Thursday, 31 July 2014
DUNIANI KUNA MAMBO JAMANI, UNAAMBIWA MISUKULE YA GWAJIMA YATINGA POLIS... NDUGU WATHIBITISHA KUHUSU VIFO VYAO
Baada ya hivi karibuni kutoa waraka mzito unaowalenga watumishi wa mungu kwa kile alichodai kuwa ni ukiukwaji wa sheria za mungu, Nabii Hosea Chamungu ametangaza rasmi kuiwasilisha ripoti ya misukule feki mikononi mwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe…
.
.
Akiongea kwa kujiamini, Nabii Cha Mungu alimuonyesha mwandishi baadhi ya picha za misukule ikiwmo iliyowahi kuonyeshwa ndani ya kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na mchungaji Josephat Gwajima…..
“Unapofanya kazi ya mungu hutakiwi kuwa mwoga kwa lolote kwani yeye ndiye anayetulinda sisi sote, kondoo wa bwana wamekuwa wakipotea siku hadi siku huku wachungaji tukiwaangalia bila kuwaokoa.Mimi sikubaliani na hii miujiza ya kutoa misukule inayotangazwa kila siku wakati hatujui hao misukule walifia wapi….“Baada ya kufunuliwa na mungu juu ya jambo hili, nimeanza kukusanya taarifa kuhusiaa na hili jambo na tayari uelekeo umeshapatikana, watu hawataamini siku nitakapoliweka wazi hili suala kwani nitaliomba jeshi la polisi liwashitaki wote waliorubuniwa na kujifanya misukule pamoja na wale walioinjinia ishu nzima.Kama kuna watu wenye uwezo wa kufufua watu kwa nini vifo vinaendelea kutokea kila siku?”,alisema Cha Mungu
Cha Mungu alidai kuwa zoezi hilo litafikia hitimisho mwishoni mwa mwezi ujao.
Aidha, alitoa wito kwa ndugu, jamaa na wazazi ambao kwa namna moja au nyingine wamehusika na kuficha siri za ndugu, jamaa au watoto wao waliojihusisha na zoezi la kumdhihaki Mungu la kujifanya wao ni misukule wangali wakijua si kweli wajisalimishe kabla hajawaumbua….
“Nitakapokamilisha details nitawataja kwa majina, mahali walipo na jinsi walivyohusika, kwa wale ambao wanaogopa vitisho waje nitawaombea na roho ya woga itaondoka na hakuna atakayewadhuru,” alisema
Jitihada za kumpata mchungaji Gwajima kuongelea suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutopatikana.
AIBU KUBWA HII: MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFUMWA AKILIWA URODA GESTI MCHANA KWEUPE
Askari wa jeshi la polisi na wasamaria wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba moja ya shule ya msingi Manispaa ya Morogoro,
binti huyo anadaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi wakati akipelekwa kituo kidogo cha polisi. Kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na mapenzi na masomo.
binti huyo anadaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi wakati akipelekwa kituo kidogo cha polisi. Kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na mapenzi na masomo.
Wasamalia wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba Manispaa ya Morogoro baada ya kumnusuru na kipigo
Sunday, 27 July 2014
RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali
James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security
and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa
cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai
26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki
tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi
walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe.
Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa
umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali
C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia
katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni
jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa
kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni
zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili
ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es
salaam leo Julai 26, 2014.
zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili
ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es
salaam leo Julai 26, 2014.
NEWS ALERT : BASI LA HOOD LAPATA AJALI MBAYA ASUBUHI HII LIKITOKEA MBEYA
Muda mchache baada ajali kutokea
Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo
Basi la Hood limepata ajali asubuhi hii likitoka Mbeya haijafahamika mara moja lilikuwa linaelekea wapi na haijafahamika kama kuna watu waliojeruhiwa, endelea kufutilia hapa kupata taarifa kamili hii ni taarifa ya awali. Picha na Mbeya yetu Blog
MWIMBAJI BAHATI BUKUKU APATA AJALI MBAYA YA GARI
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendokasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)