August 17, 2018 Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda leo amefungua semina ya kimkakati iliyoandaliwa na TCRA inayolenga kulifanya jiji la DSM kuwa katika mpangilio wa kisasa na kuhakikisha mitaa yote inawekwa katika mfumo wa anwani za makazi na Postcode.
RC Makonda amesema Mfumo huo ni ukombozi kwa wananchi kwakuwa utarahisisha huduma na kuwezesha kila mwananchi kuwa na anwani, kuwasaidia wageni kujua maeneo, kudhibiti wezi na matapeli, na kusaidia Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika haraka kwenye eneo lenye tukio.
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishangiliwa na abiria wa ndege yetu Boeing 787-8 Dreamliner ya Air Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza asubuhi ya leo Agosti 18, 2018. Amepata nafasi ya kuwasalimu abiria na wamempongeza kwa juhudi zake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametoa mwezi mmoja kwa wanaume waliotelekeza watoto wilayani humo kuhakikisha wanaanza kutafuta watoto wao na kuanza kuwahudumia .
Dc Muro amesema baada ya muda aliotoa kuisha ataanza kuwakaribisha Wanawake wote wanaoishi wilayani humo waliotelekezewa watoto kupeleka Malalamiko yao ofisini kwake.
Muro alitoa maagizo hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya utelekezji wa watoto wilayani humo, amesema lengo la zoezi hilo ni kupunguza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hatarishi na wanaojihusisha na uhalifu na wale wanaozurura na kuzagaa mitaani kwa kukosa malezi ya Wazazi wawili.
“Nichukue fursa hii kuwataarifu akina mama na akina dada waliozalishwa na kutelekezewa watoto na kuachwa wabebe mzigo wa kuwahudumia watoto wako, natoa mwezi mmoja kwa kila mwanaume anayejua huko Arumeru aanze kutafuta mtoto aliyemtelekeza”amesema Muro
” Nitoe rai tu najua wako watu watakaokaidi naomba wajifunze kupitia zoezi lililofanyika DSM likiongozwa na RC Paul Makonda zoezi la Arumeru nitakuwa mkali zaidi kuliko la Dar, wajue zoezi limeisha huko na limetua Arumeru.”
Mara nyingi kwenye maisha ukiwauliza watu waliofanikiwa safari yao ilikuaje basi lazima watakueleza jinsi walivyo anzia chini mpaka kufikia mafanikio hayo, Novati Tenga ambaye ni mchaga mwenye taaluma ya uhasibu ambaye ameelzea safari yake ya utafutaji ilipoanzia mpaka sasa kumiliki kampuni ya kuuza magari.
Bonyeza PLAY hapa chini kumtazama Novati akisimulia.
Ligi ya Serie A haiwezi ikawa ni ya mtu mmoja tu, haijawahi kuwa hivyo na haitakaa kuwa ya Cristiano Ronaldo pekee.
Hatahivyo, ni ngumu sana kudharau namna gani kuhamia kwake katika timu ya Juventus kumeleta kishindo katika ligi hiyo hata kabla ya mpira kuanza kuchezwa.
Ronaldo mwenye miaka 33 na mshindi mara tano wa tuzo za mchezaji bora wa dunia, Ballon d'Or, si tu ni mmoja ya wachezaji bora wawili wa mpira wa miguu katika mwongo uliopita bali ni mmoja ya watu maarufu kabisa duniani kwa sasa.
Katika mitandao ya kijamii, Ronaldo anawafuasi milioni 313 na yawezekana kabisa umati huu mkubwa wa watu sasa utaelekeza macho na masikio yao kuelekea Serie A.
"Hatimaye dunia inaiongelea ligi ya Italia tena," kocha maarufu wa Italia Fabio Capello ameliambia gazeti la Gazzetta dello Sport. "Katika miaka ya 80 na 90 sisi (Italia) tuliwakilisha ubora na umaarufu, halafu tukapotea na tukashindwa kuwekeza katika miundombinu ya kuturudisha juu."
"Kwa kuwa na Ronaldo sasa twaweza kujaribu kunyanyua vichwa juu, lakini hilo pekee halitoshi, tunahitaji kutumia weledi wa hali ya juu kutumia mshawasha wa Ronalso ili kuupa mchezo wetu uhai kwa mara nyengine," amesema Capello.
Makubaliano katika vyombo vya habari ni kuwa uhamisho wa Ronaldo kutoka Real Madrid ya Uhispania kwenda Juve uliogharimu pauni milioni 99.2 ni hatua muhimu zaidi iliyochukuliwa katika harakati za kuirejesha Serie A katika umaarufu wake wa zamani.
"Kilele klilikuwa mwaka 2003 pale tulipoingiza timu zetu mbili katika fainali ya klabu bingwa bara Ulaya," amekumbushia kocha wa zamani wa Juve Claudio Ranieri, alipoongea na gazeti la Stampa. "Hatujarejea katika zama zile bado, lakini nahisi siku za unyonge zimefikia tamati."
Ni dhahiri kuwa Tanzania na Marekani zimeingia katika majibizano ya kidiplomasia kutokana na mwenendo wa chaguzi ndogo zilizofanyika mnamo Agosti 12.
Taarifa ya ubalozi wa Marekani Agosti 15 jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Buyungu na kata za udiwani 36 ulikumbwa na kasoro nyingi.
Tamko la ubalozi ambalo wameliita la 'masikitiko' limetaja kasoro hizo kuwa ni vurugu zilizohusiana na uchaguzi, ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani.
Kasoro nyingine zilizotajwa na ubalozi huo ni vitisho vya polisi dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani, watu kukamatwa kiholela bila kuwepo vibali vya ukamataji na kukandamizwa kwa uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni katika kipindi chote kuelekea chaguzi hizo.
"Mambo haya yanakwaza haki ambazo Katiba ya Tanzania imewapa raia wake na kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini na katika eneo lote la kanda," ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliibua Tume ya Uchaguzi (NEC) klicha ya kukanusha tuhuma hizo ilihoji uhalali wa Marekani kuhoji juu ya uendeshwaji wa chaguzi ndogo nchini Tanzania.
Taarifa ya NEC imesema kuwa hapakuwa na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa na kuutaka ubalozi wa huo uleleza umepata vipi taarifa hizo na kwa kutumia utaratibu na sheria gani.
"…Buyungu mgombea wa ubunge mmoja wapo (Chadema) alijitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii akaeleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo…" inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza, "Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani, mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura."
Taarifa ya NEC pia imesema hakuna chama chochote cha siasa kilichojitokeza na kuthibitisha kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki.
Hata hivyo, Chama ca ACT-Wazalendo hata kabla ya matamko ya ubalozi na NEC walitoa tathmini yao na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo kimesema haitatumia mabavu wakati wa uchaguzi.
Chama hicho kimetoa kauli hiyo kikidai kuwa uchaguzi huo wa mdogo wa Agosti 12 ulivurugwa.
CCM ilishinda kiti cha ubunge Buyungu na kata 77. Hatahivyo kati ya kata 77, uchaguzi umefanyika katika kata 36 tu huku katika kata 41 wagombea wa CCM walipia bila kupingwa.
Je, Marekani imeingilia mambo ya ndani ya Tanzania?
Ni mwiko kidiplomasia kwa nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine, lakini je, Marekani imeingilia mabmbo ya ndani ya Tanzania kwa tamko lao?
Akijibu swali hilo, mhadhiri wa sayansi ya siasa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt Richard Mbunda amesema japo hatua hiyo ya Marekani kidiplomasia ni ya kushtua, lakini haishangazi.
"Marekani wamekuwa wakijipambanua duniani kote kama walinzi wa demokrasia, hivyo haishangazi wao kutoa tamko juu ya jambo hili," amesema Dkt Mbunda na kuongeza "uchaguzi huu na kishindo chake ni sehemu tu ya wimbi kubwa la kisiasa linaloendelea nchini, ikiwemo kuhama kwa viongozi wa upinzani kwenda CCM. Wimbi hili limekuwa likitiliwa shaka juu ya uhalali wake na kama kama ni kweli sababu pekee ya hama hama hiyo ni kutekeleza utashi wa wanasiasa hao unaolindwa kikatiba."
Mhadhiri wa masuala ya diplomasia kutoka kituo cha diplomasia (CFR) Dar es Salaam Godwin Gonde, ameiambia BBC kuwa tathmini yake ni kuwa Marekani ilikuwa na mengi ya kusema juu ya hali ya kisisasa nchini Tanzania lakini ilikuwa ikitafuta upenyo.
"Tamko lao (ubalozi wa Marekani) halibadili matokeo ya chaguzi, bali wanajaribu kuiambia serikali kuwa wapo macho na wanatazama kila kinachoendelea."
Gonde amesema katika hali ya kawaida, balozi ama jumuiya ya kimataifa haingalii chaguzi ndogo na ndio maana Marekani hawakutoa tamko lao wakati hatua za uchaguzi zikiendelea kwa sababu hawakuwepo kwenye maeneo ya uchaguzi.
"Tafsiri ya wazi ni kuwa wameingilia mambo ya ndani ya Tanzania, wameeleza sababu zao, lakini hapa itategemea na serikali ya Tanzania itataka kuliendea jambo hili, inaweza ikawa ni mwanzo wa msuguano."
Aliyekua rais wa Uruguay Jose Mujica, aliyejulikana kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.
Mujica aliacha kazi ya useneta mnano Jumanne, kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumua kama raisi ukamilika mwaka wa 2015.
Alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mrengo wa kushoto ana miaka 83.
Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema ya kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.
Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya inafanya kazi.
Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.
Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi.
Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye ikulu ya rais.
Wakati akiwa rais na hata sasa, yeye pamoja na mkewe, ambaye pia alimusaidia katika vita vya msituni wamekua wakiishi katika shamba moja nje ya kidogo mwa mji wa Montevideo.
Alitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.
Gari hilo lilipata umaarufu na mwaka 2014 alipewa dola milioni moja lakini akataa huku akidai kuwa atashindwa kumbeba mbwa wake mwenye miguu mitatu.
Kuacha kazi kwa Mujica hakukupokelewa na mshangao kwa sababu alikua amedokeza kufanya hivyo mnano Agosti 3 alipofika mara ya mwisho seneti.
Ubongo umegawanyika katika hemispheres mbili, left side na right side, watu wanaotumia upande wa kulia control huwa inatoka left side of the brain, sasa ukija kwa left handers control inatoka right side of the brain. Ambayo watu left handers ni special cases mostly ether by inheritance au genetical make up kama ilivyo swala la mapacha... What to note is that wazazi wengi huwa wanawadescourage watoto wao wanapojua ni mashoto THIS IS NOT RIGHT inakuja kumsababishia matatizo mengi sana ikiwemo tatizo la kumbukumbu na ugumu wa vitu kama mahesabu...So cha kufanya ni kumuacha na kumtafutia vifaa ambavyo vina encourage left handedness mfano mlango wa chumba chake uwekwe tofauti na mingine, na baadhi ya vifaa kama mikasi iliyotengenezwa maalum kwa left hand people...watu wengi wa namna hiyo huwa wana uwezo mkubwa ,sana katika sayansi, mahesabu kama hawatakuwa discouraged na pia wana uwezo mkubwa sana kimichezo na hasa kama ni wasichana wanakuwa na extraordinary capacity of learning.
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah anachunguzwa na polisi baada ya video yake kuibuka akionekana kuendesha gari akiwa bado anatumia simu.
Klabu yake inadaiwa kuwa ndiyo iliyopiga simu kwa polisi.
Polisi wa Merseyside wamethibitisha kupitia ujumbe wa Twitter kwamba video hiyo imekabidhiwa kitengo husika.
Msemaji wa Liverpool amesema waliwafahamisha polisi kuhusu video hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji huyo.
Ameongeza kwamba hatua zozote zinazohitajia kuchukuliwa kuhusu tukio hilo zitachukuliwa kwa kufuata mifumo ya ndani.
Video hiyo ambayo imesambazwa sana kwenye Twitter inaonekana kumuonesha mchezaji huyo, akiwa anatumia simu yake akiwa amelisimamisha kwa muda huku akiwa amezingirwa na mashabiki, wakiwemo watoto. Kisha analingurumisha gari na kundoka akiwa bado anaitumia simu yake.
Msemaji wa klabu hiyo amesema: "Klabu, baada ya kushauriana na mchezaji, imewafahamisha Polisi wa Merseyside kuhusu kanda hiyo ya video na matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kupigwa kwa video hiyo."
"Tumezungumza na mchezaji huyo na tutashughulikia hatua nyingine zozote zinazohitajika kuchukuliwa kwa kutumia mifumo ya ndani.
"Hakuna yeyote kati ya klabu na mchezaji ambaye atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hili."
Raia huyo wa Misri aliwafungia Liverpool magoli 44 msimu uliopita.
Mo Salah alifunga bao Jumapili katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England msimu huu ambapo aliwasaidia Liverpool kuwalaza West Ham 4-0.
Mabao hayo mengine yalifungwa na Sadio Mane (mawili) na Daniel Sturridge.
Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine anadai kuwa dereva wake ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi akiwa ndani ya gari la mbunge huyo.
Mbunge huyo wa Kyadondo aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa walikuwa eneo linalojulikana kama Arua kwenye kampeni wakati mauaji hayo yalitokea.
Uchaguzi mdogo unatarajiwa kuandaliwa eneo hilo siku ya Jumatatu katika juhudi za kumtafuta yule atakayechukua mahala pake mbunge aliyeuawa Ibrahim Abiriga .
Bobi Wine na viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa eneo hilo kumuunga mkono mgombea huru Kassiano Wadri.
Mikutano hiyo ilienda sawa siku yote kabla ya polisi kuanza kukabiliana na wafuasi wa Wadri.
Wafuasi wa Wadri nao waliripotiwa kukabiliana na wale wa mgombea wa NRM Tiperu Nusura.
Bobi Wine pia aliandika kuwa hoteli yake ilizingirwa na polisi kufuatia visa hivyo.
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wafuasi wa upinzani watalaumiwa kwa kuuliwa dereva huyo wa Bobi Wine Yasin Kawuma.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima, anasema watu waliokuwa wamevaa shati za kampeni za mgombea Wadri, walianza kuurushia mawe msafara wa rais hali ambayo ilisababisha polisi kufyatua risasi.
"Mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni msafara wa rais ulishambuliwa na wahuni katika manispaa ya Arua wakati rais alikuwa anaondoka uwanja wa Boma ambapo alikuwa amefanya mkutano wa mwisho," Kayima alisema.
Tanzania imetajwa na Benki ya Dunia kuwa miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo yamefanikiwa pakubwa kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini.
Kwenye ripoti ya benki hiyo kuhusu usawa duniani, Tanzania imeorodheshwa pamoja na Cambodia na Brazil kama nchi tatu zilizopiga hatua sana.
Nchini Tanzania, ripoti hiyo inasema, ufanisi ulipatikana katika kipindi ambacho taifa hilo lilipata ukuaji thabiti wa uchumi wa kiwango cha wastani cha asilimia 6.5 kila mwaka kati ya 2004-2014.
"Kiwango cha umaskini kitaifa kilishuka kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012," ripoti ya benki hiyo inasema.
Kwenye kipimo cha pengo kati ya maskini na matajiri, Tanzania iliimarika kutoka alama 39 mwaka 2007 hadi chini ya alama 36 mwaka 2012.
Kipimo cha wastani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2015 kilikuwa alama 45.1.
"Hatua zilizopigwa na Tanzania katika kupunguza pengo kati ya maskini na matajiri kipindi hiki kifupi ni cha kutia moyo," Benki ya Dunia inasema.
"Ushahidi unaonesha ufanisi huu ulitokana sana na ongezeko la matumizi miongoni mwa watu wa tabaka la chini."
Miongoni mwa asilimia 40 maskini, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 60 wenye pesa ambao ongezeko lao la matumizi lilikuwa asilimia 1 pekee.
"Ni wazi kwamba mambo yaliwaendea vyema zaidi watu maskini kuliko matajiri kipindi hiki," ripoti hiyo inasema.
Kuanzia mwaka 2007, kulikuwa na ongezeko katika biashara ya rejareja na viwanda, hasa vya vyakula, vinywaji na tumbao jambo ambalo benki hiyo inasema liliwezesha watu wasio na ujuzi sana kushiriki katika uchumi.
Kujitolea kwa serikali katika kuendeleza sera ambazo zinalenga kusawazisha mapato pia kumechangia Tanzania kupiga hatua, benki hiyo inasema.
Moja ya sera hizi ni mkakati wa serikali wa kuimarisha kupatikana kwa huduma za msingi kama vile afya, elimu ya msingi, maji na usafi miongoni mwa watu maskini.
Pili ni Mfuko wa Maendeleo wa Tanzania ambao benki hiy inasema umesaidia jamii maskini kuweka akiba na kuwekeza hasa katika mifugo.
Hata hivyo, benki hiyo imesema Tanzania inafaa kufanya juhudi zaidi kupunguza tofauti kati ya mikoa pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimsingi. Juhudi zaidi zinahitajika katika upatikanaji wa umeme na huduma za usafi.
Mji wa Harare, Zimbabwe ni miongoni mwa miji ambayo haivutii kwa watu kuishi duniani.
Ni mara ya kwanza kwa jiji la bara Ulaya kuongoza kwenye orodha hiyo ya kila mwaka ambayo huandaliwa na Kitengo cha Uchunguzi cha Jarida la Economist.
Utafiti huo uliorodhesha miji 140 duniani kwa kufuata vigezo mbalimbali vikiwemo uthabiti wa kisiasa na kijamii, visa vya uhalifu, elimu na kupatikana kwa huduma bora ya afya.
Katika utafiti huo, jiji la Manchester ndilo lililoimarika zaidi miongoni mwa miji ya Ulaya ambapo jiji hilo lilipanda hatua 16 hadi nafasi ya 35.
Jiji hilo limo mbele ya London kwa hatua 13, ambalo ndilo pengo kubwa zaidi kwa miji hiyo miwili kwenye orodha hiyo tangu kuanza kuandaliwa kwa orodha hiyo miongo miwili iliyopita.
Jarida la Economist limesema kuimarika kwa Manchester ni kwa sababu ya kuimarishwa kwa usalama.
'Ukakamavu'
Utafiti huo ulikosolewa mwaka jana kwa kuushusha hadhi mji wa Manchester baada ya shambulio la Manchester Arena ambapo watu 22 waliuawa.
Mwaka huu, mhariri wa utafiti huo Roxana Slavcheva amesema jiji la Manchester "limenyesha ukakamavu na kujikwamua kutoka kwa shambulio hilo la kigaidi ambalo lilikuwa imetikisa uthabiti wake.
Bi Slavcheva amesema usalama pia umeimarika katika miji kadha ya Ulaya magharibi.
Kuongoza kwa Vienna ni iashara ya kurejea kwa utulivu kiasi katika maeneo mengi ya Ulaya.
Kwa mujibu wa utafiti huo, karibu nusu ya miji imeimarika katika mwaka mmoja uliopita.
Melbourne, ambao kwa sasa ni mji wa pili duniani kwenye orodha hiyo, ilikuwa imeongoza kwa miaka saba mfululizo.