MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba, wameialika Asante Kotoko ya Ghana kucheza nayo mechi ya kirafiki katika kilele cha maadhimisho ya Simba Day Agosti 8, mwaka huu.
Simba hufanya tamasha hilo Agosti ya kila mwaka ambapo kabla ya kufikia kilele tarehe nane, hufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kumalizia na kucheza mechi ambapo pia hutambulisha kikosi chake pamoja na jezi watakazotumia kwa msimu mpya.
Akizungumzia mechi hiyo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema wamechagua Asante Kotoko kutokana na historia yake ya kufanya vizuri ukanda wa Afrika Magharibi na michuano ya Klabu bingwa Afrika.
“Hii ni timu kubwa Afrika na inatajwa kuwa klabu namba moja kwa Ghana, na namba mbili kwa Afrika katika karne ya 20 nyuma ya Al Ahly ya Misri,” alisema.
Alisema timu hiyo iliwahi kucheza na Yanga mwaka 1969 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kutoka sare mechi zote mbili nyumbani na ugenini.
Pia, iliwahi kuchukua mataji mawili ya Afrika mwaka 1970 na 1983 na Ligi Kuu ya Ghana mara 24, mara ya mwisho ilikuwa msimu wa mwaka 2013/2014.
Kwa sasa wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Uturuki na wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki hii tayari kwa tamasha hilo.
Kuhusu tamasha la wiki ya Simba, Mratibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajula alisema watatumia wiki hii kutambulisha jezi za nyumbani na ugenini keshokutwa.
Amesema pia, maveterani wa klabu hiyo watawatembelea wenzao wa Yanga na kuchangia damu kwenye matawi, kutembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada na shughuli nyingine mbalimbali.
Kajula amesema, baada ya mchezo siku hiyo ya tamasha kutakuwa na hafla ya chakula cha jioni itakayohudhuriwa na mashabiki, wachezaji na wadau kwa ajili ya kuwashukuru wachezaji
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg