Leo February 23, 2018 Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako ameahidi kumsomesha mdogo wake Akwilina Akwilini, Angela Akwilini hadi chuo kikuu ambapo kwa sasa anasoma kidato cha tatu.
Prof. Ndalichakoamezungumza hayo katika mazishi ya Akwilinaaliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika daladala wakati Polisi wakitawanya maandamano ya Wafuasi wa CHADEMA.
Nae Mbunge wa Rombo, Selasini amewasilisha rambirambi ya Shilingi Milioni 1 na laki tano kwa niaba ya Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA.
Walichozungumza Rais Magufuli na Kenyatta nchini Uganda
Leo February 23, 2018 Wakazi wa Kijiji cha Mtegu kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara wamelalamikia kuwepo kwa sintofahamu ya kufunguliwa kwa kituo cha Afya kijijini hapo ambacho kimejengwa kwa nguvu zao tokea mwaka 2006 kupitia makato ya Shilingi 50 kwa kila kilo ya zao la korosho kwa ahadi ya kufunguliwa mwezi September, 2018 ahadi ambayo haijatekelezeka.
Wakazi hao wamesema kuwa ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu mwaka 2006 na kukamilika May 17, 2108 lakini hadi sasa hakuna huduma yeyote ya afya ilioanza kutolewa licha ya wakazi hao kutembea umbali Kilometa 35 kufuata huduma katika kijiji cha luagala.
KILICHOAMULIWA KUHUSU KUAHIRISHWA KESI YA DR. TENGA LEO
Leo February 23, 2018 Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa Madini yote nchini ni Mali ya Watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.
“Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya” -Biteko
Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.
“Nataka niwajulishe tu Watanzania wenzangu Rais Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine” -Biteko
Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.
Leo Jumamosi February 24, 2018 kumekuwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha polisiOysterbay, ambapo inasemekana wana majeraha ya risasi na mpaka sasa hawajapelekwa hospitali.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa watu hao wote watatu walijeruhiwa siku ya Ijumaa ya February 16, 2018 katika maandamano ya wafuasi wa CHADEMA kwenye kipindi cha uchaguzi mdogo, katika eneo la Kinondoni walipokuwa wakidhibitiwa na jeshi la polisi.
Hatahivyo Ayo TV na millardayo.com imefanya mawasiliano na Kamanda wa Polisi Kinondoni RPC Murilo Jumanne Muliro kuthibitisha suala hilo ambapo amesema ni kweli wanawashikilia watu hao lakini mtu yeyote akiwa mahabusu na kuhitaji matibabu, hupatiwa matibabu hayo kwa wakati.
Kamanda Murilo ameeleza kuwa mtuhumiwa yeyote akiwa mahabusu na akahitaji matibabu yoyote hata kama anaumwa malaria hupelekwa hospitali kutibiwa tena bila gharama yoyote hivyo hizo ni propaganda.
“Kuna Charge Room Officer ambaye moja kati ya kazi yake ni kuhakikisha kila baada ya masaa manne anakagua mahabusu kuangalia hali za watuhumiwa, kama kuna anayehitaji matibabu anapelekwa hospitali na hii haihitaji shinikizo ni haki yao kisheria na tumeshaifanya kabla wao hawajaongea.” – Kamanda Muliro
Wananchi waomba Jengo la Zahanati walilojenga kwa Fedha zao Wafugie Mifugo
Maamuzi ameyafanya Prof: Ndalichako kwa mtoto aliyekuwa analia kwenye msiba wa Akwilina