Semina za Fursa Twenzetu ambazo hutangulia kabla show za Fiesta, leo hii inafanyika Mwanza. Lulu ni mmoja kati ya wazungumzaji katika semina ya Mwanza. Wazungumzaji wengine wanaotegemewa kuzungumza ni DPP of Clouds Media Group Mr Ruge Mutahaba,Mrisho Mpoto,Nikki wa Pili...
Saturday, 28 September 2013
MAMBO YA LIKIZO YA VYUO....DENT AAMUA KUMTUMIA MPENZI WAKE PICHA ZA UTAMU NA KUAMBULIA KUZAGAA MTANDAONI
RAY C AMZIMIKIA "ABDUL HAJI" SHUJAA WA WESTGATE ALIYE OKOA WATU WENGI KUTOKA MIKONONI MWA MAGAIDI
Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.
“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.
“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.
Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”
Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.
Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.
Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo.
SAKATA ZIMA LA MWANAMKE WA KITANZANIA ALIYEAMUA KUUGEUZA MWILI WAKE KUWA KITEGA UCHUMI HUKO UGHAIBUNI....
Wengi waliyaamini madai hayo kutokana na ujasili aliokuwa nao wakati akiieleza dunia kuhusu tendo la ubakwaji alilotendewa....
Hakika jambo usilolijua ni kama usiku wa giza...Amini usiami, mwanamke huyu hakubakwa .Ujasili wake ulikuwa ni mchezo wa kuigiza na tayari mtandao huu umefanikiwa kupata sehemu ya mchezo huo ambao ni komedi tupu.
Baada ya mchezo huo kukosa mafanikio na hali ya maisha kuwa ngumu kifedha, mtandao huu umedokezwa kuwa Florah amejikuta akiwa ni mtumwa wa mwili wake ndani ya nchi za watu....
Utumwa huo unadaiwa kutokana na kitendo cha yeye kuugeuza mwili wake kuwa kitega uchumi..
Zifuatazo ni picha chafu za mwanamke huyo ambazo zimekuwa zikitundikwa katika mtandao wake kwa lengo la kujiongezea wateja....
PICHA YA KWANZA: << BOFYA HAPA>>
PICHA YA PILI: << BOFYA HAPA >>
PICHA YA TATU: << BOFYA HAPA>>
Monday, 23 September 2013
HUYU NDIYE MWANAMKE ADAIWA NDIO KIONGOZI WA MAGAIDI WA AL SHABAAB WALIOTEKA WESTGATE MALL KENYA
Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.
Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.
Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch @watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.
Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo
Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.
Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza kuhusika na shambulio la jana.
Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?
Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.
Akitokea Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.
Mwezi May hati ya kumkamata ilitolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani nchini Kenya kwa kesi ya kutengeneza bomu.
TAZAMA PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ AKILA BATA MALAYSIA
Posted by Boss Ngasa at 11:21
MSANII WA BONGO FLEVA SAM WA UKWELI AELEZEA JINSI ALIVYOMUUA MDOGO WAKE BILA KUKUSUDIA
Sam anasema kuwa baada ya hapo baba huyo wa kufikia alisema sam kamuua mwanae maksudi na kuleta mtafaruku mzito katika familia yao jambo lililosababisha ndoa hiyo kuvunjika na wakarudi kwa bibi yake mzaa mama na ndipo walipokuja kushangaa baada ya baba yao mzazi ambae waliambiwa kafa kurudi nyumbani akiwa mzima kabisa na ndio safari ya kuja dar kwa mara ya kwanza.
TAFSIRI YA KISWAILI YA MAHOJIANO YA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA UVAMIZI NA MAUAJI YA WATU KENYA
Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.
JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu. Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.
JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo. Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.
JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?
Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.
JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?
Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?
Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.
JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?
Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia. Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya.
HAWA NDIO WASHINDI WA TUZO ZA TANZANIAN BLOG AWARDS:
Nashukuru sana kwa wote waliopigia kura blog yetu ya bossngasa.com na kufanya kuwa mshindi wa kwanza katika Category ya the best newcomer blog,shukrani na pongezi kwa wote walioshiriki zoezi hili:The Best Newcomer BlogBonyeza hapo chini kuona matokeo yote kwa wale walioshiriki:http://tanzanianblogawards.blogspot.com/ |
PICHA ZINGINE NAMNA DAMU ILIVYOMWAGIKA KENYA,TAHADHARI PICHA ZINGINE NI MBAYA SANA
Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari
Mashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana.Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatiliMfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyoMtoto akikimbia kuokoa maisha yake
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawaZaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa na zaidi ya 162 wakijeruhiwa.Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo haoMwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askariMwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shoppingMwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwaOfisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silahaPolisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mallPolisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine. “Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili.Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-ShababPolisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-ShababPolisi wakipambana na Al-ShababRaia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi haoWanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-ShababWananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa
Subscribe to:
Posts (Atom)