MCHEZAJI mpya aliyesajiliwa na Manchester United kutoka Crystal Palace, Wilfred Zaha alijikuta akiwa kituko na kutia aibu pale alipotinga Uwanja wa ndege na mavazi ya” kibrazamen” wakati wenzake walitakiwa kuvaa suti kama sare ya kuwatambulisha walipokuwa wakijiandaa kuondoka kwa ajili ya ziara yao ya kujiandaa na msimu unaokuja.
Alipoulizwa kuhusu wapi alipoacha vazi hilo Zaha hakukumbuka na ndipo msaada wa kumsaidia kutoka kwa maofisa wa Manchester kuanza kushughulikiwa
Hali hiyo ilimfadhaisha mchezaji huyo na kutaka kupanda ndani ya gari lake kuondoka na ndipo akasaidiwa na maofisa wa klabu hiyo waliompatia vazi hilo na kulitinga kabla ya safari hiyo.
Ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara na klabu hiyo toka asajiliwe zaha alijikuta kama mtu mwenye mwanzo mbaya lakini tatizo hilo liliisha mara baada ya kupewa suti nyingine alizozitinga na kupendeza.
ZAHA AKIINGIA UWANJA WA NDEGE NA BEGI LAKE AKIWA NA MAVAZI YASIYO RASMI KWA SAFARI. |
ZAHA AKIWA NA FURAHA MARA BAADA YA KUVAA VAZI LA SUTI LIOLILOWEZA KUMLIONGANISHA NA WENZAKE |