YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 9 March 2014

PICHAZ..KUFURU KUBWA YA BONGO MOVIE AMBAYO INASHIKA REKODI MPAKA SASA...ILIKUWA NI FULL AIBU AISEEE....!!


ILITOKEA NA SIDHANI KAMA ITAKUJA TOKEA TENA KAMA HII, MAYBE BAADAE SANA..SHUKA NAYO HAPA CHINI
Ziara ya mastaa wa filamu Dodoma ni kufuru, fedha ilitumika, wasanii wajiachia kimapenzi wao kwa wao, wengine nusu wazipige.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda lina ‘full nondoz’ hatua kwa hatua ndani ya Dom kama ifuatavyo.


FULL KUJIACHIA
Baada ya mechi na wabunge iliyochukua nafasi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dom, wasanii walijigawa makundi mawili.
Kundi A ambalo lilitinga mjengoni na magari ya kifahari lilibaki na kugeuka Dar asubuhi ya Jumatatu (Juni 20), wakati Kundi B, walinyanyuka himahima Jumapili (Juni 19) saa 6:00 mchana.
Kundi B lilikuwa na wanaume wengi zaidi, wao waliambiwa wawahi Dar kwa sababu basi dogo walilokuwa wanalitumia lilikuwa linahitajika jijini.

Baada ya Kundi A kuondoka, Kundi A walijiachia ‘kinoma noma’ kwenye bwawa la kuogolea la Hoteli ya African Dream ambayo walifikia.
Katika bwawa hilo, mastaa ‘walishoo lavu’ kwa kuoga pamoja na kufurahi kwa michezo mbalimbali.

Wale waliokuwa hawataki kuingia majini, walisukumwa bwawani na nguo zao.
Mtiti uliibuka pale mchekeshaji Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ alipomvaa Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ na kutaka kumtupia majini.
Vincent Kigosi ‘Ray’ naye aliongezeka kumsaidia Steve lakini baadaye timbwili hilo lilimalizwa na Mwenyekiti wa Klabu, Hartmann Mbilinyi aliyewatawanya.

TIMBWILI LA POSHO
Wasanii wote walipanga kuondoka Dom Jumatatu ya Juni 20 lakini tangazo kuwa basi dogo ni lazima liondoke Jumapili, liliwanyong’onyesha wengi, kwa hiyo ulianza mvutano wa nani atangulie, nani abaki.
 
 
Baada ya viongozi kubainisha wanaopaswa kutangulia na wengine wabaki, wale walioambiwa waondoke siku hiyo na basi, baadhi yao walianzisha timbwili la kudai posho.
Madai ya posho yalichochea hasira kwa viongozi na kusababisha Kiongozi wa Nidhamu, Issa Musa ‘Cloud’ kutaka kuzipiga na Soud Ally lakini Katibu, Salum Mchoma ‘Chiki’ alitumia busara kuwatuliza.
 
 
WAHESHIMIWA MACHO JUU
Kwa muda ambao wasanii hao walikuwa Dom, baadhi ya wabunge walikosa utulivu, wakipigana vikumbo jinsi ya kunasa mapenzi.
Baadhi ya wasanii walikamatika kutokana na uhuru uliokuwepo, kwani hakukuwa na kizuizi cha mtu kutoka na kwenda kupiga misele anapopataka.

NANI ANASEMA WASANII WA KIKE WANAUZWA?
Uchunguzi umeonesha kuwa baadhi ya wasanii wanajiuza wenyewe na wakati mwingine hutangaza ‘teni pasenti’ kwa mtu anayewasaidia kuwaweka kwa wafanyabiashara au wanasiasa wenye fedha.

Mbunge mmoja aliliambia gazeti hili kuwa alipigiwa simu na mrembo mmoja wa Klabu ya Bongo Movie akaomba kuwa naye karibu.

“Ni kama shule, kuna watu wazuri lakini wengine wabaya sana. Kuna mtoto nilikuwa namheshimu lakini alinipigia simu ananitongoza. Amenikera kweli, nilitaka kusaidia klabu yao lakini nimevunjika moyo kusaidia watu wa aina hiyo,” alisema mbunge huyo anayotokea moja ya majimbo ya Mkoa wa Morogoro.
 
 
JACK WOLPER BALAA
Jacqueline Wolper alitisha, kwani alitinga Dom akiwa na gari matata aina ya Toyota Land Cruiser V8, namba T 798 AXY na ndiye alikuwa ‘bei mbaya’ kuliko wenzake, kwani hata kambini alikuwa hakai.

SIKU MBILI WEMA HAONEKANI
Ijumaa (Juni 17) usiku, Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ walitinga Dom na kudondosha ‘shoo’ kwenye Ukumbi wa Kilimani, kwa hiyo wasanii wote waliingia kuona mambo wazee wa mjini.

Baadhi ya wasanii hao, walipotezana na Wema Sepetu kuanzia muda huo, siku iliyofuata ambayo ndiyo mechi ilifanyika Uwanja wa Jamhuri hakuonekana mpaka Jumapili.
Gazeti hili lilimnasa msanii Zuwena Yusuf ‘Shilole’ akimhoji Wema: “Ulikuwa wapi? Siku mbili hatujakuona.”
Wema alijibu kwa kifupi kuwa hakuwepo lakini mwandishi wetu alipomhoji ni kwa nini hakuonekana siku ya mechi na wabunge ambayo ndiyo iliyowapeleka Dom alijibu: “Nilikuwa naumwa mafua.”
Mwandishi: Hayo mafua ni jana tu, mbona leo mzima?
Wema: Aah bwana yaache hayo.

RATIBA YAO
Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla alikata zaidi ya shilingi 2,500,000 kulipia malazi ya wasanii hao kwenye hoteli hiyo.
Kila siku mchana, wasanii hao walikuwa wanakwenda kula nyumbani kwa Makalla mjini humo.Siku ya mechi, baada ya Bongo Movie kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Bunge Soka na 17-7 dhidi ya Bunge Netiboli, walialikwa nyumbani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambako walikula chakula cha usiku pamoja na kuzungumza mpaka usiku mkubwa ambapo walirejea hotelini

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg