JARIDA maarufu la Times nchini Uganda limemtaja mama wa watoto wawili Zari Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo kwa wakati huu.
Kwa mujibu wa jarida hilo Zari (30) ambaye ni Mwanamuziki,Mfanyabiashara na Mtangazaji wa runinga amepata mafanikio makubwa kwenye muziki na pia kipindi chake cha runinga kinachofananishwa na kipindi cha ‘Keeping up with the Kardashians’ kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.
Huku likiambatanisha picha za magari na nyumba anazomiliki mwanadada huyo, jarida hilo limeandika kuwa huenda akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho endapo ataendelea na mwenendo wake wa sasa kibiashara.
hata hivyo jarida hilo pia limetaja zari kuwa mmoja wa mstaa wapenda starehe na amekuwa akitumia mkwanja alionao kumnasa mwanaume wa aina yoyote anahisi kuwa anahitaji kumliza kwa wakati huo ingwa tuhuma hizo hazikusibitishwa moja kwa moja.
katika hatua nyingine jarida hilo limesema kuwa Zari mwenye maskani yake pia nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa uganda kuzaliwa ispokuwa ni wahamiji kwani baba yake ni raia wa Buurundi mwenye asili ya Somalia na mama yake ni raia wa India kutoka kabila la Mutoroo.
Aidha Times limeandika kuwa Zari anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW – 2006, Black Chrysler – 2008, – Audi Q7 2010 Silver Crysler – 2008, JETTA-2006, Mercedes Benz convertible -2008. Range-Rover, Lamborghin, Hummer na mengine mengi huku pia akiwanaumiliki wa maduka, hotel na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria, Cape Town na Kampala.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg