YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 15 June 2013

Wananchi Arumeru wateketeza shamba la mwekezaji



Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku nyumbani kwa mwekezaji huyo, Ikbar Abdalah (53)ambaye ni mkulima mwenye asili ya Kiasia na mkazi wa kijiji hicho.

Arusha. Wananchi zaidi ya 1000 wa kijiji cha kwa Ugoro wilayani Arumeru, wamevamia shamba la mwekezaji na kuliteketeza kwa moto na kupora bidhaa mbalimbali mali za mwekezaji huyo zenye thamani ya mamilioni ya fedha.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3.30 usiku nyumbani kwa mwekezaji huyo, Ikbar Abdalah (53)ambaye ni mkulima mwenye asili ya Kiasia na mkazi wa kijiji hicho.
Katika tukio hilo wanakijiji hao walichoma nyumba yake,mabanda mawili, trekta moja chakavu,mashine ya kusaga nafaka,spea za magari na kupora vitu mbalimbali ikiwamo pikipiki moja aina ya Honda.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas ,chanzo cha uharibifu huo ni mgogoro wa muda mrefu kati ya wanakijiji hao na mwekezaji wa kugombea eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 100 linalomilikiwa na mwekezaji huyo.
Alifafanua kuwa viongozi wa eneo hilo walidai kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu, kiasi cha kufikisha suala hilo ngazi ya mahakama na kwamba kesi hiyo ilishawahi kutolewa uamuzi mara mbili na sasa iko ngazi ya rufaa.
Hata hivyo, polisi ilifanikiwa kumnasa mwanakijiji mmoja (jina linahifadhiwa na polisi) anayeshikiliwa katika kituo cha polisi jijini hapa huku wengine wakiendelea kusakwa kutokana na kutenda kosa la kujichukulia sheria mkononi.
Wakati huo huo, Kamanda Sabasi ametoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote cha watu watakaojihusisha na matukio ya kuvuruga uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Juni 16 mwaka huu
.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg