Ligi ya Serie A haiwezi ikawa ni ya mtu mmoja tu, haijawahi kuwa hivyo na haitakaa kuwa ya Cristiano Ronaldo pekee.
Hatahivyo, ni ngumu sana kudharau namna gani kuhamia kwake katika timu ya Juventus kumeleta kishindo katika ligi hiyo hata kabla ya mpira kuanza kuchezwa.
Ronaldo mwenye miaka 33 na mshindi mara tano wa tuzo za mchezaji bora wa dunia, Ballon d'Or, si tu ni mmoja ya wachezaji bora wawili wa mpira wa miguu katika mwongo uliopita bali ni mmoja ya watu maarufu kabisa duniani kwa sasa.
Katika mitandao ya kijamii, Ronaldo anawafuasi milioni 313 na yawezekana kabisa umati huu mkubwa wa watu sasa utaelekeza macho na masikio yao kuelekea Serie A.
"Hatimaye dunia inaiongelea ligi ya Italia tena," kocha maarufu wa Italia Fabio Capello ameliambia gazeti la Gazzetta dello Sport. "Katika miaka ya 80 na 90 sisi (Italia) tuliwakilisha ubora na umaarufu, halafu tukapotea na tukashindwa kuwekeza katika miundombinu ya kuturudisha juu."
"Kwa kuwa na Ronaldo sasa twaweza kujaribu kunyanyua vichwa juu, lakini hilo pekee halitoshi, tunahitaji kutumia weledi wa hali ya juu kutumia mshawasha wa Ronalso ili kuupa mchezo wetu uhai kwa mara nyengine," amesema Capello.
Makubaliano katika vyombo vya habari ni kuwa uhamisho wa Ronaldo kutoka Real Madrid ya Uhispania kwenda Juve uliogharimu pauni milioni 99.2 ni hatua muhimu zaidi iliyochukuliwa katika harakati za kuirejesha Serie A katika umaarufu wake wa zamani.
"Kilele klilikuwa mwaka 2003 pale tulipoingiza timu zetu mbili katika fainali ya klabu bingwa bara Ulaya," amekumbushia kocha wa zamani wa Juve Claudio Ranieri, alipoongea na gazeti la Stampa. "Hatujarejea katika zama zile bado, lakini nahisi siku za unyonge zimefikia tamati."
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg