YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 19 September 2013

AIBU!! MKE ASHIKWA UGONI NA WAKWE ZAKE AKIWA NA DEREVA WA BODABODA,MUME AANGUA KILIO....!!




WAZAZI wa mwanamme aliyejulikana kwa jina la Ally Maulidi Kambi, wakazi wa Kibada jijini Dar es Salaam wamemshika ugoni Farida Omar ambaye walidai ni mke wa Ally akiwa na dereva wa bodaboda, Risasi Mchanganyiko linakujuza mwanzo mwisho.
  Farida Omar akiwa na dereva bodaboda aitwaye Chidi baada ya kushikwa ugoni.
Tukio hilo la aibu lilijiri usiku wa Septemba 15, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kibada ambayo anaishi dereva huyo aliyejulikana kwa jina moja la Chidi.
KISA CHA UGONI
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kunaswa kwa Farida kulitokana na familia ya mumewe kutilia shaka nyendo za mwanamke huyo, hususan mumewe anapokuwa safarini.
“Wakwe zake, wakiwemo mashemeji na mawifi walishaziona nyendo za Farida kuwa si za kiuadilifu hasa mume wake anapokuwa safarini,” kilisema chanzo hicho.

 Mke akiwa chumbani kwa Chidi baada ya kunaswa na wakwe zake.
Kikaongeza kuwa mara nyingi mume akisafiri mwanamke huyo huenda kuishi na mwanamme mwingine mpaka mumewe anaporudi, hali ambayo imezua minong’ono mitaani kwa wale waliofanikiwa kujua hilo.
Maelezo ya wazi kutoka kwa vyanzo ni kwamba, chumba anachoishi Chidi kilipangwa na mwanamke mwingine na baadaye kumwachia Farida ili atanulie kiaina.

               Chumbani kwa Chidi alipokutwa Farida Omar.
WAKWE WAONGEA KWA JAZBA
Wakizungumza kwa jazba siku ya tukio, wakwe wa Farida ambao ni wazazi wa Ally walisema mwanamke huyo aliyeolewa na mtoto wao miaka mitano iliyopita, amekuwa si mwaminifu kwa mumewe hasa anapokwenda nje ya nchi, habari ambazo wao walizisikia na kuzifanyia kazi.
Waliongeza kuwa kutokana na tabia hiyo chafu, walijaribu kumuweka kikao mumewe na kumpasulia kila kitu lakini jamaa huyo hakuwa akiwaamini, alidhani ni roho mbaya zao tu.
 
SHEMEJI MTU APIGILIA MSUMARI
Wakati wazazi wakiongea hayo, shemeji mmoja wa Farida, yaani kaka wa Ally alidakia na kusema kuwa baada ya ndugu yao kwenda Kongo kikazi, Farida naye aliondoka nyumbani hapo bila kuaga na alipomtafuta kwa njia ya simu yake ya mkononi, mwanamke huyo alijibu kuwa yupo kwa mama yake mzazi, Kivule, Dar.
Msome shemeji mtu hapa: “Siku moja nikiwa katika safari zangu za usiku, nilimuona Farida akiwa na kijana anayeitwa Chidi.
“Niliamua kuwafuatilia nyendo zao kwa vile tayari tabia yake ilikuwa inajulikana. Niligundua kuwa alikuwa anaishi na kijana huyo kwenye chumba kimoja ambacho mwanamke huyo ndiye aliyekipanga. Hebu fikiria mke anapanga chumba nje ili awe anasalitia!”
Shemeji mtu huyo akaendelea kusema kuwa baada ya kukigundua chumba hicho, yeye na ndugu wengine walikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Saidi Juma Mpili ambaye aliwathibitisha kuwa ni kweli Farida anaishi na Chidi japokuwa chumba kilipangishwa kwa jina la mtu mwingine.
 
MTEGO WAWEKWA
Baada ya kuthibitishiwa hivyo, familia hiyo iliwasiliana na mapaparazi kwa lengo la kuwanasa wawili hao ambao kwa muda huo walikuwa mitaani wakitanua.
Kwa ushirikiano wa familia, mapaparazi na mjumbe huyo mtego uliwekwa na baada ya muda Chidi na Farida waliwasili wakiwa kwenye pikipiki bila kujua wako ndani ya kumi na nane ya wakwe zake.
 
WABANWA LAIVU
Nje ya nyumba hiyo, wawili hao walibanwa na kuulizwa uhusiano wao ambapo Chidi alisema yeye ni kaka wa hiyari wa Farida na kukataa kwamba wanaishi pamoja, utetezi ambao uliwapandisha hasira wakwe hao na kumwomba mjumbe wapekue chumbani ili kujiridhisha kuwa hawaishi pamoja.
 
FARIDA AWAPOTOSHA WAKWE ZAKE
Farida ndiye aliyeongoza msafara wa kuingia ndani akifuatiwa na jamaa yake, lakini cha ajabu aliwapotosha ndugu wa mume kwa kuwaingiza ndani ya chumba cha mpangaji mmoja akidai ni chake, jambo ambalo lilishtukiwa na mapaparazi wetu waliokuwa wameshafanya uchunguzi wa kutosha kabla.
Farida aliambiwa chumba hicho sicho, wakamtaka aoneshe chake ndipo akaenda kuingia huko ambako zilionekana suruali aina ya ‘jeans’ za Chidi na makoti mengi ya kuendeshea bodaboda ambayo yalitoa ushahidi kuwa watu hao wanaishi pamoja humo.
 
BAADA YA UTHIBITISHO, MUME AJULISHWA KWA SIMU, ALIA
Kufuatia ushahidi huo na Farida mwenyewe kukiri, ndugu walimwendea hewani mume wa mwanamke huyo, yaani Ally na kumtumbulia siri hiyo nzito ambapo alilia kwenye simu.
 
HUENDA ILIKUWA HIVI
Katika kupashana huko, huenda kaka mtu ndiye aliyepiga simu na kusema hivi:
“Haloo dogo.”
Ally: Ee bro, shikamoo.”
“Marhaba. Nakutaarifu kuwa tumemfumania mkeo akiwa kwa kijana mwendesha bodaboda.”
Ally: Nini? Kweli bro?
Bro: Kweli dogo, hivi ninavyoongea na wewe tupo hapa, mama, mama mdogo na sista.
Ally: (kilio).
 
ALICHOKISEMA MUME
Akizungumza baada ya kupata taarifa za kubambwa  kwa mke wake na Chidi, mume wa Farida alisema akiwa nchini Kongo mkewe alimuaga anakwenda kwa mama yake Kivule na hatambui kama alikuwa amepanga chumba na kuishi na mwanaume mwingine, jambo alilosema limemshangaza sana.
Ally akaulizwa atachukua uamuzi gani baada ya tukio hilo, akajibu huku akilia na kusema atarejea Bongo kumaliza suala hilo mwenyewe kisha akakata simu huku sauti ya kilio ikimalizikia kusikika kwa mbali hali iliyowafanya ndugu zake washikwe na  huzuni.
 
FARIDA AOGOPA KUONDOKA NA WAKWE ZAKE
Baada ya tukio zima kukamilika, Farida aligoma kuondoka na wakwe zake akidai kwamba anahofia watakwenda kumpiga au kumfanyia jambo lolote baya kutokana na kitendo alichomfanyia mtoto wao, lakini akafunguka kwamba bado anampenda mumewe na hataki kupewa talaka.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg