YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 26 March 2013

ZITTO KABWE NA IDI AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO




Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.


Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama.

Monday, 25 March 2013

HILI NDO DANGURO JIPYA LA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI DAR



  Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka shule hiyo, gazeti la mwananchi linaripoti
Hilo ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka walimu wao.

Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey(Pichani juu) alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.

KITABU CHA KIFO NI HAKI YANGU CHAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR



Mtunzi mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo.
Mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo, akiongea na wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar.
Mtunzi Eric Shigongo akimpatia kitabu mtunzi mwenziye, mzee Walter Bgoya.
Mzee Walter Bgoya akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Eric Shigongo cha 'Kifo ni Haki Yangu'.
Afisa wa polisi Patrick Massawe ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa hadithi za magazeti nchini, akisainiwa kitabu na Shigongo wakati wa uzinduzi.
Eric Shigongo (kushoto), akibadilishana mawazo na msomaji wa hadithi zake, Ahmed El Maamry, wakati akimsainia kitabu.
Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.
Eric Shigongo akisaini kitabu kwa ajili ya mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng'itu.
Shigongo akiwasainia vitabu baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Waratibu wa uzinduzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Abdallah Mrisho (kulia) na Angela Msangi wakisubiri uzinduzi.
Afisa wa polisi Patrick Massawe na msomaji mwingine wakipitia baadhi ya kurasa za kitabu cha Eric Shigongo aliyesimama kulia.
Baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la TPH.
MTUNZI mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo, leo amezindua rasmi kitabu chake cha 'KIFO NI HAKI YANGU' katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata zawadi ya kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala ya kitabu hicho na vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo chini:

KIZAAZAA CHA MVUA JIJINI DAR





Mvua kubwa iliyonyesha juzi na jana jijini Dar es Salaam, ilisababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo, hivyo nyumba kadhaa kujaa maji na baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.

Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua iliyoanza kunyesha muda wa asubuhi, pia yalisababisha hasara kubwa kutokana na vitu na mali mbalimbali kusombwa na maji.

Mwananchi lilitembelea maeneo mbalimbali na kushuhudia wananchi wakihangaika kuokoa mali zao, baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kujaa maji.


Barabara kadhaa zilikuwa hazipitiki kutokana na kujaa maji, huku baadhi ya nguzo za umeme na simu ambazo zilikuwa karibu na mifereji ziliharibiwa na kusombwa na maji.

Cheti alichotumia Mulugo cha Mhadhiri wa Mkwawa



Dar es Salaam. Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (Muce), kilichopo mkoani Iringa.

Mhadhiri huyo ni Dick Aron Mulungu ambaye alisoma na Mulugo katika Shule ya Sekondari ya Songea Wavulana kati ya 1994 na 1996 na alijiunga na shule hiyo baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kafule, ambayo iko mkoani Mbeya.

Taarifa zinaonyesha kuwa Mulungu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata Shahada ya kwanza katika Elimu (BA Education) 2001 na baadaye alisoma na kupata Shahada ya Uzamili (MA Development studies ) 2007.

Alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Hallow…(mwandishi akajitambulisha)
Mulungu: Sawa, unasemaje?
Mwanishi: Nazungumza na Dick Mulungu?

Mulungu: Ndiyo mimi.
Mwandishi: Hivi unamfahamu mtu anayeitwa Hamimu Agustino?
Mulungu: Aah… hivi ulisema unaitwa nani?
Mwandishi: Si nimeshajitambulisha jina na ofisi ninayotoka?
Mulungu: Nipigie kesho naona hapa kuna kelele.

Mwandishi: Mbona nakusikia vizuri tu?
Mulungu: Nipigie baada ya nusu saa basi.
Baada ya nusu saa…….
Mwandishi: Haloo… naona nusu saa imekwisha, uko tayari kuzungumza?
Mulungu: Huyo simfahamu.
Mwandishi: Kwani wewe si ulisoma Songea Boys?

Mulungu: Ndiyo
Mwandishi: Kwa hiyo humkumbuki mtu aliyekuwa akitumia jina hilo?
Mulungu: Huyo mtu namkumbuka ndiyo.
Mwandishi: Kwa sasa yuko wapi?
Mulungu: Siwezi kujua, si unajua tumesoma siku nyingi sasa huwezi kujua mtu amekwenda wapi… ni siku nyingi mno.
Mwandishi: Ahsante.

Chuo Kikuu na siasa
Taarifa zinaonyesha kuwa Waziri Mulugo alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania 2002 akitumia majina ya Philipo Hamimu Augustino na alisomea Shahada ya Sanaa katika Elimu (BA. Ed). Namba yake ya usajili chuoni hapo ni 08652/T.02.
Alipokuwa akiendelea na kazi ya ualimu Mulugo alianza harakati za kisiasa na ndipo alipoamua kwenda kugombea ubunge katika majimbo ya wilaya ya Chunya.

Kada wa chama cha NCCR Mageuzi wilayani Chunya, Nyawili Kalenda aliyejitambulisha kama mlezi wa siasa wa Waziri huyo alisema walifahamiana naye 2004 wakati Mulugo na rafiki yake walipokwenda kumtaka ushauri wa kugombea ubunge katika jimbo la Songwe.
Katika nakala za wasifu wake zinaonyesha kuwa 2008 alishika nafasi ndani ya CCM ambazo ni pamoja na mjumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi wilaya ya Chunya, Katibu wa Elimu, Uchumi, Malezi na mazingira wa jumuiya ya wilaya hiyo na mjumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Mbeya.

Kauli yake
Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule. “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo.

Licha ya kukiri kurudia darasa la saba, Waziri Mulugo alisema jina la Hamimu amekuwa akilitumia katika elimu tangu awali na kwamba hakuvunja sheria kufanya hivyo.

“Jina la Hamim ni la nyumbani Philipo ni jina langu la ubatizo, nadhani haya ni mambo ya kawaida na kweli nilipokuwa shule watu walikuwa wananifahamu kama Hamimu pia Philipo ni jina langu la ubatizo na kumbuka tukifika chuo huwa tunatumia jina la baba.

“Na pia ni kweli nilirudia shule kwa sababu wakati ule wa Mwalimu Nyerere na Mwinyi (Ali Hassan), sheria ilikuwa inaruhusu maana wanafunzi walikuwa wachache mno, fikiria katika darasa letu la saba tulimaliza watu saba tu. Baadaye sheria hiyo ilibadilishwa,” aliongeza.

Kuhusu jina la Dick Mulungu, alikiri kumfahamu mtu huyo na kwamba walisoma wote shule ya Sekondari ya Songea Boys. Hata hivyo, alipinga kutumia vyeti vyake.
Source;Mwananchi.

Supreme Court orders poll recount for 22 centres



The panel of six judges have until Saturday to decide whether Kenyatta should be confirmed as Kenya's new president or whether new elections should take place/CFM
The panel of six judges have until Saturday to decide whether Kenyatta should be confirmed as Kenya’s new president or whether new elections should take place/CFM
NAIROBI, Kenya, Mar 25 – The Supreme Court on Monday ordered a recount of votes cast at 22 polling stations during the March 4 General Election.
According to the court, re-tallying is meant to ascertain if the number of votes cast exceeds the number of registered voters in the respective stations.
The court also ordered the scrutiny of all forms 34 and 36 used by the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) in tallying the presidential election results.
“Re-tallying is to be done in 22 polling stations to verify the numbers of votes cast, valid votes and rejected votes,” said Supreme Court Judge Smokin Wanjala.
“On forms 36 the scrutiny will be aimed at ascertaining accuracy of transfer from forms 34 comparing the numbers on both forms,” the judge added.
Forms 34 contain results as recorded at each polling station while forms 36 contain aggregated results from forms 34.
Among the areas listed for re-tallying is the Don Bosco Primary School, St Andrews Primary School, Nairibi, Sango Primary School and the NCC Social Hall.
Both the petitioners and respondents have been ordered to appoint 10 agents each, to act as observers in the process.
The Registrar of the Supreme Court is expected to administer the oath of secrecy and confidentiality to all those who will be involved in the process.
The results are expected to be filed with the Supreme Court by 4pm on Wednesday.
Official election results showed president-elect Uhuru Kenyatta won 50.07 percent of the vote, approximately 800,000 votes ahead of his closest rival, Prime Minister Raila Odinga.
The court also ordered IEBC to provide the voter registration list it used in the tally of the presidential vote after an electronic system failed.
“We order the IEBC to provide the principal voter register in its entirety,” said Judge Njoki Ndung’u.
The court has also issued proposed timelines for the hearings which are expected to commence on Wednesday and close on Thursday.
In petition three and four, the parties have been allocated 54 minutes each while petition five – the one filed by Odinga – was allocated two hours and six minutes.
Respondents in all the three petitions have also been awarded time, similar to that awarded to the respective petitioners.
The respondents and petitioners objected to the time allocations insisting that they needed more time although the court insisted that the hearings will last 15 hours.
The court is expected to issue a conclusive statement on the time allocations on Tuesday when the parties meet for the last day of the pre-trial conference.
Already, arrangements are in place to fit the court with another stopwatch to help regulate the times that each participant is allocated.
“We have little time and it will be up to you to decide how to use your time; one thing that will not change is the time we have allocated for the hearing,” urged Justice Njoki Ndung’u.

 
 
 
 
 
 
 

HUKUMU YA MSANII KAJALA IMETOLEWA



Habari njema kwa mashabiki wa muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.


Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200. Taarifa kutoka mahakamani zinadai kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga fedha hizo ili wazilipe na tayari inasemekana Wema Sepetu amezitoa fedha hizo zote kutoka mfukoni mwake.

Mrembo huyo na mumewe Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni pamoja na kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria.