YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 31 October 2014

BUNGE LACHOMWA MOTO

Bunge lachomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais agoma kuachia madaraka

Burkina FAMbali na maafa makubwa yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na majengo ya bunge kuchomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais aliye madarakani amegoma kuachia madaraka yake.
Blaise Compaore rais wa Burkina Faso aliyekaa madarakani kwa miaka 27 anatajwa kuwa mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi na bado anasisitiza kuwa ana miezi 12 zaidi ya kuendelea kuwepo madarakani kabla ya kukabidhi madaraka kwa rais ajaye.
Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya machafuko hayo.
Chanzo cha machafuko hayo kinatajwa kuwa ni kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangemfanya Blaise Compaore kubakia madarakani kwa kipindi kingine zaidi.
Burkina FBurkina FAS
Burkina-Faso-600x337
Taarifa zinasema jeshi limelazimika kuongoza nchi hiyo ili kurejesha utulivu.

MISUKULE YA GWAJIMA KUTINGA MAHAKAMANI


Misukule ya Gwajima Yatinga Polisi.....Ndugu, Wazazi kuitwa ili kuthibitisha vifo vyao. Baada ya hivi karibuni kutoa waraka mzito unaowalenga watumishi wa mungu kwa kile alichodai kuwa ni ukiukwaji wa sheria za mungu, Nabii Hosea Chamungu ametangaza rasmi kuiwasilisha ripoti ya misukule feki mikononi mwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe....
Akiongea kwa kujiamini, Nabii ChaMungu alimuonyesha mwandishi baadhi ya picha za misukule ikiwemo iliyowahi kuonyeshwa ndani ya kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na mchungaji Josephat Gwajima..



"Unapofanya kazi ya mungu hutakiwi kuwa mwoga kwa lolote kwani yeye ndiye  anayetulinda sisi sote, kondoo wa bwana wamekuwa wakipotea siku hadi siku huku wachungaji tukiwaangalia bila kuwaokoa.Mimi sikubaliani na hii miujiza ya kutoa misukule inayotangazwa kila siku wakati hatujui hao misukule walifia wapi.

KIFO CHA MSANII MKONGWE BONGO MOVIE






Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi za chanzo cha kifo cha mzee wetu huyu.
Mzee Manento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakini na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi amina. 

  

UNAAMBIWA CHIDI BENZI ALIFANYIWA KITU MBAYA NA MAHABUSU WENZAKE,USTAA WAMPONZA




Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ alijikuta akizodolewa na mahabusu wenzake mara baada ya kuingizwa katika Karandinga kupelekwa Segerea baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Tukio hilo lilitokea Oktoba 28, mwaka huu ambapo Chid Benz alikuwa akipelekwa Segerea huku mahabusu waliokuwemo ndani ya gari hilo wakitoa maneno ya kumkejeli pale alipokosa kiti na kulazimika kusimana.
Mmoja wa mahabusu alisikika akimzodoa Chid Benz kwa kumwambia: ‘Ustaa wako hukohuko, simama’ ambapo msanii huyo hakuleta ubishi, alisimama na safari ya kuelekea Segerea ikaanza.Chid Benz akiwa chini ya ulinzi mkali Mahakamani hapo.
Chid Benz anadaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya  aina ya Heroine yenye thamani ya Tsh. 38,638, Bangi zenye thamani ya Tsh. 1,720 pamoja na vifaa vya utumiaji wa kuvuta dawa hizo ambapo alikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande hadi Novemba 11, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Wednesday, 29 October 2014

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO TAREHE 30, October 2014

.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Image00045
.
.
.
.
.
.
.
.
Image00005
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.