YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 4 August 2018

UPDATES!! WAZIRI KIGWANGALA AAMISHIWA SELIAN HOSPITAL ARUSHA

UPDATES:Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangalla amehamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Selian ,Arusha kwa helkopta kutoka katika kituo cha afya cha Magugu,Manyara alipopelekwa baada ya kupata ajali

MANENO YA MUHIMU NA KUZINGATIA KUTOKA KWA MH. RAISI J. P. MAGUFULI


Mh. Rais John Pombe Magufuli
Alipokua akizungumza wakati wa kukabidhi hati hizo Rais Magufuli alisema serikali ya awamu ya tano imeamua kutekeleza kwa vitendo maneno mazuri ya hayari Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuhamia Dodoma, hivyo ameona sio vema yeye kuhamia Dodoma na kuwaacha mabalozi na wawakilisha wa marais wa  mataifa mbalimbali jijini Dar- esa Salaam na ndio maana ameamua kutoa hati hizo mapema.
Rais Magufuli alisema serikali imeamua kutoa bure maeneo yenye ukubwa wa zaidi hekari tano kwa ajili ya Mabalozi na taasisi mbalimbali lengo likiwa ni kuonesha urafiki uliopo wa mataifa na nchi zinazowakilishwa na viongozi hao, na kwamba viongozi mbalimbali wa serikali yake tayari wamekwisha hamia Dodoma ikiwa ni pamoja na watumishi karibu 60,000.
Alisema serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya umeme, huduma za jamii hasa afya, elimu, maji na usafiri ambapo mkoa wa Dodoma umeunganishwa na barabara za lami na mikoa yote inayozunguka yani Morogoro, Singida, Manyara na Iringa.
Aliongeza “Leo nimetoa maagizo kwa Viongozi wa TANROADS watangaze tenda kwa ajili ya kuanza ujenzi mkubwa wa uwanja wa Msalato ili ndege kubwa zinazotua Dar- esa Salaam zitue Dodoma nimefurahi kumuona mwakilishi wa African Development Bank ( Banki ya Maendeleo ya Afrika) tulizungumza na rais wa benki hiyo kwamba watatoa dola milioni 200 tumeshawaandikia barua ninauhakika watazitoa mapema kwa sababu tumewapa hati ya bure ya kukaa Dodoma”.
Rais Magufuli alieleza  kuwa wakati serikali ikisubiri fedha hizo kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika ametoa maagizo ya tenda kutangazwa ili kazi ya ujenzi wa uwanja huo mkubwa wenye urefu wa zaidi ya kilimeta 3 ianze mara moja ambapo ndege ya aina yoyote inaweza kutua ikiwamo ndege mpya ya serikali Boeing Dreamliner 787-8 pamoja na ndege nyingine kubwa kutoka mataifa mbalimbali.
Aidha Rais Magufuli alitoa wito kwa Mabalozi, Mashirika na Wawakilishi hao wa Mataifa mbalimbali waliopokea hati hizo kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri fursa ya ukubwa wa viwanja walivyopewa kwa kuwekeza ipasavyo hasa kwa kujenga majengo ya ubalozi, sehemu za biashara na makazi kuliko kuendelea kubanana jijini Dar- es Salaam.
 

NUKUU MADHUBUTI ZA MH. RAISI JOHN POMBE MAGUFULI ZIPATE HAPA

Katika dunia ya sasa hakuna kitu kinaweza kupotea ili mradi kimewahi kutamkwa mbele ya jamii. Lakn pia tunaweza kupoteza vitu admu pale tu tutakaposhindwa kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na vya sasa. Kwa kipindi kirefu tumekua na nukuu za Baba wa Taifa mwalimu nyerere. Ni wakati mwafaka kuweka kumbumbuku ya maneno mazuri ya mheshimiwa Rais Magufuli.

Duniani tuna nukuu (quotes) zawa watu maarufu kama Martn Luther king, Jr. Abraham lincoln na wengine wengi. Kwa hapa kwetu tuna nukuu za baba wa taifa mwalim Nyerere.

Sasa ni wakati mwafaka kuweka nukuu zake kwenye uzi huu. Usihofu iwe mbaya masikio mwako au iwe nzuri wewe weka tu maana lolote analo litamka mkuu wa nchi linapaswa kutunzwa.

Naweka maneno mawili matatu kuanzisha ukurasa wa maneno ya mkuu wetu.

''Mimi ni Rais wa maskini. Waliozoea kuishi kama malaika wataishi kama mashetani''.

''Serikali yangu haitawapa chakula. Kila mtu atabeba msalaba wake. 
Njaa haijaletwa na serikali''.



Hakuna serikali iliyowahi kujenga nyumba za wahanga duniani pote. 
Na sisi hatujengi.


''Hakuna kufanya za siasa mpaka 2020''.

''Siwezi kuwashirikisha wapinzani kwenye serikali yangu. 
Nakushangaa Shein kuwaingiza wapinzani''. 


''Sijawahi kutamka katiba kwenye kampeni zangu za kuomba urais. 
Katiba sio kipaumbele changu. Kwa sasa nainyoosha nchi kwanza''.


''Police mkukita mtu anaendesha gari kwenye njia ya mwendo kasi, 
ng'oa tairi uzeni''.


''Watoto watasomeshwa bure kwenye utawala wangu 
hivyo fyatueni watoto wengi maana watasoma bure''.


Haya ni machache kati ya mengi aliyowahi kuyaongea. Ni wakati mwafaka kuweka maneno yake hapa.
=========

TAZAMA VIDEOS ZA SPEECHES MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI 

ALICHOKISEMA MKUU WA WILAYA YA DODOMA - PATROBAS KATAMBI MARA BAADA YA KUAPISHWA


Leo August 3, 2018 Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi baada kuapishwa alipata nafasi ya kuzungumza na Waandishi wa habari ambapo amezungumzia namna alivyopokea taarifa za uteuzi uliofanywa naRais Magufuli na sababu zilizomfanya aondoke kwenye upinzani na kuhamia CCM.
Maagizo makubwa matatu ya RC Dodoma kwa wakuu wapya wa Wilaya

RC MAKONDA AMUAGIZA RAS MPYA KUTEKELEZA YAFUATAYO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda timu ya kufanya ukaguzi wa Mali zote za serikali zilizotaifishwa na wajanja ikiwemo maeneo ya wazi na Nyumba za umma.
RC Makonda ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wapya wa wilaya za Kinondoni na Kigamboni, Katibu Tawala Mkoa na kuwaaga wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ambapo amemuagiza katibu tawala kuhakikisha anakamilisha ripoti kabla ya September 3,2018.
“Nataka uunde timu yako ndani ya mwezi ya mmoja muanze kukagua mali za serikali ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, Ninazo taarifa kuna viwanja vya Manispaa na nyumba za serikali lakini kuna watu binafsi wamevichukua,”

ALICHOKISEMA AIDANI EYAKUZE KWA IDARA YA UHAMIAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TWAWEZA, Aidan Eyakuze amedai kuwa Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria ambapo amezuiwa kusafiri kwa kutumia Shahada ya Dharura iliyotolewa kwa utaratibu uliopo ili aweze kushiriki mikutano ya kikazi kwenye Ofisi za TWAWEZA jijini Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Twaweza, Eyakuze, amesema hadi sasa bado hajajua sababu ya msingi juu ya Idara ya Uhamiaji kuishikilia hati yake ya Kusafiria(Passport), na hakuna taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.
“Kwa wiki kadhaa sasa TWAWEZA, imekua katika changamoto kubwa ya mashirikiano baina yake na baadhi ya Taasisi za Serikali kufuatia uzinduzi wa taarifa za ripoti mbili za Sauti za Wananchi mnamo July 5, 2018 zenye vichwa vya habari visemavyo “Kuwapasha viongozi” na “Nahodha wa Meli yetu wenyewe” -Aidan Eyakuze
“Ni zaidi ya miaka 8 sasa tangu Shirika hilo lianzishwe mnamo mwaka 2009, ambapo limefanya kazi za tafiti mbalimbali na miongoni mwa tafiti zao zimeweza kuishtua serikali katika ufatiliaji wa masuala muhimu hususani katika sekta ya elimu,” amesema Eyakuze

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII Mh. KIGWANGALA APATA AJALI ASUBUHI YA LEO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Hamis Kigwangala amepata ajali asubuhi ya leo eneo la Magugu alipokuwa akitokea Arusha kwenda Manyara. Taarifa iliyothibititshwa na RPC mkoa wa Arusha inasema Afisa habari wa Wizara Ndugu @Hamza Temba amaefariki dunia katika ajali hio huku Mh waziri akiwa na majeraha lakini hali yake sio nzuri.
Tunakuombea Mungu akuponye na Kuipa Faraja familia ya Ndugu yetu mwanahabari mwenzetu Hamza Temba kwa kuondokewa na Kijana wao.
R.I.P Hamza Temba

Friday, 3 August 2018

ZIJUE FAIDA ZA KUMNYONYESHA MTOTO.

Mwanamke akimnyonyesha mtoto wake

Image captio
Wakati ulimwengu ukiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto na kuelezea faida zake kwa wazazi na taifa, wakazi wa dunia wanahamashishwa kufahamu umuhimu wa maziwa ya mwanzo kabisa ya mama kwa mtoto .
Takriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na shirika la Shirika la Afya duniani.
Kadhalika shirika hilo linasema kuwa zaidi ya maisha ya watoto 820 000 walio na umri wa chini ya miaka 5 yanaweza kunusurika kila mwaka, ikiwa watoto wenye umri kati ya if all miezi 0 hadi 23 wangenyonyeshwa kikamilifu.

Ukweli kuhusu umuhimu wa kunyonyesha:

  • Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa mwenye afya na kuendelea kuishi.
  • Kama viwango vya kunyonyesha vingekuwa vya hali ya juuduniani , takriban maisha 820 000 ya watoto yangenusurika kila mwaka, linasema shirika la afya duniani (WHO).
  • Unyonyeshaji wa mtoto kwa miezi 6 kuna faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto.
  • Kumnyonyesha mtoto mara anapozaliwa kwa kipindi cha saa moja, humkinga kwa maambukizi yanayowapata watoto wachanga na kupunguza vifo vya watoto wachanga.
  • Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto wa kati ya miezi 6 hadi 23.
  • Maziwa ya mama yanaweza kuchangia nusu au zaidi ya nguvu za mtoto katika umri wa miaka 6 hadi 12
  • Watoto na vijana wadogo walionyonyeshwa wakiwa wachanga wana uwezekano mdogo wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia .
  • Unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya utu uzima.
  • Kunyonyeshwa kwa muda mrefu pia huchangia afya na maisha bora ya mama kwani humpunguzia hatari ya kupata saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi na matiti.
  • Kunyonyesha hutengeneza vichocheo vyamwili( hormone) ambazo humtuliza mama na mtoto
Juma hili linaadhimishwa huku baadhi ya wanawake duniani wakishindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali. .
Mwanamke akimnyonyesha mwanaeHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGE
Image captionTakriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na shirika la Shirika la Afya duniani
Licha ya juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuelemisha wakina mama na jamii nzima juu ya umuhimu wa kunyonyesha na maziwa ya mama kwa mtoto, baadhi ya mila na tamaduni hususan za Kiafrika zimekuwa na changangoto kubwa ya kuelewa na kukubali umuhimu wa kunyonyesha kutokana na kukosa elimu ya kunyonyesha.
Miongoni mwa changamoto zinachangia wanawake kushindwa kuwanyonyesha watoto wao ni pamoja na kazi, magonjwa pamoja na tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma.
Hivi karibuni mwanamke mmoja nchini Kenya alifukuzwa kwenye mgahawa jijini Nairobi alipokuwa akimnyonyesha mwanae ndani ya mgahawa huo.
Aidha baadhi yao wamekuwa na imani potofu kuhusu suala zima la kunyonyesha na faida zake. Hili limechangia pakubwa katika kudhoofisha jitihada za kuhakikisha kila mama mwenye mtoto mchanga anamyonyesha ipasavyo.
Baadhi ya imani potofu kuhusu kunyonyesha:
  • Maziwa ya kwanza ya mama si mazuri kwa mtoto yanapaswa kumwagwa
  • Kunyonyesha humfanya mama anenepe kupindukia
  • maziwa ya mama pekee hayawezi kumridhisha mtoto wa umri wa miezi 0 hadi sita.
  • Baadhi ya vyakula si vizuri kwa wanawake wanaonyonyesha
  • Ni lazima mtoto mchanga anywe maji mara baada ya kuzaliwa
  • Maziwa ya mama humfanya mtoto ajihisi mwenye kiu
  • Baadhi ya wanawake hudai wanaponyonyesha matiti yao husinyaa na kuanguka.
Shirika la watoto la Save the Children linasema kuwa watoto wenye utapiamlo unaochangiwa na kutonyonyeshwa ipasavyo unakadiriwa kusabisha vifo vya watoto 2.7 kila mwaka.
Aliya Shagieva akimnyonyesha mwanaeHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionAliya Shagieva akimnyonyesha mwanae, Wataalam wanasema mguso wa mwili baina ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama
Wiki ya kimataifa ya kunyonyesha inaadhimishwa huku serikali na wakazi wa dunia kwa ujumla wakitolewa wito kuwasaidia wanawake kuwanyonyesha watoto katika kipindi cha saa moja ya kwanza ya uhai wake.
Wataalam wanasema mguso wa mwili kwa mwili pamoja na kunyonya husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama , yakiwemo maziwa ya mwanzo kabisa ya mama baada ya kujifungua ambayo hutambuliwa kama''chanjo ya kwanza'' , yenye virutubisho vingi pamoja na kinga ya ya mwili.

NELSON CHAMISA APINGA USHINDI WA RAISI EMMERSON MNANGAGWA

Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Haki miliki ya pi
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe amepinga ushindi wa rais Emmerson Mnangagwa akisema matokeo yaliotolewa ni bandia.
Mnanganga alitangazwa mshindi kwa mara ya kwanza tangu kung'atuliwa kwa rais Robert Mugabe.
Chama cha Nelson Chamisa MDC Allkiance kimeapa kwenda mahakamani kupinga uchaguzi huo akisema kuwa kura hiyo ilifanyiwa udanganyifu.
Bwana Mnangagwa amewatalka raia wa Zimbabwe kuungana nyumba ya uongozi wake.
Maafisa wa polisi wanaendelea kupiga doria katika barabara za mji wa Harare baada ya maandamano kusababisha vifo vya watu sita.
Usalama umeimarishwa nje ya afisi za MDC mjini HarareHaki miliki ya pichaEPA
Image captionUsalama umeimarishwa nje ya afisi za MDC mjini Harare
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa gari la polisi lililokuwa na kipaza sauti lilizunguka likisambaza ujumbe kwamba 'Zimbabwe iko wazi kwa biashara'.
''Tuko hapa kuwalinda .Jisikieni huru mutembee na kufungua biashara, kila kitu kiko shwari musiogope''.
Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura kwa asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise.
Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo.
Hatahivyo Mwenyekiti wa chama cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki.
Kwa ushindi wa asilimia 50 wa Mnangagwa umesababisha aepuke kwenda duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya Chamisa.
Rais Mnangagwa amesema katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huu ni mwamzo mpya.

MOISE KATUMBI AZUIWA KUINGIA DR CONGO

Moise Katumbi aliondoka DRC mnamo Mei 2016, siku moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake
Haki miliki ya pichaREUTERS
Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Moise Katumbi umerudi nchini Zambia baada ya serikali ya DR Congo kumzuia kuingia nchini humo.
Alikuwa amekwama mpakani kati ya mataifa hayo mawili kwa saa kadhaa .
Mwandani huyo wa karibu wa rais Kabila amekuwa akiishi mafichoni kwa miaka miwili na alikuwa na matumaini ya kurudi nyumbani ili kuwania urais.
Awali kiongozi huyo alikuwa amevuka na kuingia eneo lisilodhibitiwa na nchi yoyote kati ya mpaka wa zambia na taifa la DR Congo huku maelfu ya wafuasi wake wakielekea katika eneo hilo kumlaki.
Alikuwa katika mji wa Kasumbalesa, kulingana na mwandishi wa BBC Anne Soy. Awali tuliwanukuu wafuasi wake wakisema kuwa alikuwa amevuka mpaka na kuingi nchini DR Congo.
Mji wa Kasumbalesa upo takriban kilomita 95 karibu na nyumbani kwao Lubumbashi.
Vikosi vya DR Congo vilifyatua risasi hewani kuwatawanya wafuasi wake waliosubiri kumkaribisha akijaribu kuvuka mpaja kulingana na mwandishi wa BBC Poly Muzalia.
Wafuasi wake wanasema alikuwa amevuka mpaka na kuingia nchini humo akiabiri gari lililotoka Zambia licha ya utawala wa taifa hilo kutishia kumkamata iwapo angejaribu kurudi nyumbani.
Kundi la chama cha bwana Katumbi Ensemble pour le Changement, lilichapisha kanda ya video ya bwana katumbi akiwa katika eneo la Kasumbalesa , mji wa mpakani nchini DR Congo.
Moise Katumbi, alikuwa amezuiwa kurudi nchini kugombea urais katika uchaguzi mkuu Desemba mwaka huu.

Thursday, 2 August 2018

ZANZIBAR VS INDONESIA NI MAENDELEO TU.

PichaKutoka habari leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Indonesia, Muhammad Jusuf Kalla. Viongozi hao wamesisitiza haja ya kuzidisha ushirikiano katika maendeleo.
Viongozi hao walizungumza Ofisi ya Kalla mjini Jakarta Indonesia na mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri wa pande zote mbili.
Rais Dk Shein alimpongeza Makamu wa Rais wa Indonesia kwa mwaliko wake huo muhimu unaoimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Indonesia, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla na makhsusi kwa Zanzibar.
Alimweleza makamu huyo wa Rais Tanzania inajivunia kwa kiasi kikubwa uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo ulioasisiwa na viongozi wa nchi hizo tangu miaka ya 60 na kuahidi utaendelezwa.
Alisema tangu mwaka 1964 kulikuwa na uhusiano na ushirikiano mkubwa wa Zanzibar na Indonesia katika biashara ya karafuu ambapo zao hilo lilikuwa likizalishwa kwa wingi zaidi na bei yake ilikuwa juu katika soko la dunia Indonesia, ikiwa moja ya wanunuzi wakubwa.
Dk Shein alieleza Indonesia imekuwa ikiunga mkono juhudi za Zanzibar kwa kusaidia maeneo mbali mbali ikiwemo kuwajengea uwezo wananchi katika elimu na kilimo na kusisitiza haja kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano.
Kwa upande wa kilimo, Rais Dk Shein alieleza haja ya kuongeza uzalishaji mpunga sambamba na kuangalia kilimo cha mwani na mazao yake.
Dk Shein alieleza haja ya kuirejesha biashara ya karafuu na kuwawezesha vijana kujiajiri katika kilimo kwa kuwapatia taaluma ya teknolojia mpya kwenye kilimo cha mikarafuu.
Katika uvuvi, eneo jipya la ushirikiano, Rais Dk Shein alieleza kuwa ni vyema na eneo hilo likaangaliwa kwa upeo mkubwa zaidi hasa katika kuimarisha uvuvi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kuvua hasa katika bahari kuu.
Kuhusu sekta ya utalii, Rais Dk Shein alisema juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kuhakikisha watalii wanaongezeka ikizingatiwa sekta hiyo inachangia asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa fedha za kigeni sambamba na kuchangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa.
Kuhusu utalii kipengele cha ukarimu, alisema ni vyema ushirikiano ukaimarishwa kati ya pande mbili hizo hasa ikizingatiwa tayari Indonesia yenyewe imeshapata mafanikio makubwa.
Dk Shein alisema mbali na juhudi hizo pia, hatua za makusudi zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha utalii wa Zanzibar unatangazwa na kusisitiza ili utangazwe vizuri, ni vyema kukawa na njia nzuri za kuwasafirisha watalii.
Rais Dk Shein pia alitumia fursa hiyo kueleza haja ya kuwepo na kuimarisha ushirikiano wa nyanja ya utafiti na maendeleo ambalo ni eneo lingine la ushirikiano na kupelekea taasisi za elimu kuhusishwa ikiwemo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Taasisi ya Afya pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo.
Alisema taasisi hizo ni vyema zikashirikiana na na za Indonesia katika nyanja mbali mbali na kubadilishana taaluma na uzoefu chini ya Mpango wa Ushirikiano wa Nchi za Kusini mwa dunia katika utalii, kilimo, afya na elimu.
Dk Shein alieleza tayari Zanzibar ina vyuo vitatu vya Amali kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana wa kujiajiri, hivyo aliona haja kwa mawaziri husika kukutana pamoja kujadili namna bora ya kushirikiana katika nyanja hiyo.
Akieleza suala la uchumi wa kisasa, Rais Dk Shein alieleza umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano katika kuimarisha uchumi huo kwa kuangalia uwezekano kuwekeza katika miradi ya miundombinu kushirikiana na sekta binafsi.
Rais Dk Shein alimwalika Makamu huyo wa Rais wa Indonesia kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2019 ambapo kiongozi huyo alikubali mwaliko huo.
Makamu wa Rais wa Indonesia, Muhammad Jussuf Kalla alimpongeza Rais Dk Shein kwa kukubali mwaliko wake huo akisema Indonesia itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo ambao umewekwa na waasisi wa mataifa hayo.
Alisema uhusiano huo ulianza kutoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Baba wa Taifa hilo, Soekarno Hatta.
Alisema kuna haja ya kuongeza ushirikiano hasa katika sekta ya biashara kati ya pande mbili hizo kutokana na soko kubwa la bidhaa za nchi hizo.
Kuhusu sekta ya utalii, alitaka ushirikiano kati ya pande mbili hizo utasaidia kuimarisha sekta hiyo hasa ikizingatiwa Zanzibar ina vivutio vingi vya kitalii zikiwemo fukwe nzuri.
Alieleza kutokana na Indonesia kuwa na Chuo Maalum cha Kitalii, wanaona iko haja ya kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta hiyo ya utalii katika nyanja ya mafunzo.
Aliahidi kuunga mkono uimarishaji sekta ya kilimo kwa kutoa mafunzo kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga na kueleza haja ya vijana wa Kizanzibari kwenda kujifunza nchini humo kutokana na nafasi maalum watakazozitoa.
Alisema Agosti 26 mwaka huu Indonesia itafanya mkutano wa kimataifa wa kilimo ambao utagusia kilimo cha mpunga na kutafuta njia za kuwasaidia vijana kujihusisha na kilimo.
Alitilia mkazo kubadilishana uzoefu kwa vijana huku akieleza namna ya kuwasaidia vijana kwa kuwapa ufadhili kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo utalii, uvuvi, mifugo na kilimo.
Alisema nchi yake imekuwa ikitoa mafunzo ya amali kwa vijana na mbali ya mafunzo hayo pia, wataongeza maeneo mengine ya uvuvi, utalii, mifugo, kilimo kwa vijana wa Zanzibar.

SIMBA KUIALIKA ASANTE KOTOKO KUTOKA GHANA "SIMBA DAY"

Kutoka Habari Leo.
Picha

MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba, wameialika Asante Kotoko ya Ghana kucheza nayo mechi ya kirafiki katika kilele cha maadhimisho ya Simba Day Agosti 8, mwaka huu.
Simba hufanya tamasha hilo Agosti ya kila mwaka ambapo kabla ya kufikia kilele tarehe nane, hufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kumalizia na kucheza mechi ambapo pia hutambulisha kikosi chake pamoja na jezi watakazotumia kwa msimu mpya.
Akizungumzia mechi hiyo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema wamechagua Asante Kotoko kutokana na historia yake ya kufanya vizuri ukanda wa Afrika Magharibi na michuano ya Klabu bingwa Afrika.
“Hii ni timu kubwa Afrika na inatajwa kuwa klabu namba moja kwa Ghana, na namba mbili kwa Afrika katika karne ya 20 nyuma ya Al Ahly ya Misri,” alisema.
Alisema timu hiyo iliwahi kucheza na Yanga mwaka 1969 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kutoka sare mechi zote mbili nyumbani na ugenini.
Pia, iliwahi kuchukua mataji mawili ya Afrika mwaka 1970 na 1983 na Ligi Kuu ya Ghana mara 24, mara ya mwisho ilikuwa msimu wa mwaka 2013/2014.
Kwa sasa wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Uturuki na wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki hii tayari kwa tamasha hilo.
Kuhusu tamasha la wiki ya Simba, Mratibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajula alisema watatumia wiki hii kutambulisha jezi za nyumbani na ugenini keshokutwa.
Amesema pia, maveterani wa klabu hiyo watawatembelea wenzao wa Yanga na kuchangia damu kwenye matawi, kutembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada na shughuli nyingine mbalimbali.
Kajula amesema, baada ya mchezo siku hiyo ya tamasha kutakuwa na hafla ya chakula cha jioni itakayohudhuriwa na mashabiki, wachezaji na wadau kwa ajili ya kuwashukuru wachezaji