YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 29 March 2014

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MAREHEMU TUPPA MKOANI DODOMA



Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu wa Bunge),Mh. William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh. Rehema Nchimbi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara likiwa uwanja wa Nyerere mjini Dodoma wakati wa ibada ya kuuaga.
Viongozi mbali mbali wa Vyama na Serikali wakiwa kwenye Ibada ya Kuaga mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
 
 
 
 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza viongozi mbalimbali na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mara ambaye alifariki dunia ghafla Machi 25, 2014 akiwa ziarani wilayani Tarime. 
Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu John Gabriel Tuppa kwa wakazi wa mji wa Dodoma ilifanyika leo mchana (Ijumaa, Machi 28, 2014) kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere ambako ibada ya kumwombea marehemu ilifanyika. Baadaye mchana, mwili wake ulisafirishwa kwenda wilayani Kilosa, mkoani Morogoro kwa mazishi.
 
Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Padri Chesco Msaga ambaye aliongoza ibada hiyo, alisema Mungu aliwaumba wanadamu ili wampende na wamtumikie na kwamba marehemu Tuppa alilitimiza jambo hilo vilivyo.
 
Alisema wakati wa uhai wake, Bw. Tuppa alipenda haki na popote alipokwenda alitetea haki za wanyonge. “Sote ni mashahidi wa jinsi alivyopenda watu na jinsi alivyowatumikia watu. Alikuwa mnyenyekevu, aliwasikiliza wengine na alithamini michango ya wengine. Na sisi tunapaswa kuiga hilo,” alisema.
 
Naye Dk. Right Mmbaga, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Baraza la Wazee la Dodoma Mjini alisema: “Wale watumishi ambao bado wako kazini na walipata nafasi ya kufanya kazi na Bw. Tuppa, wajifunze kutoka kwake na wafuate nyayo zake kama njia ya kumuenzi.”
 
Naye Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba, akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, alisema Chama cha Mapinduzi kimempoteza kamisaa makini sana aliyekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Bw. William Lukuvi aliwaasa wakazi wa Dodoma kuenzi mambo ambayo Bw. Tuppa aliwafanyia wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma hata kama walikuwa hawayaoni.
 
“Alikuwa na upeo wa kufanya kazi kwa spidi lakini kwa utulivu. Wakati tumeanza naye kazi hapa Dodoma mwaka 2006, kulikuwa na shule sita tu za sekondari lakini katika kipindi cha miaka miwili alifanikisha kusimamia ujenzi wa shule za sekondari 30,” alisema Bw. Lukuvi ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
 
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Makanisa ya mkoa wa Dodoma, Askofu Dk. Yohana Masinga alisema viongozi hawajui kwamba wakishateuliwa, wao ni watumishi wa Mungu kwa sababu wanawaongoza watu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu..
 
Akinukuu neno la Mungu kutoka kitabu cha Waebrania sura ya 13 aya ya 7, linalosema wakumbukeni waliokuwa wakiwaongoza, ichunguzeni miisho ya mwenendo wao na iigeni imani yao, Askofu Masinga aliwataka wote waige mfano wa utendaji kazi wa Bw. Tuppa.
 
“John Tuppa alikuwa ni mtendaji na kanisa limempoteza mtu makini. Ninawaomba viongozi wa nchi hii waige mfano wa John Tuppa. John Tuppa awe ni mfano kwao, na wafanye hivyo kwa ukombozi wa nchi yetu,” alisema.

Bw. Tuppa anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Machi 29, 2014) wilayani Kilosa. Alizaliwa Januari mosi, 1950. Amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara  mwaka 2011. Ameacha mke na watoto watano.

ENEO LA JANGWANI LINAVYOONEKANA SASA KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM


Picha kwa hisani ya mdau Bilal Ahmed

Friday, 28 March 2014

"WABUNGE WANAOTAKA KUTUMIA KURA YA SIRI BADALA YA WAZI NI MASHOGA.."MWIGULU NCHEMBA




Naibu Katibu wa Fedha, Mwigulu Nchemba  jana  katika Bunge Maalum La Katiba alichafua hali ya hewa baada ya kumwambia Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa kwamba wanataka wabunge wa bunge hilo watumie kura ya siri badala ya wazi kwa kuwa ni mashoga.

"Wanaotetea kura ya siri itumike katika kupitisha Katiba ya Watanzania, wanaunga mkono sera za ushoga, ni wale ambao vyama vyao vinazaminiwa na wanaotetea sera za ushioga," alisema Nchemba bungeni.

Kutokana na Kauli ya Nchemba, bunge hilo lilipuka likitaka aombe radhi huku akionyesha kusita kuomba radhi, lakini Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan alimtaka aombe radhi mara kadhaa.
"Mheshimiwa Mwigulu, naomba usimame na kuomba radhi wabunge wenzako, tafadhali simama," alisema Samia
Baada ya kauli ya Makamu Mwenyekiti Samia, Mwigulu alisimama na kusema: "Mheshimwa Makamu Mwenyekiti, Naomba radhi kwa wote wanaodhani wao wako hivyo kama nilivyosema."
Kauli hiyo ilionekana kuendelea kuwachefua wabunge wa bunge hilo huku wakimzomea na kumtaka aombe radhi kwa kuwa bado alikuwa hajaomba radhi moja kwa moja bali kauli yake ilionekana kuwa na utata.

Kwa mara nyingine, Makamu Mwenyekiti, Samia alisimama tena na kumtaka aombe radhi. "Mheshimiwa Mwigulu tafadhali omba radhi bila condition, tafadhali, bila kuomba radhi, Bunge haliwezi kuendela, na ninyi wabunge wengine kaeni kimya bila utulivu hatuwezi kusikilizana, tafadhali," alisema Samia.
Baada ya kauli kauli ya Makamu Mwenyekiti, Samia, Mwigulu alisimama tena na kuomba radhi kwa heshima na bunge kuendelea na utaratibu wake.
"Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti, nakiheshimu hicho kiti hapo mbele, siwezi kudharau, Naomba radhi kwa wote nilowaudhi," alisema Mwigukulu na kukaa chini.
Baada ya kauli ya Mwigulu ya kuomba radhi, shughuli za bunge ziliendelea kama kawaida

TAZAMA PICHA MWALIMU ANASWA AKIJIUZA,ASEMA MSHAHARA MDOGO,



Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
 Wakati Wakristo bado wapo kwenye Kwaresma, mama aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, amenaswa laivu akijiuza maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 24, mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina INAENDELEA HAPA

AACHIWA HURU BAADA YA KUKAA GEREZANI KWA MUDA WAMIAKA 46 JERA.


iwao 3

Mahakama moja nchini Japan imemuachia huru mfungwa aitwae Iwao Hakamada aliekua akitumikia kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1968 ambapo wanaomtetea wanasema ushahidi wa kumfunga ulitengenezwa.Mahakama imeunga mkono kwa kusema ni kweli ushahidi wa uongo ulitengenezwa mwaka 1968 ili kumfunga kwa tuhuma za kumuua boss wake pamoja na kuiteketeza kwa moto nyumba ya boss huyo.Hakamada alizikataa hizi tuhuma mwanzoni lakini baadae alikuja kuzikubali huku akisisitiza kuzikubali huko kutokana na shinikizo ambapo kesi yake ilirudiwa tena na kuanza kupiganiwa mwaka 1980.


Iwao Hakamada

Wanaomuunga mkono pamoja na jamaa na marafiki walikuwa wakiendesha kampeni za muda mrefu kuhusu bondia huyu wa zamani ambae ana umri wa miaka 78 sasa hivi na kusema damu iliyoonekana katika nguo zilizoletwa kwenye ushahidi Mahakamani ilikua ya uongo.Vipimo vya DNA baadae vilionyesha kwamba hakukuwa na uhusiano wowote wa damu hiyo ya nguo na damu ya Hakamada mwenyewe ambapo mwaka 2007 mmoja wa Majaji watatu waliomuhukumu Hakamada kwenda gerezani mwaka 1968 K.Norimichi alisema amejutia uamuzi alioufanya.


iwao 2

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MARCH 28, 2014


.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.