|
Meneja TANESCO KAGERA mhandisi Martine Madulu akieleza jinsi mradi huo unavyokamilishwa |
|
Transformer mpya yenye MVA15 |
|
Transformer ya zamani inayotumika sasa yenye MVA5 |
|
Mtaalamu kutoka makao makuu Tanesco Dar es salaam anayefunga Transformer hiyo Bwana AMON GAMBA, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu. |
|
Fundi msaidizi kulia akiendelea kukunjua waya unaotumika kuweka mawasiliano ya umeme katika transformer hiyo mpya. |
|
Mwonekano wa Transformer mpya ya kufua umeme kwa MVA15. |
Meneja wa shirika hilo mkoa wa kagera mhandisi MARTINE MADULU akiongea na waandishi wa habari, amesema wananchi mkoani kagera wanatarajiwa kuondokana na kukatikakatika kwa umeme kutokana na kufungwa transfoma mpya ya kusambaza umeme katika mkoa wa kagera.
Bwana madulu amesema kuwa serikali imeamua kufanya kuleta transfoma hiyo mpya iliyogharimu zaidi ya bilioni 1.4 kutokana na kuongezeka kwa wateja na kusababisha transfoma iliyokuwepo kushindwa kutoa huduma iliyokuwa inahitajika.
Mhandisi madulu ameongeza kuwa taransfoma hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya elfu 22 wa mkoa wa kagera kuliko hii ambayo ilikuwepo.
Pia amewataka wananchi kuendelea jkushirikiana na tanesco katika kutoa taarifa kwa wanahoujumu miundo mbinu ya shirika hilo.