MACHANGU: HATUTAACHA KUJIUZA NG’O, HATA WAKIKAMATWA WANARUDI TU
Wadada hao waliyasema hayo, juzi Jumatano baada ya kunaswa na paparazi wetu maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku chache baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara hiyo ndiyo maisha yao.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.
“Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.”
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.
Hata hivyo, katika pitapita ya mwandishi wetu maeneo mengi kama vile Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila mteja anayewatokea.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg