YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 15 June 2013

BREAKING NEWS......! WATU SABA WAMEJERUHIWA VIBAYA BAADA YA BOMU KULIPUKA HUKO ARUSHA

6510_197909020362132_1935330081_n
Takriban watu saba wamejeruhiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu, kilicholipuka eneo la Soweto, jijini Arusha, ambako mkutano wa CHADEMA ulikuwa ukifanyika. Tukio hili limetokea muda mfupi tu baada ya mwenyekiti wa CHADEMA, kumaliza kuhutubia wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo na inasemekana Watu 6 Wamepoteza Maisha Na Wengine Kujeruhiwa,,

Wananchi Arumeru wateketeza shamba la mwekezaji

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku nyumbani kwa mwekezaji huyo, Ikbar Abdalah (53)ambaye ni mkulima mwenye asili ya Kiasia na mkazi wa kijiji hicho.

Arusha. Wananchi zaidi ya 1000 wa kijiji cha kwa Ugoro wilayani Arumeru, wamevamia shamba la mwekezaji na kuliteketeza kwa moto na kupora bidhaa mbalimbali mali za mwekezaji huyo zenye thamani ya mamilioni ya fedha.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku nyumbani kwa mwekezaji huyo, Ikbar Abdalah (53)ambaye ni mkulima mwenye asili ya Kiasia na mkazi wa kijiji hicho.
Katika tukio hilo wanakijiji hao walichoma nyumba yake,mabanda mawili, trekta moja chakavu,mashine ya kusaga nafaka,spea za magari na kupora vitu mbalimbali ikiwamo pikipiki moja aina ya Honda.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas ,chanzo cha uharibifu huo ni mgogoro wa muda mrefu kati ya wanakijiji hao na mwekezaji wa kugombea eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 100 linalomilikiwa na mwekezaji huyo.
Alifafanua kuwa viongozi wa eneo hilo walidai kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu, kiasi cha kufikisha suala hilo ngazi ya mahakama na kwamba kesi hiyo ilishawahi kutolewa uamuzi mara mbili na sasa iko ngazi ya rufaa.
Hata hivyo, polisi ilifanikiwa kumnasa mwanakijiji mmoja (jina linahifadhiwa na polisi) anayeshikiliwa katika kituo cha polisi jijini hapa huku wengine wakiendelea kusakwa kutokana na kutenda kosa la kujichukulia sheria mkononi.
Wakati huo huo, Kamanda Sabasi ametoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote cha watu watakaojihusisha na matukio ya kuvuruga uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Juni 16 mwaka huu
.

Video: mwanamke anaswa akivunja amri ya sita vichakani huku akiwa na mtoto mchanga mgongoni

Mwanamke mmoja amenaswa akifanya uchafu porini huku akiwa na mtoto mchanga mgononi...

Tukio hilo la kusikitisha liliwanasa wawili hao wakiridhishana chini ya kichaka huku mtoto mchanga akionekana kulia kwa huzuni.....

Haijafahamika mara moja kama watu hao ni mtu na mume au ni wazinzi tu...!!!

VIDEO HAPO CHINI

MAMA WEMA SEPETU ATISHIA KUMCHOMA MTU KISU KISA MWANAE...

VIDEO inayomuonesha mama wa Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu akizua timbwili ‘hevi’ nyumbani kwa mwanaye huyo huku akitishia kumchoma mtu kisu imevuja, Ijumaa limeinasa.

Kwa mujibu wa video hiyo, mama Wema alitimba nyumbani kwa mwanaye huyo Kijitonyama, Dar kwa lengo la kuwasambaratisha marafiki wanafiki wa Wema ambao alidai wanamharibu mwanaye.
Pamoja na matusi yanayosikika kwenye video hiyo, mzazi huyo alikuwa akitoa vitisho kwa Maila ambaye ni mmoja wa mashosti wa karibu wa Wema.

“Nitammaliza huyu…(tusi), hana kwao, hana chochote,” sauti ya mama Wema inasikika na kuongeza:
“Nina data, mimi nilipigiwa simu, huyu sijui Maila, sijui nani kuwa alishikwa na begi lenye vipisi vya bangi Airport (uwanja wa ndege).
“Hawamshauri Wema chochote, wanamharibu ili maisha yake achanganyikiwe. Ningekuwa na kisu ningemchoma…ningekuwa na kisu leo ningemchoma visu…potelea mbali.”

Mbali na vitisho hivyo, mama Wema anaonekana akibinua vitu vya ndani kama makabati na makochi ikidaiwa kuwa alikuwa akisaka bangi aliyoletewa mwanaye na rafiki zake.

Kwa mujibu wa watu walioiona video hiyo walisema marafiki wa Wema kama Kajala Masanja, Snura Mushi, Martin Kadinda, Jamila na wengine kibao wanapaswa kuwa makini na mama huyo kwani anaonekana kuwa na hasira nao.

Baada ya kuinasa video hiyo, Ijumaa lilimsaka mama Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Mwandishi Wetu alikwenda nyumbani kwa mama huyo Sinza-Mori, Dar ili kuzungumza naye ‘laivu’ lakini alipogonga tu getini alitokea binti aliyedai mama Wema hakuwepo.

PICHA ZAIDI MIAKA 13 YA LADY JAYDEE

Umati wa watu unaoshuhudia show ya Lady J Dee sasa hivi hapa Nyumbani Longe.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Professa Jay akiwa back stage anajiandaa kupanda jukwaani kutoa burudani nzuri kwa mashabiki

Miaka 13 ya Lady j Dee#sasa hivi ndiyo Mh.Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ameingia

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Team Times Fm 100.5 (Dj Jors Bless,Ndimbo na Mariam)

Sugu na Mkoloni wanatoa burudani kali kwa mashabiki.

Mama mzazi wa Lady J Dee naye amekuja kushuhudia show ya mwanae.

Juma Nature anatoa burudani kwa mashabiki

Sugu akitoa burudani kali kwa mashabiki

M 2 The P akiongea machache baada ya kukaribishwa kwenye jukwaa na Juma Nature.