YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 4 September 2014

DIAMOND AKIONGEA LIVE KWA YALIYOTOKEA SHOW YAKE YA GERMANY.


Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.12 AMKuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na millardayo.com
1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.38 AM3. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.59 AM6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’
Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

MSKILIZE WEMA AKIONGELEA YOTE YANAYOSEMWA IKIWEMO ISSUE YA KUAJIRIWA NA KAJALA

wemaaKupitia mitandao na magazeti siku chache zilizopita ilitoka stori ambayo ilidai Kajala anaelekea kumuajiri Wema Sepetu,leo Wema kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala.
Kupitia You heard ya  XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye[Wema],Wema Sepetu akamjibu>>’Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy’
Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu>>’Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy’
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu>>’Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali’.
98.6 Clouds Fm inasikika ukiwa Musoma.
Bonyeza play kusikiliza.

MAGAZETI YA LEO SEPT. 4/2014


DSC_0138
.


DSC_0139

DSC_0141
DSC_0142
DSC_0143
DSC_0144
DSC_0146
DSC_0147
DSC_0148
DSC_0149
DSC_0150
DSC_0151
DSC_0152
DSC_0153
DSC_0154
DSC_0155
DSC_0156
DSC_0158
DSC_0159
DSC_0160
DSC_0161
DSC_0162
DSC_0163
DSC_0164
DSC_0165
DSC_0166
DSC_0167
DSC_0170
DSC_0171
DSC_0172
DSC_0173
DSC_0174
DSC_0175
DSC_0176
DSC_0177
DSC_0178
DSC_0179
DSC_0180
DSC_0181
DSC_0182
DSC_0183
DSC_0184
DSC_0185

SIKILIZA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA CLOUDS FM

12345Mara baada ya kuwa umepitia kurasa mbalimbali za Magazeti naomba utumie nafasi hii pia kusikiliza yakichambuliwa na kusomwa kupitia kipindi cha Power Breakfast,hapa yanachambuliwa na kusomwa na PJ.
87.8 Clouds Fm inasikika ukiwa Mbeya.
Bonyeza play kusikiliza.
Tags :

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA UTAKAZOZIONA:-Majambazi Watano wauawa katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma




Majambazi watano waliokipata cha moto katika Majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakiwa na siraha za kivita wakisubiri kuteka magari Alfajiri ya Septemba 03,2014 wakiwa chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Kasulu.

 



JESHI la polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45 alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.





Kwa mujibu wa kamanda Ibrahim alisema askari polisi wakiwa katika doria walipata taarifa za majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakitaka kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kuteka magari ya wasafiri yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo. 

Alisema kufuatia taarifa hiyo askari polisi walijipanga na kuweka mtego katika eneo lililokusudiwa kufanyika uhalifu huo ambapo baada ya muda watu hao walifika eneo la tukio ili kukamilisha azma yao ambapo askari waliwafuata ndipo walipoanza majibizano ya risasi na askari polisi.



Katika tukio hilo askari walifanikiwa kuwauwa majambazi wote watano ambapo katika eneo la  tukio hilo walikuta mabomu matatu, silaha mbili za kivita aina ya SMG  No. 691220  pamoja na AK 47 no. UA40501997 magazini tatu zenye risasi 64 sambamba na mikate na juice aina ya Zaam Zam orange kutoka katika kampuni ya Monas Beverages.  

Kamanda alisema miili ya majambazi hao ipo katika hospitali ya wilaya ya Kasulu ambapo majina yao hayajatambulika huku askari polisi waliokuwa katika tukio hilo wakiwa wamesalimika na hakuna aliyejeruhiwa ambapo msako unaendelea katika maeneo yote ili kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani Kigoma.


Chanzo mwanawamakonda blog