YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 17 August 2018

MAREKANI NA CHAGUZI ZA TANZANIA

Ni dhahiri kuwa Tanzania na Marekani zimeingia katika majibizano ya kidiplomasia kutokana na mwenendo wa chaguzi ndogo zilizofanyika mnamo Agosti 12.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani Agosti 15 jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Buyungu na kata za udiwani 36 ulikumbwa na kasoro nyingi.
Tamko la ubalozi ambalo wameliita la 'masikitiko' limetaja kasoro hizo kuwa ni vurugu zilizohusiana na uchaguzi, ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani.
Kasoro nyingine zilizotajwa na ubalozi huo ni vitisho vya polisi dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani, watu kukamatwa kiholela bila kuwepo vibali vya ukamataji na kukandamizwa kwa uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni katika kipindi chote kuelekea chaguzi hizo.
"Mambo haya yanakwaza haki ambazo Katiba ya Tanzania imewapa raia wake na kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini na katika eneo lote la kanda," ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliibua Tume ya Uchaguzi (NEC) klicha ya kukanusha tuhuma hizo ilihoji uhalali wa Marekani kuhoji juu ya uendeshwaji wa chaguzi ndogo nchini Tanzania.
Taarifa ya NEC imesema kuwa hapakuwa na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa na kuutaka ubalozi wa huo uleleza umepata vipi taarifa hizo na kwa kutumia utaratibu na sheria gani.
Je, Marekani imeingilia mambo ya ndani ya Tanzania?Haki miliki ya picha
Image captionJe, Marekani imeingilia mambo ya ndani ya Tanzania?
"…Buyungu mgombea wa ubunge mmoja wapo (Chadema) alijitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii akaeleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo…" inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza, "Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani, mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura."
Taarifa ya NEC pia imesema hakuna chama chochote cha siasa kilichojitokeza na kuthibitisha kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki.
Hata hivyo, Chama ca ACT-Wazalendo hata kabla ya matamko ya ubalozi na NEC walitoa tathmini yao na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo kimesema haitatumia mabavu wakati wa uchaguzi.
Chama hicho kimetoa kauli hiyo kikidai kuwa uchaguzi huo wa mdogo wa Agosti 12 ulivurugwa.
CCM ilishinda kiti cha ubunge Buyungu na kata 77. Hatahivyo kati ya kata 77, uchaguzi umefanyika katika kata 36 tu huku katika kata 41 wagombea wa CCM walipia bila kupingwa.
Je, Marekani imeingilia mambo ya ndani ya Tanzania?
Ni mwiko kidiplomasia kwa nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine, lakini je, Marekani imeingilia mabmbo ya ndani ya Tanzania kwa tamko lao?
Akijibu swali hilo, mhadhiri wa sayansi ya siasa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt Richard Mbunda amesema japo hatua hiyo ya Marekani kidiplomasia ni ya kushtua, lakini haishangazi.
"Marekani wamekuwa wakijipambanua duniani kote kama walinzi wa demokrasia, hivyo haishangazi wao kutoa tamko juu ya jambo hili," amesema Dkt Mbunda na kuongeza "uchaguzi huu na kishindo chake ni sehemu tu ya wimbi kubwa la kisiasa linaloendelea nchini, ikiwemo kuhama kwa viongozi wa upinzani kwenda CCM. Wimbi hili limekuwa likitiliwa shaka juu ya uhalali wake na kama kama ni kweli sababu pekee ya hama hama hiyo ni kutekeleza utashi wa wanasiasa hao unaolindwa kikatiba."
Mhadhiri wa masuala ya diplomasia kutoka kituo cha diplomasia (CFR) Dar es Salaam Godwin Gonde, ameiambia BBC kuwa tathmini yake ni kuwa Marekani ilikuwa na mengi ya kusema juu ya hali ya kisisasa nchini Tanzania lakini ilikuwa ikitafuta upenyo.
"Tamko lao (ubalozi wa Marekani) halibadili matokeo ya chaguzi, bali wanajaribu kuiambia serikali kuwa wapo macho na wanatazama kila kinachoendelea."
Gonde amesema katika hali ya kawaida, balozi ama jumuiya ya kimataifa haingalii chaguzi ndogo na ndio maana Marekani hawakutoa tamko lao wakati hatua za uchaguzi zikiendelea kwa sababu hawakuwepo kwenye maeneo ya uchaguzi.
"Tafsiri ya wazi ni kuwa wameingilia mambo ya ndani ya Tanzania, wameeleza sababu zao, lakini hapa itategemea na serikali ya Tanzania itataka kuliendea jambo hili, inaweza ikawa ni mwanzo wa msuguano."

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg