Leo Kikao cha Bunge kilikuwa kikiendelea Dodoma, Mbunge Zitto Kabwe alikuwa mmoja ya Wabunge waliochangia katika mjadala uliokuwa unaendelea jioni ya leo kabla ya kupewa nafasi ya kusimama na kutoa maelezo binafsi.
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu alimpa nafasi hiyo Zitto Kabwe ambaye alisimama na kuanza kuongea; “Nashukuru kwa kunipa fursa hii kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wenzangu.. Leo mchana nimemuandikia barua Mheshimiwa Spika ya kung’atuka Ubunge sina sababu ya kwenda kwenye details kuhusiana na jambo hilo kwa sababu taarifa ambayo nilikuwa nimeandaa kuitoa jana imesambaa na ipo na nitaisoma kwenye vyombo mbalimbali vya habari…“
Mnamo tarehe 10 March 2015 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA akiwa makao makuu ya Chama hicho akiambatana na Katibu Mkuu wa CHADEMA alitangaza kuwa Chama hicho kimenifukuza uanachama…Nimeamua kutii uamuzi wa CHADEMA na hivyo kung’atuka rasmi…
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwenu Wabunge wote kwa yale yote ambayo tumeyafanya pamoja kwa ajili ya nchi yetu. Tumefurahi pamoja.. Tumehuzunika.. Tumelia.. Tumeisimamia pamoja Serikali na ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge hili la kumi.. Na Mungu akipenda tutakuwa pamoja mwezi November… Kwaherini.. Asanteni sana”
Sauti yote iko hapa, play umsikilize Zitto Kabwe na Mwenyekiti Mussa Zungu.