Maduka yafungwa Harare huku jeshi likipiga doria
Wanajeshi waliojihami wamepiga doria wakiwataka raia kuwa na nidhamu.Watu watatu waliuawa mjini humo siku ya Jumatano wakati wa ghasia kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nelson Chamisa.
Bwana Chamisa alisema siku ya Jumatatu kwamba uchaguzi huo wa Jumamosi ulifanyiwa udanganyifu ili kumpatia rais Mnangagwa ushindi.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung'atuliwa madarakani.Biashara zimefungwa katika mji mkuu wa Zimbabwe harare huku taifa hilo likisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg