YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 7 September 2013

MSIKITI WA ANSWAR SUNNA ULIOPO MJINI DODOMA WATEKETEA KWA MOTO


Msikiti mkubwa wa Answar Sunna  uliopo  barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika....

Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mpekuzi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo...

Hata  hivyo, shuhuda  mwingine  aliyeongea  na  mtandao  huu  amedai    kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  hitilafu  ya  umeme  iliyoanzia  ghorofa  ya  juu  ya  jengo  hilo. 
 
Kwa  mujibu  wa  mashuhuda  hao, moto  huo  umefanikiwa  kudhibitiwa  na  jeshi  la  zima  moto  na  kwamba  hakuna  mtu  aliyepoteza  maisha  kutokana  na  moto  huo.

  <<seemoresearchbongo>>
You might also like:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 07/9/2013 YA HABARI,UDAKU NA MICHEZO



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
. 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
You m

PICHA 5 ZA DAKTARI FEKI ALIYENASWA AKIHUDUMIA WAGONJWA KWENYE HOSPITALI YA KCMC...!!



Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'.
Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe.
Daktari Feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituoni.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33).
Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000.

Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha kwa madai zitatumika kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji.

Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari.

AIBU..!. MUME AMRUHUSU MKEWE AJIUZE ILI WAPATE PESA YA CHAKULA...!



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina.
Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.

Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya wanahabari  kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.

Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:

“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.


“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili nije kupata pesa.”


Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa ameshikilia upande wa khanga.

Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali wa kamera   walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai hayawahusu .

MTEGO MZITO BAADA YA KUPEWA AHADI YA MILION 3.5 KULALA NA BOSI WAKE MPAKA ASUBUHI...!!




Salam kwa wana jamvi wote!
Napenda kutoa funzo moja hapa! Ila sio msimulizi mzuri sana lakini naamini nitaeleweka tuuu....
Mimi na rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki baada ya kuajiriwa siku moja hapa jijini!
Kwa kweli, bila hata kumaliza mwenzi mmoja the big boss akaanza kutupa mawe kwa rafiki yangu huyu ila hakuniambia kama boss anataka kungonoka! Ila binti akamtolea nje!!
Alipo ona yamashindikana kule si ndoo akaamua ahamie kwangu kujaribu bahati yake, mimi nisivyo na siri nikaona nimshirikishe huyu rafiki yangu si ndo akafunguka nami nikajua kuwa boss ana mchezo mchafu!!
Nikamwambia hakuna dinner atakayo nialika nikaenda ila mwenzangu vi dinner alikuwa havikosi!
Ila anavyo sema rafiki yangu hajawahi ku do naye!!!!!
Sasa wiki hii, boss kanivulia uvivu macho kodo kwangu kila wakati, mara ohooo leo umependeza sana ohoo you luk scorching gorgeous hajui mwenzie najua kuwa tabia yake ni hafu!
Sasa jana si akanipigia simu after work twende kwa coffe enening coloessum, kwa kuwa ilikuwa mapema nikasema kwa nini niwahi home hivi!
After those thoughts na maamuzi ya kwenda binti nikamwambia poa not a big deal, nikamtonya shosti yangu akaniambia usiogope nothing he shall do to you! Hao mpaka coloessum
After coffee akasema twende ukaone mahali ninapoishi nkamwambia poa............
Kufika hapo, akaanza can we spend a night together tomorrow?
Nikamwambia what will be the reward? huwezi nikunja usiku mzima for nothing atiiiii, cause i know hakuna love!!
Boss aka offer 500,000/ nikamwambia labda millioni tano!!!!!
Kapanda mpaka 3.5 mil nikasema 5 mil cash final + HIV test!
Akasema hapana that is too much! nIkamwambia then call it a day and take me home!!!!!!
Sasa this morning at work he texted me, the offer is granted come and pick your cash!!!!!!
Nimeenda kwa ofisi nikamwambia my mind has changed keep your dirty money with you!!!!!
He looked at me with a surprise usoni, I told him i thought few days after the incident will i be able to work again and a thought mapenzi ofisini ni upuuzi mtupu!!!!!
He said good thoughts, u re too emotional!
He ended we shall be always frends & anything you nid just tell me will be glad to help!!!

JINSI MSANII BATULI ALIVYONASWA LIVE NA SLIMU OMARY WAKIWA SEHEMU TATA....!!


Msanii wa bongo movie Yobi nesh au Batuli katika pozi
 Hivi ndivyo thesuperstarstz ilivyowanasa wasanii hawa maarufu katika maeneo ambayo ni ngumu kuwakuta wawili hao,mwanzoni mwandishi wa habari hizi alijua wana rekodi filamu ila alipowasogelea  akagundua hapakuwa na kamera yoyote katika eneo lile kitu kilichompa maswali mengi sana na kujikuta akipata hamu ya kutaka kujua kulikoni wawili hawa kuwa close namna ile.

Mwandishi wa tsstz alijibanza asijulikane kama yupo eneo lile na hapo alimshuhudia slim omari msanii wa bongo movie akizidi kumsomesha Batuli ili akubaliane na anachomueleza japo hatukupata bahati ya kusikia walichokuwa wanaongea kwani wangejua nipo eneo lile.

Mara baada ya kupata picha za uhakika thesuperstarstz iliwafuata wawili hao na walipomuona muandishi wetu waliachina mikono haraka na kuanza kucheka huku slimu akionyesha kutokuamini kama  amebambwa na muandishi wetu na kisha wakaondoka haraka eneo lile nakuingia katika mlango flan kwa staili ya kumkwepa muandishi wetu na tulipowafuata tulizuiliwa na ungozi wa eneo lile kwa madai ya kuwabuguthi wateja wao.
Hapa ni mwanzo Batuli alionekana kufurahiya maneno ya slimu
Bado thesupestarstz inalifuatilia swala hili kwa kina kutaka kujua kulikoni maana hata simu hawapokei hata tulipojaribu kubadili namba tulimpata Batuli na tulipomsomea mashtaka yake alicheka na kusema wacha zako bwana hiyo ni kikazi zaid wala hakuna jipya  tulipombana zaidi alisema tumtafute hawezi kuongea kwenye simu
baada ya kukata simu tulipigiaslimu na  kwa upande wake hakutaka kupokea simu yetu
Hapa Slim Anaonyesha aliongeza utamu wa maneno na kumfanya Batuli aanze kuingia mkenge kwa maneno yake
Endelea kuwa nasi tutahakikisha tunakuletea kilichojiri kwani kazi yetu ni kukupa habari popote pale ulipo nataka ujue hii sio filamu mdau ni tukio la kweli kaaa na sisi

DRAMA ZA WEMA SEPETU ZAGONGA MWAMBA MBELE YA LULU.


Wema Sepetu anadaiwa kutaka kuitawala katika media shughuli nzima ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ambayo Elizabeth Michael(Lulu) na Diana Kimaro ni moja wa waigizaji wakuu wa filamu hiyo. Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika tarehe 30 mwezi wa 8 Mlimani City, Dar es salaam. Muigizaji mmoja wa kike maarufu ambaye alikuwepo ukumbini hapo siku ya uzinduzi huo
akizungumza na Swahiliworldplanet alisema kuwa hakuona umuhimu wowote wa Wema kujichetua namna alivyofanya wakati shughuli ilikuwa ya Lulu, alisema kuwa kitendo cha kwenda kumpa pesa Mama Kanumba hakikuwa na maana pale mbele za watu bali kujichoresha kwenye media ili auze magazeti kama kawaida. " Wema nae haachi kujichetua kila siku, shughuli ni ya mwenzake lakini alitaka kila mtu ajue kuwa Wema yupo ukumbini, kama alikuwa na nia ya kumpa mama kanumba pesa si anagempa tu nyumbani kwake au anataka attention kila alipo."

Muigizaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa Wema ni mtu wa kumwaga pesa huku akishindwa kutoa filamu yoyote mpaka sasa kupitia kampuni yake iliyozinduliwa kwa kishindo mwanzoni mwa mwaka huu wakati mwenzake Lulu akizindua filamu yake na tayari ipo sokoni kwasasa huku ile ya Wema ya Superstar iliyozinduliwa kwa gharama kubwa na kutangazwa sana haijulikani ilipo mpaka leo. " mpaka sasa Wema hajatoa filamu yoyote na hata ile tuliyohudhuria uzinduzi wake mwaka jana kwa kumleta Omotola sijui kamuuzia nani, ajipange kama mwenzake,  unajua Wema alitaka kuitawala ile event kupitia media kwa kumfunika Lulu lakini Lulu alifunika siwamjua Lulu tena, shosti yake Kajala pia hakujituliza kitini mbona mastaa wengine walikuwepo bila drama zozote!" alisema muigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake akizungumza na Swahiliworldplanet.

Wema, Kajala na mama Kanumba katika uzinduzi wa filamu hiyo
source- swahiliworldplanet