YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 29 June 2013

MAOFISA WA MAREKANI WADAI KUWA WAO NDO WATAPANGA MAWAZIRI WA TANZANIA WATAKAORUHUSIWA KUSHIKANA MKONO NA OBAMA AKIJA DAR


Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.

“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki.


Aliongeza kuwa japokuwa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA) inaendelea kufanya kazi zake kama kawaida, lakini Jumatatu, Wamarekani watasimamia kila kitu hadi ukaguzi wa wageni.

“Siku hiyo mwongoza ndege wa TAA, atafanya shughuli kidogo, mambo mengine yatafanywa na wao,” alisema.

Idadi ya maofisa wa Tanzania
Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.
“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:
 
“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”
 
Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.
 
“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chika

TIZAMA YALIYOJIRI NJE YA HOSPITALI YA MEDICLINIC HEART ALIKOLAZWA MZEE NELSON MANDELA

Mke wa Mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela–Mandela  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumtembelea Rais wa zamani wa Afrka ya kusini Mzee Nelson Mandela hapo jana ijumaa
Akiendelea kuzungumza na vyombo vya habari nje ya hospitali alikolazwa mzee Nelson Mandela
Baadhi ya watu waliofika hospitalini hapo wakimpa moyo mke wa Mzee Nelson Mandela 

Endelea kusoma zaidi kwa kubofya hapa chini


Hiki ni chombo maalumu (kinachotumia remote) chenye mwonekano kama wa helicopter ambacho kimefungwa kamera kikiwa kinazunguka kwenye maeneo ya hospitali ya Mediclinic Heart iliyoko kwenye mji wa Pretoria nchini Afrika ya Kusini.
 Mtotot akiwa kapumzika nje ya jengo la Uhuru akiwa  ameweka picha ya Nelson Mandela kwenye maua hujo Pretoria, Afrika ya kusini hapo jana ijumaa
 Mtoto mdogo akiwa ameshika  picha ya rais wa kwanza mwafrika nchini afrka ya kusini mzee Nelson Mandela
Baadhi ya wanachi wakiomba kwa ajiri ya afya ya mzee Nelson Mandela
Mtoto Lesibana Kekana mwenye miaka mitano(5) akionesha upendo wa nchi yake baada ya kuonekana usoni ana bendera ya Afrika Kusini kwenye maeneo ya Soweto
Kweli kufa kufahana, baadhi ya wafanya biashara wakiuza khanga zenye pica ya Rais wa zamani, mzee Nelson Mandela nje kidogo ya hospitali ya Mediclinic Heart alikolazwa mzee Mandela

FUMANIZI LA AINA YAKE MUME AKIMBIA NA BOKSA MWANAMKE AVALIA NGUO YA NDANI KWENYE BAJAJI


KATIKA kuonesha kuwa bado uaminifu kwa wapenzi ni tatizo, juzikati lilitokea fumanizi la aina yake baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Flaviana kumnasa mwanaume aliyedaiwa ni mumewe, aitwaye Aron akifanya mapenzi na mwanamke mwingine
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika gesti moja iliyopo Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake huyo walichukua chumba baada ya kushindwa kurudi nyumbani kutokana na kuzidiwa na kilevi.

“Wakati Aron akiwa chumbani pale, alifika shosti wa Flaviana aitwaye Dina na kwa kuwa Flaviana alikuwa hajitambui, wawili hao walianza kupeana malavidavi.
“Flaviana akiwa amelala alikuwa kama vile anasikia watu wakishughulika lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na kuzidiwa na pombe.
“Wale wakaendelea kubanjuka. Ilipofika saa 12 asubuhi Flaviana akapata nguvu na kuamka kwenda kujisaidia, aliporudi akabaini shosti wake amemsaliti na ndipo alipoanzisha timbwili,” alidai mtoa habari wetu.
Flaviana apigia simu mapaparazi
Wakati timbwili hilo likiendelea chumbani hapo, Flaviana alipata mwanya wa kuwapigia simu mapaparazi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshuhudia Dina akiwa ndani ya Bajaj huku akivaa nguo kabla ya kumuamuru dereva kuondoka kwa spidi.
Naye mwanaume ambaye alikuwa ndani ya chumba cha gesti hiyo, aliposikia waandishi wamefika, alitokea mlango wa nyuma akiwa amevaa ‘boksa’ na tisheti, akaacha suruali yake chumbani hapo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi huku akiwaonesha mapaparazi kitanda kilichokuwa vululuvululu, kilichotumika katika usaliti huo pamoja kondom, Flaviana alisema: “Nimeumia sana, yaani nimesalitiwa nikiwa humuhumu chumbani, Aron kanidhalilisha sana na huyo Dina naye kumbe siyo mtu, nitahakikisha namsaka nimshikishe adabu.”

JOKATE AMWANIKA MWANAUME MPYA


MWANAMITINDO daraja la kwanza Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.
Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.
“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.
Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.
Baada ya paparazi wetu kuzitia kibindoni picha hizo, alimsaka Jokate kwa njia ya simu ili azitolee ufafanuzi.
Mwandishi: Haloo Jokate…
Jokate: Nitumie meseji nipo kwenye kikao.
Mwandishi wetu alimtumia meseji kama alivyoshauri staa huyo ambapo alimtaka amtambulishe mwanaume huyo na aeleze kama ndiye mpenzi wake mpya, hakujibu chochote.
Paparazi wetu alimtumia meseji ya pili kumsisitiza atoe majibu ndipo alipojibu kwa kifupi:“Hapana mumy!”
Pamoja na majibu hayo, paparazi wetu alimtumia meseji nyingine kumuuliza kama siyo mpenzi wake ni nani lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakujibu chochote.
Kabla ya kumuanika mwanaume huyo, Jokate aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku pia akitajwa kutoka na mcheza kikapu, Hasheem Thabeet.

PICHA ZIKIIONYESHA MAYI HOTEL MWANZA.

KWA MAWASILIANO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA MENEJA WA HOTEL. Mr JERARUDO D JOSEPH KWA NAMBA ZA SIMU +255 765 551 686
                                                                                    +255 786 685 191
AU UNAWEZA KUWASILIANA KUPITIA E-mail YA MENEJA MOJA KWA MOJA AMBAYO NI jodeph2013@gmail.com.  MTAA WA RWAGASORE/LUMUMBA St.
           P.O.Box 11972-Mwanza Tanzania, East Africa,

Mayi Hotel Mwanza,
logo ya Mayi Hotel MWANZA

MAYI HOTEL KAMA INAVOONEKANA KWENYE PICHA.

Vyumba vya Mayi Hotel.






The bloger himself akiwa ndani ya Mayi Hotel Mwanza,































































KWA MAWASILIANO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA MENEJA WA HOTEL. Mr JERARUDO D JOSEPH KWA NAMBA ZA SIMU +255 765 551 686
                                                                                    +255 786 685 191
AU UNAWEZA KUWASILIANA KUPITIA E-mail YA MENEJA MOJA KWA MOJA AMBAYO NI jodeph2013@gmail.com.  MTAA WA RWAGASORE/LUMUMBA St.
                                        P.O.Box 11972-Mwanza Tanzania, East Africa,