Pichani juu askari wakikagua mwili wa Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia
Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Habari zaidi tuvute subra kidoogo, tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg