Friday, 21 February 2014
Wednesday, 19 February 2014
MATAJIRI WAKUBWA BONGOZZ NA VYANZO VYAO VYA MAPATO VIKO HAPA LIVEE
R. Mengi |
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).
Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.
Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.
Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.
Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.
Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.
Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.
Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.
Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.
Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.
“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.
Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.
Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.
Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.
Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.
Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”
Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.
Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.
Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.
Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.
Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.
Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.
Ni mmoja wa waanzilishi wa taasisi mbalimbali ikiwemo East Africa Capital Partners, vyombo vya habari, sekta ya mawasiliano ikiwamo Venture Capital Fund Manager na nyingine katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mwananchi Communications Limited, Benki ya Stanbic, Mwenyekiti wa Africa Leadership Initiative East Africa Foundation.
Akizungumzia taarifa hiyo, Mufuruki aliwapongeza waliotajwa kuwa ni matajiri.
“Ningefurahi sana kama ningekuwa na utajiri huo lakini kwa upande wangu naona kwangu kuna tatizo la taarifa kwani walizotoa si sawa,”alisema Mufuruki na kuongeza;
“Sizungumzii watu wote waliotajwa, bali nazungumzia mimi mwenyewe ‘data’ walizotoa si sawa kwa upande wangu.”
Hata hivyo, alisema anafurahi kuona watu wanaanza kuzungumzia utajiri wa watu wengine ‘in a positive way’ (kwa mrengo chanya) na si vinginevyo.
LOWASSA NA WENZAKE WATIWA KITANZINI-WAFUNGIWA KUGOMBEA UONGOZI CCM.
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imetangaza uamuzi mzito dhidi ya wanachama wake sita ambao hivi karibuni waliitwa na Kamati Ndogo ya Maadili na kuwahoji kutokana na tuhuma za kuanza kabla ya wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu wa urais wa mwaka 2015.
CCM imewatia hatiani vigogo wote sita kwa makosa ya kujihusisha na kampeni za uchaguzi kabla ya wakati, hivyo kuwafungia kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho kwa miezi 12, pia wakiwa chini ya uangalizi.
Waliokumbwa na adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jana alisema wanachama hao wote sita walitiwa hatiani kwa makosa ya kuanza kampeni za kuusaka urais wa 2015 kabla ya wakati jambo ambalo ni kinyume na taratibu za chama hicho, hivyo kutoa onyo kali. Adhabu ya onyo kali kwa mujibu wa taratibu za chama hicho inamaanisha kuwaweka chini ya uangalizi kwa miezi 12 ili kuhakikisha hawajihusishi na vitendo vyovyote vinavyokwenda kinyume na misingi ya chama hicho, vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Mwanachama aliyepewa onyo kali atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12 ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha,” alisema Nnauye.
Hatua hiyo ya CCM imezitia doa harakati za vigogo hao, kwani watatumikia adhabu yao hadi Februari 2015 na wakati wote watakuwa wakichunguzwa mienendo yao.
Nnauye alisema makada hao kwa kuanza kwao kampeni za kutafuta kuteuliwa kuwania urais kabla ya wakati ni kinyume na kanuni za uongozi na maadili za CCM, toleo la Februari 2010, Ibara 6 (7)(i).
“Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. “Vitendo vya namna hii ni kosa kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili za CCM toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo,” alisema Nnauye.
Alisema: “Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo, imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya onyo kali na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo chama kitawachukulia hatua kali.”
Alisema Kamati Kuu imeiagiza kamati ya maadili kuwachunguza mawakala na watendaji wa wanachama hao waliokuwa wakiratibu shughuli mbalimbali ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu hatua inayolenga kuhakikisha chama hakigawanyiki.
Nnauye alisema Ibara 6 (2) (1-5) ya maadili ya viongozi wa chama hicho inawazuia kutoa michango, misaada, zawadi za aina yoyote, kukusanya michango na kufanya kampeni bila ya kupata kibali kutoka kamati ya siasa ya halmashauri ya eneo husika.
BREAKING NEWS: MAPIGANO MAKALI YANAENDELEA KATIKA ENEO LA MBEZI JUU JIJINI DAR ES SALAAM.. SOMA ZAIDI HAPA
Hili ni kundi la vijana waendesha bodaboda wakienda mtoni kumwokoa mwenzao ambaye wanadai ametekwa na wahuni wanaojificha mtoni na kukaba watu, mpaka sasa boda boda aliyetekwa yupo mwananyamala hospital na mmoja wa vijana wanaoaaminika kwamba ni vibakaba ameshauawa
Kuna mapigano makali eneo la kwa mzee Juma Kata ya Mbezi juu.
Habari zaidi zionasema kwamba Waendesha Bodaboda hao wanaendelea kupambana kwa kutumia silaha za jadi dhidi ya vijana wanaosemekana aidha ni vibaka au wameiba pikipiki ya mwenzao.
Hali ni mbaya majeruhi ni wengi na inasemekana kuna vifo vimetokea.

Monday, 17 February 2014
MASIKINI MTOTO HUYU:AOKOTWA AMEKATWA MAPANGA NDANI YA MSITU MNENE
Add caption |
MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba.
Alisema aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani haikuwa ya kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
“Wenye ng’ombe walishakimbia, waliniambia ni lazima waniue, niliwaomba wasiniue, lakini hawakunijali, niliishiwa nguvu, damu nyingi ilikuwa imenitoka,waliondoka na kuniacha porini peke yangu.
“Nilipiga kelele ili nipate msaada lakini hakuna aliyejitokeza, nilikata tamaa, baada ya saa kadhaa mtu mmoja alipita na kuniona, akawaita watu akiwemo Mwenyekiti wa kijiji chetu, wakaja kunichukua na kunikimbiza katika zahanati,” alisema mtoto huyo.
Kijana huyo alisema kwamba baada ya huduma ya kwanza katika zahanati hiyo, alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuonekana mbaya zaidi na kwamba ana uhakika wazazi wake hawajui alipo kwani hadi sasa hawajafika kumtembelea.
“Ninamshukuru sana mwenyekiti kwa kunipa msaada mkubwa, sasa hivi amerudi kijijini, najua atawapa taarifa ndugu zangu, ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa kuokoa maisha yangu kwani kwa sasa nina nafuu tofauti na nilivyookotwa katika msitu mnene,” alisema Barihegi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Athumani mtasha alipoulizwa kuhusiana na tukio alisema kuwa amehamishiwa makao makuu.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP Urich matei yupo nje ya mkoa kikazi ila kaahidi kufuatilia sakata hilo kwa undani.
Add caption |
Mtoto Ismail Barihegi.
Barihegi ambaye amelazwa katika Jengo la Mwaisela Wodi na 17, Muhimbili, alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba siku ya tukio (hakumbuki)alikuwa akichunga ng’ombe porini lakini ghafla walitokea watu na kumwuliza kwa nini aliwaachia ng’ombe wake kufika shambani.Alisema aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani haikuwa ya kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
Add caption |
“Nilipiga kelele ili nipate msaada lakini hakuna aliyejitokeza, nilikata tamaa, baada ya saa kadhaa mtu mmoja alipita na kuniona, akawaita watu akiwemo Mwenyekiti wa kijiji chetu, wakaja kunichukua na kunikimbiza katika zahanati,” alisema mtoto huyo.
Kijana huyo alisema kwamba baada ya huduma ya kwanza katika zahanati hiyo, alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuonekana mbaya zaidi na kwamba ana uhakika wazazi wake hawajui alipo kwani hadi sasa hawajafika kumtembelea.
“Ninamshukuru sana mwenyekiti kwa kunipa msaada mkubwa, sasa hivi amerudi kijijini, najua atawapa taarifa ndugu zangu, ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa kuokoa maisha yangu kwani kwa sasa nina nafuu tofauti na nilivyookotwa katika msitu mnene,” alisema Barihegi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Athumani mtasha alipoulizwa kuhusiana na tukio alisema kuwa amehamishiwa makao makuu.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP Urich matei yupo nje ya mkoa kikazi ila kaahidi kufuatilia sakata hilo kwa undani.
MIKOSI YAZIDI KUMUANDAMA SHILOLE YALIYOMKUTA IGUNGA HAYASIMULIKI
Ile Ziara ya wanamuziki Mad, Queen Durleen na Shilole imeingia doa kufuatia wananchi wengi kutokufurahishwa na uvaaji aliokuwa ameuvaa Shilole huku wazee wa Kisukuma na Kinyamwezi kumlani vikali mwanamuziki huyo na kudai siku akirudi tena huko aje amevaa gauni la sivyo atakiona cha moto.
Mtonyaji wetu wa habari hizi ambae alikuwa kwenye msafara wa wasanii hao aliieleza Xdeejayz kuwa Shilole aliwafanya wakazi hao kushindwa kufurahia ujio wa wanamuziki hao kutokana na kingu kifupi alichokuwa amevaa huku sehemu ya mapaja yake ikiwa wazi na watoto kushuhudia nusu mwili wake jambo ambalo hawajawahi kuona.
Hata hivyo Shilole ambae amekuwa na kawaida ya kuvaa nusu uchi akiwa stejini jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakichukizwa nalo na wamekuwa wakimuonya mara kwa mara kuachana na kuvaa nusu uchi kwa vile mashabiki wengi wanahitaji burudani na sio kuona maungo ya miili yake, lakini ameonekan kupuuza.
Xdeejayz ilimtafuta Shilole kupitia simu yake ya kiganjani ili azungumzie balaa hilo lililom kuta lakini kwa bahati mbaya hakuweza hadi habari hii inawafikia wasomaji wetu wenye kiu ya kujua habari na matukio yalijiri wikiend.
VICKY KAMATA KATISHA.... HUU NDIO UTAJIRI WAKE , WABAYA WASEMA NI FREEMASON
Stori: Jelard Lucas
WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa.
UWAZI LINA KILA KITU
Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata. Gazeti hili lilimchimba kwa kina na kupata utajiri wote alionao kwa sasa.
KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA
Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni.
Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii.
“Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro.
“Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).
MAFANIKIO YAANZA
Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano.
Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.
MJENGO WA GHOROFA MBILI
Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne.
Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake.
MAGARI YAKE SASA
Kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261.
Ana Toyota Voxy- Noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16.
Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130.
Mara nyingi anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90.
Pia mwanamama huyo ana gari aina ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25.
ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU
Wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake.
“Vicky amenunua mgodi wa dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
ANA SHAMBA LA EKARI 157
Utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba lenye ekari 150, Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la miti Kibamba, Dar lenye ekari 7.
NI MFUGAJI
Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.
ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA
Katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.
KIPATO CHAKE KIKOJE?
Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.
AMFUNIKA ANNE MAKINDA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake ipo Kijitonyama.
ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME
Uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24.
Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.
WABAYA WAKE WAMUUNDIA ZENGWE LA FREEMASON
Huwezi kupendwa na kila mtu, hii ni baada ya mwandishi wa gazeti hili kuamua kupiga kambi kwa muda wa siku mbili jirani na nyumba ya mheshimiwa huyo ambapo baadhi ya watu waliohojiwa kuhusu ukwasi wa mbunge huyo mwanamke walisema huenda ni memba wa Freemason.
“Mafanikio ya mbunge huyu bwana ni makubwa mno, tunasikia watu wakisema huenda ni Freemason. Lakini ndivyo tulivyo Watanzania, mtu akifanikiwa kidogo wanasema ni Freemason, ninavyomfahamu huyu dada amepiga hatua, sijawahi kumsikia na mambo ya Freemason,” alisema jirani mmoja na kuungwa mkono na wenzake.
MSIKILIZE VICKY
Katika mahojiano maalum na Uwazi kuhusu utajiri wake, Vicky alisema:
“Mafanikio yote yametokana na juhudi zangu za kujituma katika kufanya kazi, namwamini Mungu siku zote. Hakuna dhambi mbaya hapa duniani kama kukata tamaa.
“Tukifanya kazi kwa kujituma na kumwamini Mungu hakuna Mtanzania maskini.
“Kila mtu ana uwezo wa kubadilisha mfumo wa maisha akiamua, umaskini wa watu si chaguo la Mungu, kila jambo litokealo kwa mwanadamu lina maana kubwa kwa Mungu.”
KAULI YA UWAZI
Wanawake nchini waige mfano wa Vicky kwa kukamata fursa mbalimbali na wanapofanikiwa wawasaidie wengine, kama kusomesha yatima na wasiojiweza.

MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 17, 2014
Kila siku hapa millardayo.com huwa naweka magazeti ya siku husika, kuanzia udaku michezo na hardnews nikiamini kwamba wakati mwingine unaweza kuwa mbali na yanakopatikana au yakawa yanachelewa kukufikia asubuhi.
Lengo la millardayo.com ni kuhakikisha kila Mtanzania anaweza kusoma stori kubwa za Magazeti kabla ya saa mbili kamili asubuhi ambapo kwa mwaka 2014 lengo ni kuhakikisha Magazeti yanakuepo hapa millardayo.com hata kabla ya saa moja asubuhi.
Unaweza kujiunga na familia ya Millard Ayo kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili kuwa karibu zaidi ya habari zote zinazowekwa hapa ambazo huwa link zinawekwa kwenye mitandao hii ya kijamii muda mfupi tu baada ya habari kupandishwa hapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)