YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday, 15 August 2012

MASWALI MANNE YALIYOJIBIWA NA PREZZO IKIWEMO MSHAHARA ANAOLIPWA SASA HIVI KAMA BALOZI.

Najua utakua umesikia sana stori mbalimbali za mshindi wa pili wa Big brother Africa Cmb Prezzo kutoka Kenya lakini nyingine hazina ukweli wowote.

Haya ni maswali manne aliyoyajibu kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Aug 14 2012.
1. Ni kweli kuhusu taarifa zilizoandikwa kwamba unalipwa shilingi milioni nne za Kenya kutokana na kuchaguliwa kuwa balozi?
“ningependa kumfahamisha kila mtu kwamba hii One campaign sio kampeni ya michuzi, ni kampeni ambayo mtu mwenyewe unajitolea kujaribu kuwasaidia kwenye ujumbe wao wanaousambaza, kama leo nimeona kwenye gazeti nikaangalia nikasema ehhh naomba kweli ingekua hivyo, sio kweli kwa sababu mshahara wangu ni kuona watu wanalala wamekula chakula na sio kulala njaa” – Prezzo
2. Kwa time hii kuna uwezekano ukaingia studio kurekodi single yoyote? utatumia studio gani pia?“sasa hivi nimepewa muda wa siku tatu za kupumzika kwa hiyo nazitumia kadri ya uwezo wangu ila baada ya hapo kazi lazima iendelee.. mi huwa sibagui studio lakini sanasana nitakua homeboys studios” – Prezzo
Unakwenda kwenye Consert ya Jay Z Marekani, kuna chochote umepanga kufanya nae?
“Kati ya watu ambao nawaheshimu Jay Z ni mmoja wao so huwezi kujua mwenyezi Mungu kapanga nini mbele ya safari, naamini Mungu anasababu yake kunifanya nipate nafasi kama hii, Mungu alikua ana sababu yake mimi kushinda namba mbili na Keagan kuwa wa kwanza” – Prezzo
Ni kazi gani utakua unafanya kwenye huu ubalozi wa kampeni ya One Campaign?
“Kama balozi wa One Campaign kwa miaka mitatu hivyo nitakua nasafiri kwa nchi tofauti kwenda kuangalia na kuwasaidia watu wenye upungufu wa chakula, lengo ni kumaliza ukame ambapo licha ya malipo kuna njia nyingi tu ambazo unaweza ukalipwa na kama tukiweza kufanikisha kila mtu akawa na chakula nadhani hakuna

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg