YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 19 September 2013

Hofu ya mashahidi Kenya kuhusu ICC


Jaji anayeongoza vikao hivyo amewaonya wanablogu dhidi ya kuwatambulisha mashahidi katika kesi hiyo
Mwanamke mmoja nchini Kenya amesema kuwa anahofia maisha yake baada ya kutambuliwa visivyo kwenye mitandao ya internet kwamba yeye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Mwanamke huyo anasema aliathirika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 lakini yeye si shahidi katika mahkama ya ICC.
Mama huyo Rahab Muthoni Kagiri ,mwenye umri wa miaka 27 kutoka eneo la Burnt Forest , huko Rift valley anasema yeye sii shahidi katika kesi hiyo inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto pamoja na mtangazaji wa zani Joshua arap Sang.
Akionekana mwenye wasiwasi Bi Rahab asema sie yeye aliyesimama kizimbani kama shahidi wa kwanza katika kesi hiyo kinyume na inavyodaiwa na mitandao ya kijamii nchini Kenya.
Mama huyo anadia kuwa picha hiyo alipigwa na rafiki yake kwa lengo la kuiweka katika mtandao wake wa Facebook majira ya saa tano siku ya jumanne.
Lakini alishangaa saa mbili baadaye alianza kupigiwa simu na jamaa , ndugu na marafiki wakisema wameona picha yake katika mtandao ukisema yeye ndie shahidi aliyetoa ushahidi dhidi ya naibu Rais Wiliam Ruto.
Bi Rahab anasema japo yeye pia ni muathiriwa wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1,00 waliuwawa lakini hajajitolea kutoa ushaidi katika mahakam hiyo ya ICC.
Na kutokana na madai ya ufichuzi wa mashahidi nchini Kenya , hii leo Mahakama ya ICC iliamuru shahidi wa kwanza ambaye alianza kutoa ushaidi wake siku ya jumatatu atoe ushahidi wake faraghani.
Hii nikutokana na kudaiwa kuwa na hofu nyingi

Tume ya Marikana - Polisi walidanganya


Wachimba migodi wa Marikana waliandamana wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi
Polisi wa Afrika Kusini wanatuhumiwa kwa kudanganya kuhusu mauaji ya Marikana yaliyotokea mwaka jana, ambapo wachimba migodi 34 waliuawa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza mauaji hayo.
Inasemekana polisi walitoa ushahidi wa uongo au kuficha nyaraka ambazo zilitoa taarifa za uongo kuhusu matukio katika mgodi huo
Kitendo cha polisi kuwauawa kwa kuwapiga risasi wachimba migodi katika mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin kiliwashtua sana wengi nchini humo.
Polisi walisema kuwa walikuwa wanajikinga kutokana na kuvamiwa na wachimba migodi hao siku chache baada waandamanaji kudaiwa kuwanyonga polisi wawili.
Tume ihiyo iliteuliwa na Rais Jacob Zuma kuchungza mauaji hayo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu kukamilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Taarifa yake ambayo imekuja siku kumi baada ya kupata taarifa za polisi kwenye komputa zao na pia kupitia nyaraka zao.

SHAHIDI AFARIKI GHAFLA MAHAKAMANI WAKATI AKITOA USHAHIDI HUKO MKOANI MARA...!!



Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati, wilayani Rorya, mkoani Mara, Charles Warito (38), ambaye ni shahidi wa  mlalamikaji  katika Kesi ya kudhuru mwili kwa kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kusababisha ulemavu amefariki dunia, wakati akitoa ushahidi.

Warito alikutwa na umauti huo akiwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime mbele ya Jaji  G. Ndika anayesikiliza kesi katika Wilaya za Tarime na Rorya.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana mchana baada ya Mwanasheria wa Serikali, Mayega na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta George Lutonja walimwita  kuingia Kizimbani tayari kutoa ushahidi.

Shahidi huyo alianza kutoa ushahidi wake na alieleza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na mtuhumiwa Kichohe Kichere ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Omoche Kata hiyo ya Nyahongo Shirati Januari 26, mwaka 2008 na kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kukatwa mkono na mwili wake ulianza kupooza na kulemaa upande wa kulia ambao mkono ulikatwa

Alipoanza kujibu maswali kutoka kwa wakili wa mtuhumiwa mara alianza kulegea na kuishiwa nguvu na kuanguka kizimbani na kuzimia  hali iliyofanya Mahakama hiyo Kusitisha Kusikiliza kesi na shahidi huyo kukimbizwa Hospitali ya Wilaya kupatiwa matibabu na alifariki kabla ya kupatiwa matibabu.

Mtuhumiwa katika kesi hiyo akiondoka haraka mahakamani hapo huku ndugu wa marehemu  aliyejitambulisha kwa jina Otieno Rada alisema: "Nimesikitishwa na kifo hiki cha ndugu yangu Charles Joseph kwani majeraha hayo aliyoyapata  ya kukatwa mkono na Kichere  yalisababisha alemae mkono na kuanza kupooza na yamechangia kifo chake."
Mwili wa marehemu Charles umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime ukisubili kuchukuliwa na ndugu zake kutoka Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati kwa maziko.

HUYU NDIYE MWANAMKE HATARI SANA KWA KUUZA MADAWA YA KULEVYA HADI OBAMA ANAMWOGOPA NA KUWA ADUI YAKE:



 
MWANAMKE raia wa Kenya, Naima Mohamed Nyakiniywa ambaye pia anatumia pasiport ya kusafiria ya Tanzania ikiwa na jina la Mwanaidi Ramadhani Mfundo maarufu kama Mama Leila, ni adui mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama kutokana na madai kwamba amebobea kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Obama, ambaye pia baba yake mzazi alikuwa Mkenya, mwaka 2011 alimtaja Naima katika orodha ya watu saba yeye akiwa wa 6 kuwa ni hatari kwa biashara hiyo haramu ya ‘unga’ ambapo pia aliamuru mali zake na wenzake hao zilizoko Marekani kutaifishwa, pia wasiruhusiwe kukanyaga ardhi ya taifa hilo kubwa duniani.
Septemba 16 na 17, mwaka huu, Mama Leila (na wenzake nane) alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mashitaka ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin, Juni Mosi, 2011 Mbezi Beach jijini Dar.
Rekodi zinaonesha kuwa mwanamke huyo alizaliwa Septemba 2, 1962, Majengo, Nairobi, Kenya. Ingawa ni maarufu maeneo mengi ya mji huo mkuu wa nchi jirani, Pumwani, Majengo, Kariokor, Kaloleni, Biafra na Bahati, lakini katika hali ya usiri mkubwa, mwanamke huyo hafahamiki kwa majina ya Mama Leila, Naima au Nyakiniywa, isipokuwa anafahamika kama Kanyanya.
Kanyanya anayedaiwa kuwa mama wa watoto watano, katika eneo analoishi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam anajulikana ni Mtanzania kutoka kabila la Wadigo na majirani wanasema ni mtu mwema, mwenye moyo wa kusaidia walio na shida, akiwa pia ni mfanyabiashara wa magari, saluni na ‘internet cafes’.
Nchini Kenya, inadaiwa Kanyanya alikuwa mtu mwema katika eneo la Majengo huku majirani wakisema hakukuwa na njaa katika eneo lolote ambalo Naima alikuwepo na kila mtu alipata alichokihitaji.
Kutajwa kwake na Rais Obama kunadaiwa kuwashtua wakazi wengi wa Nairobi ambako kama ilivyo Mombasa na Dar es Salaam, anamiliki mali mbalimbali, yakiwemo majumba ya kifahari.
Hata hivyo, mwaka 2009, Polisi wa Kenya walidaiwa kuwakamata vijana watatu wakiwa na madawa ya kulevya na wote walimtaja Naima kama ndiye mwenye mzigo lakini ilikuwa vigumu kwao kumuunganisha kutokana na kukosa ushahidi.
Chanzo  chetu kimethibitisha kwamba wakati mmoja Naima aliwahi kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani jijini Nairobi lakini shinikizo kutoka ‘juu’ lilisababisha mwanamama huyo kuachiwa bila kufunguliwa mashitaka.
Inadaiwa kuwa hata alipokamatwa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na biashara hiyo, kulikuwa na idadi ya simu za kutosha kutoka ofisi ‘kubwa’ jijini Nairobi zilizotaka aachiwe lakini polisi wa Bongo ‘walikomaa’ naye ili kumfahamu zaidi.
Naima anamiliki zaidi ya hati sita za kusafiria zenye majina na sura tofauti ili kufanikisha safari zake za mara kwa mara nje ya nchi na mojawapo ni ya Tanzania ambayo haifahamiki ilipatikana kutoka ofisi gani ya uhamiaji hapa nchini.
Katika orodha ya Rais Obama ya watu hao kutakiwa kufilisiwa mali zao na kutokanyaga Marekani, pia yupo mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilome, John Harun Mwau kutoka chama cha siasa cha Party of Independent Candidates of Kenya (PICK).
Wengine katika orodha hiyo ni Manuel Torres Felix wa Mexico, Gonzalo Inzunza Inzunza (Mexico) Haji Lal Jan Ishaqzai (Afghanistan), Kamchybek Asanbekovich 

AIBU!! MKE ASHIKWA UGONI NA WAKWE ZAKE AKIWA NA DEREVA WA BODABODA,MUME AANGUA KILIO....!!




WAZAZI wa mwanamme aliyejulikana kwa jina la Ally Maulidi Kambi, wakazi wa Kibada jijini Dar es Salaam wamemshika ugoni Farida Omar ambaye walidai ni mke wa Ally akiwa na dereva wa bodaboda, Risasi Mchanganyiko linakujuza mwanzo mwisho.
  Farida Omar akiwa na dereva bodaboda aitwaye Chidi baada ya kushikwa ugoni.
Tukio hilo la aibu lilijiri usiku wa Septemba 15, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kibada ambayo anaishi dereva huyo aliyejulikana kwa jina moja la Chidi.
KISA CHA UGONI
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kunaswa kwa Farida kulitokana na familia ya mumewe kutilia shaka nyendo za mwanamke huyo, hususan mumewe anapokuwa safarini.
“Wakwe zake, wakiwemo mashemeji na mawifi walishaziona nyendo za Farida kuwa si za kiuadilifu hasa mume wake anapokuwa safarini,” kilisema chanzo hicho.

 Mke akiwa chumbani kwa Chidi baada ya kunaswa na wakwe zake.
Kikaongeza kuwa mara nyingi mume akisafiri mwanamke huyo huenda kuishi na mwanamme mwingine mpaka mumewe anaporudi, hali ambayo imezua minong’ono mitaani kwa wale waliofanikiwa kujua hilo.
Maelezo ya wazi kutoka kwa vyanzo ni kwamba, chumba anachoishi Chidi kilipangwa na mwanamke mwingine na baadaye kumwachia Farida ili atanulie kiaina.

               Chumbani kwa Chidi alipokutwa Farida Omar.
WAKWE WAONGEA KWA JAZBA
Wakizungumza kwa jazba siku ya tukio, wakwe wa Farida ambao ni wazazi wa Ally walisema mwanamke huyo aliyeolewa na mtoto wao miaka mitano iliyopita, amekuwa si mwaminifu kwa mumewe hasa anapokwenda nje ya nchi, habari ambazo wao walizisikia na kuzifanyia kazi.
Waliongeza kuwa kutokana na tabia hiyo chafu, walijaribu kumuweka kikao mumewe na kumpasulia kila kitu lakini jamaa huyo hakuwa akiwaamini, alidhani ni roho mbaya zao tu.
 
SHEMEJI MTU APIGILIA MSUMARI
Wakati wazazi wakiongea hayo, shemeji mmoja wa Farida, yaani kaka wa Ally alidakia na kusema kuwa baada ya ndugu yao kwenda Kongo kikazi, Farida naye aliondoka nyumbani hapo bila kuaga na alipomtafuta kwa njia ya simu yake ya mkononi, mwanamke huyo alijibu kuwa yupo kwa mama yake mzazi, Kivule, Dar.
Msome shemeji mtu hapa: “Siku moja nikiwa katika safari zangu za usiku, nilimuona Farida akiwa na kijana anayeitwa Chidi.
“Niliamua kuwafuatilia nyendo zao kwa vile tayari tabia yake ilikuwa inajulikana. Niligundua kuwa alikuwa anaishi na kijana huyo kwenye chumba kimoja ambacho mwanamke huyo ndiye aliyekipanga. Hebu fikiria mke anapanga chumba nje ili awe anasalitia!”
Shemeji mtu huyo akaendelea kusema kuwa baada ya kukigundua chumba hicho, yeye na ndugu wengine walikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Saidi Juma Mpili ambaye aliwathibitisha kuwa ni kweli Farida anaishi na Chidi japokuwa chumba kilipangishwa kwa jina la mtu mwingine.
 
MTEGO WAWEKWA
Baada ya kuthibitishiwa hivyo, familia hiyo iliwasiliana na mapaparazi kwa lengo la kuwanasa wawili hao ambao kwa muda huo walikuwa mitaani wakitanua.
Kwa ushirikiano wa familia, mapaparazi na mjumbe huyo mtego uliwekwa na baada ya muda Chidi na Farida waliwasili wakiwa kwenye pikipiki bila kujua wako ndani ya kumi na nane ya wakwe zake.
 
WABANWA LAIVU
Nje ya nyumba hiyo, wawili hao walibanwa na kuulizwa uhusiano wao ambapo Chidi alisema yeye ni kaka wa hiyari wa Farida na kukataa kwamba wanaishi pamoja, utetezi ambao uliwapandisha hasira wakwe hao na kumwomba mjumbe wapekue chumbani ili kujiridhisha kuwa hawaishi pamoja.
 
FARIDA AWAPOTOSHA WAKWE ZAKE
Farida ndiye aliyeongoza msafara wa kuingia ndani akifuatiwa na jamaa yake, lakini cha ajabu aliwapotosha ndugu wa mume kwa kuwaingiza ndani ya chumba cha mpangaji mmoja akidai ni chake, jambo ambalo lilishtukiwa na mapaparazi wetu waliokuwa wameshafanya uchunguzi wa kutosha kabla.
Farida aliambiwa chumba hicho sicho, wakamtaka aoneshe chake ndipo akaenda kuingia huko ambako zilionekana suruali aina ya ‘jeans’ za Chidi na makoti mengi ya kuendeshea bodaboda ambayo yalitoa ushahidi kuwa watu hao wanaishi pamoja humo.
 
BAADA YA UTHIBITISHO, MUME AJULISHWA KWA SIMU, ALIA
Kufuatia ushahidi huo na Farida mwenyewe kukiri, ndugu walimwendea hewani mume wa mwanamke huyo, yaani Ally na kumtumbulia siri hiyo nzito ambapo alilia kwenye simu.
 
HUENDA ILIKUWA HIVI
Katika kupashana huko, huenda kaka mtu ndiye aliyepiga simu na kusema hivi:
“Haloo dogo.”
Ally: Ee bro, shikamoo.”
“Marhaba. Nakutaarifu kuwa tumemfumania mkeo akiwa kwa kijana mwendesha bodaboda.”
Ally: Nini? Kweli bro?
Bro: Kweli dogo, hivi ninavyoongea na wewe tupo hapa, mama, mama mdogo na sista.
Ally: (kilio).
 
ALICHOKISEMA MUME
Akizungumza baada ya kupata taarifa za kubambwa  kwa mke wake na Chidi, mume wa Farida alisema akiwa nchini Kongo mkewe alimuaga anakwenda kwa mama yake Kivule na hatambui kama alikuwa amepanga chumba na kuishi na mwanaume mwingine, jambo alilosema limemshangaza sana.
Ally akaulizwa atachukua uamuzi gani baada ya tukio hilo, akajibu huku akilia na kusema atarejea Bongo kumaliza suala hilo mwenyewe kisha akakata simu huku sauti ya kilio ikimalizikia kusikika kwa mbali hali iliyowafanya ndugu zake washikwe na  huzuni.
 
FARIDA AOGOPA KUONDOKA NA WAKWE ZAKE
Baada ya tukio zima kukamilika, Farida aligoma kuondoka na wakwe zake akidai kwamba anahofia watakwenda kumpiga au kumfanyia jambo lolote baya kutokana na kitendo alichomfanyia mtoto wao, lakini akafunguka kwamba bado anampenda mumewe na hataki kupewa talaka.

AIBU:- NDOA YASAMBARATIKA KANISANI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUIDHINISHWA



Hili  ni  tukio  la  kusikitisha, lakini  lenye  mafunzo  kibao  ndani  yake.Tukio  hilo  lilitoke  mwanzoni  mwa  mwezi wa  nane  mwaka  huu ndani  ya  kanisa  la Pentekoste  la  nchini  Kenya  ambapo  wanandoa  wawili    walikuwa  wakila  kiapo  cha  maisha  mbele  ya  mchungaji  wa  kanisa hilo.


Dakika  chache  kabla  ya  wanandoa  hao  kuapishwa  na  kuruhusiwa  kuvishana  pete, Mchungaji  wa  kanisa  hilo   aliwauliza  waumini  kama  kuna  yeyote  mwenye  pingamizi  la  kufungwa  kwa  ndoa  ya  wapenzi  hao...

Baada  ya  swali  hilo, mwanamke  mmoja  alisimama  na  kuelekea  mbele  ya  kanisa  hilo  huku  akiwa  na  vyeti  mkononi.

Alipomkaribia  mchungaji, mwanamke  huyo  alipaaza sauti  yake  na  kusema  kuwa  ndoa  hiyo  haistahili  kufungwa  kwa  sababu  yeye  na  bwana  harusi  wanamtoto  waliyemzaa  pamoja  na  kwamba  walikuwa  na  mipango  ya  kuoana....


ANGALIA VIDEO HAPA:

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA EUROPA JANA.

Europa League - Group ASeptember 19
FTSt.Gallen2 - 0Kuban Krasnodar
FTValencia0 - 3Swansea City
Europa League - Group BSeptember 19
FTDinamo Zagreb1 - 2Chornomorets O.
FTPSV Eindhoven0 - 2PFC Ludogorets Razgrad
Europa League - Group CSeptember 19
FTSalzburg4 - 0Elfsborg
FTStandard Liege1 - 2Esbjerg fB
Europa League - Group DSeptember 19
FTMaribor2 - 5Rubin Kazan
FTZulte-Waregem0 - 0Wigan Athletic
Europa League - Group ESeptember 19
FTFiorentina3 - 0P.Ferreira
FTPandurii0 - 1Dnipro
Europa League - Group FSeptember 19
FTEintracht Frankfurt3 - 0Bordeaux
FTMaccabi Tel Aviv0 - 0APOEL Nicosia
Europa League - Group GSeptember 19
FTDynamo Kyiv0 - 1Genk
FTThun1 - 0Rapid Wien
Europa League - Group HSeptember 19
FTEstoril1 - 2Sevilla
FTFreiburg2 - 2Liberec
Europa League - Group ISeptember 19
FTReal Betis0 - 0Lyon
FTVitoria de Guimaraes4 - 0Rijeka
Europa League - Group JSeptember 19
FTApollon Limassol1 - 2Trabzonspor
FTLazio1 - 0Legia Warszawa
Europa League - Group KSeptember 19
FTFC Sheriff0 - 0Anzhi Makhachkala
FTTottenham Hotspur3 - 0Tromsø
Europa League - Group LSeptember 19
FTMaccabi Haifa0 - 1AZ Alkmaar
FTPAOK Thessaloniki FC2 - 1Shakhter Karagandy

Wednesday, 18 September 2013

TAZAMA VIDEO JINSI WACHAWI WALIVYONASWA WAKIWANGA TENA WAKIWA WATUPU KAMA WALIVYOZALIWA (18+)



Tazama jinsi wanavyoona aibu, Shuhudia video ya tukio zima tongea wakiwa wanawanga mpk kukamatwa kwao.     <<TAZAMA VIDEO HAPA(18+)

KIJIJI MAARUFU KWA KUUZA MADAWA YA KULEVYA CHAGUNDULIKA HUKO KUNDUCHI


JIJI la Dar es Salaam lina mambo mengi lakini moja ambalo linatisha ni kugundulika kwa kijiji cha madawa ya kulevya ambacho kipo kando ya Bahari ya Hindi.
Kijiji hicho ni Kunduchi, nje kidogo ya jiji na uchunguzi umeonesha kuwa, madawa ya kulevya yenye thamani ya mabilioni ya shilingi yamekuwa yakikamatwa katika eneo hilo. 
Baadhi ya wananchi waliozungumza na kwa sharti la kutoandikwa majina yao , walisema matajiri wengi wa ‘unga’ wamekuwa wakitumia eneo hilo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni salama kwa shughuli hiyo.
“Hapa Kunduchi ni kando ya bahari, wengi wanatumia majahazi au boti za uvuvi kuingiza mihadarati hiyo. Wanapoleta madawa yao wanaonekana kama wanatoa samaki au mizigo mingine ya kawaida lakini kumbe ni madawa ya kulevya,” alisema kijana mmoja.
Mzee wa siku nyingi wa kijiji hicho alisema anasikitishwa kuona kuwa kitongoji chao kimekuwa makao makuu ya biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya na yanauzwa wakati serikali ipo.
“Kuna wakati tulitaka sana kijengwe kituo cha polisi lakini tukaambiwa kuna matajiri hawataki hilo, hivyo ajenda hiyo ikaisha na wengi tunaamini matajiri kwa kutumia fedha hawaruhusu kituo cha polisi kuwepo eneo hilo ndiyo maana hakijengwi,” alisema mzee huyo na kuongeza kuwa Kituo cha Polisi cha Silver Sands kiko mbali sana.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa watuhumiwa wengi wa madawa hayo haramu wanakamatiwa katika kijiji hicho.
Kwa mfano, Fred William Chande na wenzake wanane waliwahi kukamatwa kwa madai ya kuwa na madawa hayo aina ya heroin yenye thamani ya shilingi bilioni 6.4 Februari 21, 2011 na tayari wamefunguliwa kesi namba 1/ 2012 Mahakama Kuu ya Tanzania.

Chanzo kingine cha habari kilidai kuwa hata madawa aina ya Crystal Methamphetamine kilo 150 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8 walizokamatwa nazo Agness Jerald ‘Masogange’ na Melisa Edward nchini Afrika Kusini chimbuko lake ni Kunduchi.

Naye Mwanaidi Ramadhan na wenzake wanane wanadaiwa kukamatwa na madawa aina ya heroin yenye gramu 2,083.3 ambayo thamani yake ni mamilioni ya shilingi, eneo la Mbezi Beach Kata ya Kunduchi, Dar na tayari polisi wamewafungulia kesi mahakama kuu ambapo jalada lao ni namba 10/2012. Walikamatwa Juni 1, 2011.
Naye Ally Murzai Pirbakshy ‘Haji’ na wenzake watatu walikamatwa wakidaiwa kuwa na madawa aina ya heroin yenye thamani ya mamilioni ya shilingi na uzito wa gramu 3,053.5 Septemba 7, 2011. Nao wamefikishwa mahakama kuu na kufunguliwa kesi namba 10/2012.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Godfrey Nzowa alipoulizwa juu ya kijiji hicho alisema polisi wamekuwa wakifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wananchi na matokeo yake yamekuwa mazuri.
 “Yeyote ambaye ana habari juu ya wanaofanya biashara hiyo aje kuniona na njia ya bahari tunaidhibiti, wasijidanyanye kuitumia kwani kuna wenzao walifanya hivyo Lindi tukawakamata, ”alisema Nzowa.

PICHA:SERENGETI FIESTA ILIVYOWASHIKA WAKAZI WA MOROGORO JUMAPILI



IMG_6216
Msimu wa Fiesta mwaka 2013 unaendelea kwenye mikoa tofauti ya Tanzania, jumapili ya tarehe 15/9 show ilikua mkoani Morogoro. Lakini kama kawaida ya msimu wa mwaka huu Fiesta unaenda sambamba na semina ya fursa. Angalia hapa picha za show nzima na semina ya fursa zilivyoenda.
Kwa Updates Mbali mbali za Serengeti Fiesta jiunge na Official Facebook Page ya Serengeti kwa Kuclick Hapa : https://www.facebook.com/serengetipremiumlager
ssswwwDj Zero akiwa kazini
ssas (2)My boss Mr Sebastian Maganga,mdau,Mr Lee kutoka Clouds TV na mdau mwingine
ssas (1)
sdsssNey Lee
IMG_6156  Anorld Kayanda,Gea Habib,mdau na MpokijWatu walikuwa ni wengi kama kawaida ya show za fiesta
k
IMG_6092
Recho akiwa na madancer wake
IMG_5824Mwasiti akizungumza kwenye semina ya Fursa
IMG_5799Baadhi ya watu waliofika kwenye semina
IMG_5789Mrisho Mpoto akitoa maneno yake kwenye semina
IMG_5748
12Mbunifu wa mavazi kutoka Morogoro alipata nafasi kwenye semina ya fursa
7
8
asw
fff
9Nikki wa pili akizungumza kwenye semina ya fursa
10
IMG_2128
IMG_2284
11
1
2
3
4
6Picha zote na michuzijr.blogspot.com