YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 1 February 2013

AJALI MBAYA YATOKEA WATU 5 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 20 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI LA SCANIA, HUKO MBALALI MAPEMA LEO



WATU 5 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 20 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI LA SCANIA LILILOKUWA NA LIMEBEBA WATU ZAIDI YA 200, HUKO MBALALI MAPEMA LEO

ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKISHA MAJERUHI PAMOJA NA WATU WALIO FARIKI HOSPITALINI HAPO

RIPOTI IKIWA INATOLEWA JUU YA AJALI HIYO HUSSEIN
  
MMOJA YA ABIRIA WALIOKUWEMO KATIKA AJALI HIYO

AJALI MBAYA IMETOKEA MAPEMA LEO MBALALI AMBAPO LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA ILIKUWA IMEBEBA WATU ZAIDI YA MIAMBILI (200) AMBAO WALIKUWA WANAELEKEA KATIKA KITONGOJI KIMOJA CHA MWEKEZAJI .

AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T 398 BSE KUANGUKA NA KUSABABISHA WATU 5 KUFARIKI DUNIA NA WENGINE 20 KUJERUHIWA VIBAYA.

HATA HIVYO MAJERUHI WOTE WANAKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA ILIYOPO MBEYA MJINI MUDA HUU.

HIZI NI TAARIFA ZA AWALI TUU, HABARI NA PICHA ZOTE ZINAKUJA HAPA HAPA.PICHA NA MBEYA YETU BLOG

SAHINI SPORTS: HABARI MPYA KUTOKA ARSENAL

SAHINI SPORTS: HABARI MPYA KUTOKA ARSENAL: 0 .

Hallow people...

CALVIN-OBELD-blog..: SENTENSI 4 ZA MBUNGE ZITTO KABWE KUHUSU WANAOSEMA ...

CALVIN-OBELD-blog..: SENTENSI 4 ZA MBUNGE ZITTO KABWE KUHUSU WANAOSEMA ...: 2 . Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amesema hakuna mgogoro kwenye chama chake kama inavyoelezwa isipokua kuna watu wachache...

Hallow people...

CALVIN-OBELD-blog..: HAYA NI MANENO YOTE ALIYOSEMA DIAMOND KUHUSU WANAO...

CALVIN-OBELD-blog..: HAYA NI MANENO YOTE ALIYOSEMA DIAMOND KUHUSU WANAO...: 11 Diamond Platnums. Kwa kipindi kirefu kidogo toka mwaka 2012 kumekua na taarifa mbalimbali zinazopita kwenye magazeti, blogs na m...

Hallow people...

HUYU NDIO MWIMBAJI MKENYA AMBAE MAMA YAKE NI MTANZANIA, KAVUNJA REKODI KUSHIRIKI AMERICAN IDOL, TAZAMA NICKI MINAJ NA MARIA CAREY WAKIMUONGELEA

Anaitwa Sanni M’mairura.
Sio kazi rahisi kuingia kwenye moja ya mashindano MAKUBWA DUNIANI ya AMERICAN IDOL, sio kazi ndogo hata kidogo, SANNI M’MAIRURA ndio Mtanzania wa kwanza mimi kusikia kaingia kwenye haya mashindano ambayo majaji wake wa sasa hivi ni pamoja na mastaa wa muziki duniani Maria Carey na rapper Nicki Minaj, tazama hiyo video hapo chini
hii stori naitabiria kushika namba kubwa kwenye AMPLIFAYA leo,endelea kuwa karibu na Millard Ayo kwa kujiunga kwenye facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo

HAYA NI MANENO YOTE ALIYOSEMA DIAMOND KUHUSU WANAOSEMA KASHUKA KISANII, HUU NDIO MWISHO WAKE


Diamond Platnums.
Kwa kipindi kirefu kidogo toka mwaka 2012 kumekua na taarifa mbalimbali zinazopita kwenye magazeti, blogs na midomoni mwa watu kadhaa kwamba staa wa muziki wa bongofleva anaetajwa kulipwa pesa kubwa kwenye kufanya show Tanzania Diamond Platnums ameshuka kiwango, yani mwisho wake kwenye muziki umefika.
Baada ya hizo taarifa nimekua nikijaribu kufanya interview na Diamond lakini hakupenda kuliongelea hilo kwa wakati huo.
Diamond amebadili huo msimamo na kuamua kufunguka rasmi kwenye Exclusive interview na millardayo.com kuhusu yote yanayosemwa kwamba kashuka kiwango.
Namkariri akisema “unapofanya vizuri hakuna anaependa, kama Maisha Club wasanii wengi huwa wanafanya show lakini nikifanya mimi ndio panatapika hata club nyingi hata nilivyofanya show Dar Live uliona watu kutaka kutia virusi, kutaka kutengenezea mazingira”
“Mashabiki ndio wanatakiwa kusema flani labda sasa hivi ameshuka lakini mashabiki hao ndio hao kila siku wanazidi kununua kazi zangu, wanazidi kuomba nyimbo zangu kwenye redio.. kiukweli nyimbo zangu ndio zinaombwa sana kwenye radio, katika show zangu wanajaa sana” – Diamond
Kwenye sentensi nyingine Diamond amesema “kuna gazeti likaandika Diamond sijui ndio mwaka wake wa mwisho, Diamond sijui ameshuka kiwango… utaweza vipi kuandika vitu kama hivyo? mi ndio msanii ambae nalipwa pesa nyingi kuliko msanii mwingine yoyote Tanzania, vita za kibiashara kokote zipo mimi ndio maana hazinishtui kila siku ndio maana nazidi kuachia ngoma tu kuwakata vilimi vilimi, wanatakiwa wajue kabisa kwamba mimi nimeaga nyumbani… licha ya kuaga mi nafanya muziki kama kazi kwa njaa kabisa, kwa hiyo mwenyezi Mungu alienipandisha na mashabiki zangu ndio wanaweza wakataka kunishusha”

SENTENSI 4 ZA MBUNGE ZITTO KABWE KUHUSU WANAOSEMA MBOWE ANAMCHUKIA, PIA CHADEMA

2
.
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amesema hakuna mgogoro kwenye chama chake kama inavyoelezwa isipokua kuna watu wachache ambao wanataka kugombanisha viongozi wa CHADEMA.
Hii ni kauli ambayo Zitto aliitoa kwenye mkutano na wananchi Kigoma ambapo aliamplfy kwamba CHADEMA ni wamoja isipokua ni watu wachache ndio wamekua wakieneza chokochoko.
Namkariri akisema “nataka mkae mnajua hakuna mgogoro wala tofauti ya mawazo, yani hakuna kitu ambacho mimi nasema twende hivi Mbowe anasema twende hivi isipokua kuna watu wanasema kwamba Zitto Mbowe anakuchukia au Mbowe Zitto anataka kukupindua, wanasema hivyo lakini mimi nataka kuwaambia watu wa Kigoma kwamba hakuna tatizo na pangekua na tatizo lolote ningeshawaambia, kuna watu wanapandikiza mbegu za chuki, kuna watu wanajaribu kufarakanisha viongozi na kujaribu kuonyesha kwamba kuna tofauti”
Kwenye sentensi nyingine Zitto ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini amesema “sisi tutakua ni wajinga sana kukubali kugombanishwa, hatuwezi kukubali kuingia kwenye mgogoro kama ambao NCCR MAGEUZI waliingia kwa sababu leo CHADEMA ikianguka, ikapasuka hapatatokea chama chochote kingine cha upinzani chenye nguvu kwa miaka mingine 20 na watakaoumia ni nyie wananchi, sababu panapokua na upinzani imara wanaofaidika ni nyie, mawazo tofauti ndani ya bunge yanasikika kupitia vyama vya upinzani, mpinzani wako ni lazima atengeneze mbegu za chuki ili mgombane mfarakane”

SUMA LEE ASHINDWA KUFIKA KWENYE MSIBA WA BABA YAKE


Sumalee akiwa Uingereza ambako alikwenda toka december 2012 akiwa na Barnaba.
 
Miezi 8 toka mama yake mzazi afariki dunia, msanii wa bongofleva Sumalee amepata pigo jingine baada ya baba yake mzazi kufariki january 31 2013.
Taarifa zilizoifikia blog yetu ni kwamba baba yake alifariki jana jioni wakati bado Sumalee yuko Uingereza kwa shughuli za kimuziki. 

Namkariri akisema “mama yangu amekufa kwenye mikono yangu, yuko kwenye mapaja yangu na mikononi nilikua namsomea dua tu” 
Kulikua kuna taarifa kwamba Sumalee kapata matatizo ya hati yake ya kusafiria huko Uingereza hivyo itakua ngumu kuja Tanzania msibani lakini taarifa nilizonazo kutoka kwa mtu wa karibu ni kwamba hajapata tatizo lolote kama wengi wanavyodhani, kilichotokea ni kwamba alitaka kuongeza miezi sita ya kuendelea kukaa Uingereza hivyo ikabidi Passport aiache ubalozini ambapo ghafla ndio akapata msiba hivyo itabidi asafiri kwa kutumia documents. 
Mtu huyu wa karibu wa Sumalee ameiambia blog yetu kwamba baba mzazi wa Sumalee anazikwa leo February 01, 2013 na Sumalee wamejaribu kuwasiliana nae hapatikani kwenye simu hivyo hakuna uhakika kama yuko kwenye ndege kuja Tanzania ama la.
pamojapure.blogspot.com inatoa pole kwa Sumalee, familia na ndugu kwa msiba huu