MACHOZI ENTERTAINMENT
Box 3209, Dar es Salaam, Tanzania
KAMATI
ya maandalizi ya shindano la Miss Ilala 2012, kesho Alhamis saa 5
asubuhi, itatambulisha mbele ya wanahabari warembo 15, wanaowania
umalkia wa taji hilo, linaloshikiliwa na Vodacom Miss Tanzania, Salha
Israel.
Warembo
hao kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa
katika kambi hiyo kwa wiki mbili sasa na wamekuwa wakiendelea na mazoezi
katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, Dar es
Salaam sehemu ambayo kesho itatumika katika hafla hiyo fupi ya
utambulisho.
Miss
Ilala 2008, Slyvia Mashuda ndiye mkufunzi wa warembo hao na ikumbukwe
Slyvia alishika nafasi ya pili katika Miss Tanzania mwaka ambao Nasreen
Karim alitwaa taji la Miss Tanzania.
Wadhamini
waliothibitisha katika mashindano hayo ni pamoja na City Sports Lounge,
gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Uhuru One na 88.4
Cloud's FM na Redds Premmium Cold. Miss Ilala 2012 Itafanyika Septemba
7, mwaka huu katika sehemu ya nje ya Nyumbani Lounge.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg