JOHN POMBE MAGUFULI


Leo August 6, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke ambaye pamoja na kufanya nae mazungumzo amewasilisha barua kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping.
Katika mazungumzo hayo Wang Ke amemueleza Rais Magufuli kuwa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na China umeendelea kukua kwa kasi kubwa hususani katika masuala ya kiuchumi, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa na kwamba katika kipindi cha miaka 6 iliyopita uwekezaji wa China nchini Tanzania umekuwa mara kumi kutoka Shilingi Trilioni 1.58 hadi kufikia Shilingi Trilioni 15.82.
Wang Ke amemhakikishia Rais Magufuli kuwa China itaendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya Tanzania.
Kuhusu ombi alilolitoa Rais Magufuli wakati meli ya matibabu ya China ilipokuja hapa nchini mwezi Novemba 2017, Wang Ke amesema Rais Xi Jinping ameshafanyia kazi ombi hilo kwa kutoa udhamini wa masomo kwa madaktari 20 watakaosomea ngazi ya uzamili na uzamivu katika matibabu ya ini na uboho (bone marrow) katika Chuo Kikuu cha Shandong cha China, na pia nafasi 30 za wataalamu watakaohudhuria semina ya mafunzo ya usimamizi wa hospitali.
Rais Magufuli amemshukuru Rais Xi Jinping kwa kutoa nafasi hizo za masomo na kwa mchango mkubwa wa China katika maendeleo ya Tanzania, na amemuomba Wang Ke kufikisha ujumbe wake kwa Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa kidugu na kihistoria na China.
Rais Magufuli ametoa wito kwa Wang Ke kuendelea kuwahimiza wawekezaji zaidi kuja kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili na kwamba Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Canada hapa nchini Ian Myles na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini Paul Cartier baada ya Mabalozi hao kumaliza muda wao.
Baada ya mazungumzo hayo Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa kwao na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi zao na wamempongeza Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa hatua kubwa za kuleta mageuzi ya kiuchumi, kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma, kupambana na rushwa na kuboresha huduma za kijamii.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezechiel Nibigira ambaye amewasilisha barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza.
Aidha, Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Nibigira, mazungumzo ambayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa Burundi hapa nchini Gervais Abayeho.

KARIBU KAGERA BRIGEDIA JENERALI MAICO GAGUTI

Leo August 6, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Maico Gaguti leo amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu ambaye amestaafu.
Baada ya makabidhiano hayo amemuapisha Mkuu wa Wilaya Kyerwa, sambamba na kuongea na wanakagera ambapo amesema kuwa vitu atakavyohakikisha anavifanyia kazi kwa mkoa huo ni kupamabana na Wahamiaji haramu, Magendo ya mipakani na uingiaji wa mifugo kutoka nchi jirani.
Ishu ya Wanawake kukatwa matiti “Wakitembea ni watu ila roho za kinyama”

MTIKISIKO WA BURUDANI NDANI YA DSM NA VIUNGA VYAKE UNASABABISHWA MWISHO WA WIKI HII PALE MERCURY PUB & LOUNGE MWENGE LUFUNGIRA.


Ukitaka kupata burudani kila siku na hasa kila mwisho wa wiki, basi usisite kufika katika Pub yako makini kabisa MERCURY PUB & LOUNGE ambapo utaweza kupata chakula kizuri na tofauti na vinywaji vya kila aina kutoka kwa wahudumu wenye weledi na wanaoipenda kazi yao, pia burudani ya muziki safi hatupo nyuma kwani utapata vyakula na kinywaji huku ukiburudishwa na mziki thabiti kabisa kutoka kwa MaDJ wakali hapa mjini wakiongozwa na DJ YP.

Fika weekend hii upate burudani na ujumuike na marafiki wa MERCURY PUB & LOUNGE katika Birthday Party ya kuadhimisha mwaka mmoja wa utoaji huduma bora kabisa hapa MERCURY PUB & LOUNGE. Kwa siku hiyo kwa atakaye nunua vinywaji viwili basi atapatiwa kinywaji kimoja boreee kabisa. Picha nyama choma itatolewa bure kwa siku hiyo kwa yeyote atakayefika. 

TETESI ZA SOKA NA USAJILI BARANI ULAYA.

Paul Pogba

Haki miliki ya picha
Image captionPaul Pogba
Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuwaambia Red Devils kuwa anaweza kufikia makubaliano ya pauni milioni 100 kwa mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 25 kwenda Barcelona. (Daily Star Sunday)
Pia meneja wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kuweka siku ya mwisho kumwinda mlinzi wa England Harry Maguire, 25, ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 80 na Leicester. (Sunday Express)
Toby AlderweireldHaki miliki ya picha
Image captionToby Alderweireld
Manchester United wanakaribia kuafikia makubaliano ya paunia milioni 60 kumsaini mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 29. (Sunday Mirror)
Lakini mbio za Manchester United za pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Barcelona raia wa Colombia Yerry Mina zimefikia kikomo kwa sababu ya mvutano kuhusu malipo ya ajenti. (Sun on Sunday)
Aaron RamseyHaki miliki ya picha
Image captionAaron Ramsey
Chelsea wanaweka tayari pauni milioni 35 kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27. (Sunday Express)
Chelsea watafanya mazungumzona mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard siku ya Jumamosi na kumpa mchezaji huyo wa miak 27 mkataba kwa pauni 300,000 kwa wiki kumzuia asijiunge na Real Madrid. (Sunday Times - subscription required)
Anthony MartialHaki miliki ya picha
Image captionAnthony Martial
Manchester United watamtoa mshambuliaji mfaransa Anthony Martial, 22, kwa Chelsea kumbadilisha na wing'a Mbrazil Willian, 29, huku wachezaji hoa wakiwekewa thamani ya pauni milioni 75. (Sunday Mirror)
Borussia Dortmund wanakataa kumuuza wing'a mmarekani anayewekewa thamani ya pauni milioni 60 Christian Pulisic, 19, anayetafutwa pia na Chlsea na Bayern Munich. (Mail on Sunday)
Wolves wametoa ofa ya pauni milioni 16 kwa mlinzi wa Besiktas na Croatia Domagoj Vida, 29. (Sabah - in Turkish)
Jose MourinhoHaki miliki ya picha
Image captionJose Mourinho
Jose Mourinho atakuwa meneja wa Ureno ikiwa ataondoka Manchester United. (Sunday Mirror)
Benfica wameanzisha mazungumzo kumsaini beki wa Manchester United na Italia Matteo Darmian ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 15m. (Sun on Sunday)
Leicester wanakaribia kumsaini wing'a wa Algeria Rachid Ghezzal, 26, kutoka Monaco. Mchezaji hyo amekuwa akiwindwa na Watford na Southampton. (ESPN)
Lucas PerezHaki miliki ya picha
Image captionLucas Perez
Arsenal wamekubali ofa ya pauni milioni 4.45 kutoka kwa Sporting Lisbon kwa mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez, 29. (A Bola - in Portuguese)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ublegiji Mousa Dembele, 31, amekaa kuelekea Inter Milan. (Sun on Sunday)
Fulham wameuliza kuhusu kumsaini beki Real Madrid mfaransa Theo Hernandez, 20, kwa mkopo. (Mail on Sunday)