YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 29 December 2013

MAVAZI YA NUSU UCHI, MAUNO NA UFUNDI WA KUTUMIA VIUNGO UTAMPELEKA WAPI SNURA MUSHI WA MAJANGA NA WENZIE?

KWA wasiomfahamu msichana huyu, wanamuona kama chipukizi aliyeukwaa ustaa ghafla, lakini wanaofuatilia mambo ya sanaa na burudani, wanamfahamu kitambo. Ninamzungumzia Snura Mushi, ambaye anatamba sana na kibao chake cha Majanga...

Ni mmoja kati ya wasanii wapambanaji, wakisaka mafanikio kwa kujaribu kila aina ya njia. Amejaribu kwa muda mrefu katika filamu, lakini hakuweza kufanikiwa ‘kuchomoka’. Kama angetambua tokea mapema kuwa angeweza kuibuka mara moja katika muziki, nadhani asingepoteza muda wake mwingi kwenye filamu. 

Wimbo wake wa Majanga umeiteka familia ya muziki wa mduara, huenda kwa sasa ni mmoja kati ya wasanii wachache wanaopata nafasi ya kutakiwa sana katika majukwaa na hivyo kumfanya pia awe anapata hela za kutosha.

Katika uigizaji, alifanikiwa kucheza vizuri katika filamu kadhaa, ingawa kama ninavyosema mara zote, viwango vibovu vya sinema za Tanzania vilisaidia kumfanya asing’ae! 

Wimbo wa Majanga imempandisha sana chati, kwani licha ya maneno yake yaliyopangiliwa vizuri, pia midundo yake imeongeza thamani ya kibao hicho.

Lakini kama kuna kivutio zaidi katika maonyesho ya Snura, hasa katika wimbo wake huu, basi ni yeye mwenyewe. Ni kivutio kwa sababu anacheza wimbo wake kwa namna ambayo, ni mchanganyiko wa mshangao na hamasa za kingono. 

Licha ya kucheza kwa umahiri mkubwa huku akikitumia zaidi kiuno chake, hali huwa tete pale anapoyatingisha na kuyatetemesha makalio yake huku akiwa amewapa mgongo mashabiki wake ambao hulipuka kwa shangwe.

Uvaaji na uchezaji wake hauvutii machoni mwa watu wenye kuzingatia maadili ya Kitanzania, kwa maana ya tabia njema. Ni kweli anashangiliwa sana, lakini natia shaka kidogo kama kinachoshangiliwa ni muziki wake au ni namna anavyocheza. 

Akili yangu inaamini anashangiliwa kwa namna anavyocheza. Na kama hivi ndivyo, basi si jambo la kujivunia hata kidogo. Uchezaji wa msanii huyu, haustahili mbele ya watoto wetu wanaoupenda muziki wake na wala haupendezi machoni mwa wanaharakati wa maadili. 

Binafsi ninaamini Snura ameshauwezea aina ya muziki wake huu, ndiyo maana ameanza kupata washindani kama Shilole, ambaye naye kwa bahati mbaya, anaamini katika kukata mauno, uvaaji usiofaa na ufundi wa kuchezea viungo vyake!

Uchezaji na uvaaji wake unaonekana pia nchi nzima kupitia video yake. Ni wazazi wachache wanaoweza kufurahia kuutazama wakiwa na watoto wao. 

Kuna wakati nilipata kumsikia akitangaza kusaka mtu wa kumuoa. Kwa uchezaji ule jukwaani, sidhani kama anaweza kumpata mume anayemhitaji, isipokuwa watu wengi wenye tamaa ya ngono wanaweza kujitokeza. Hakuna mume makini anayeweza kukubali mkewe acheze na kuvaa namna ile. 

Labda kwa faida yake binafsi nimshauri kujitazama upya kwa sababu kubadilika ni sehemu ya maisha. Kama anafikiri uvaaji na uchezaji ule ndiyo unampatia mashabiki, mimi nakataa kwa sababu najua muziki wake umekubalika, anaweza kuvaa na kucheza kawaida na bado akaendelea kuwa juu.
Ni vyema wasanii wetu wakatambua kwamba ustaa wao unawafanya wawe mfano. Huenda zile shangwe zinazotoka kwa mashabiki siyo za kumsifu kwa uhodari wake, bali ni kumzomea kwa jinsi anavyojidhalilisha. 

Na pengine ni wakati muafaka pia kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuanza kutembelea kumbi na matamasha ili kuwabaini na kujua namna gani wanaweza kushughulika na watu wa aina hii. Hatuwezi kujenga taifa lenye maadili kama kila mtu ataachiwa kufanya anachotaka kwa sababu tu ya ustaa wao. 

Kama wameweza kupiga kelele hadi sasa waigizaji wa filamu wameanza kuvaa nguo zinazokubalika, hata huku kwenye muziki wa kizazi kipya inawezekana. BASATA inao uwezo wa kuzipiga marufuku video na nyimbo zisizoendana na utamaduni wetu

TAZAMA PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA YOUNG KILLER

20131223_151843

20131223_144529

Mwanzoni mwa wiki hii zao la Serengeti Fiesta Super Nyota 2012 Young Killer alikua  akishoot video ya nyimbo

20131223_151757
yake iitwayo Mrs.Super Star,audio ya nyimbo hii imefanywa na Mona Gangstar toka Classic Sound na video inafanywa na Adam Juma toka Next Level.
Hizi ni baadhi ya picha za utengenezwaji wa video hiyo ndani yake  walioshirikishwa ni pamoja na mdogo wake Belle 9 anaitwa Bright na Nemo.
20131223_152234

20131223_154547

20131223_144845

20131223_144549

20131223_144529

20131223_150313

20131223_151813

20131223_151843

20131223_151915

CHEKI VAZI HILI MUIGIZAJI HUYU KUTOKA BONGO MOVIE ALILOTNGA LEO..! DU! KAMA MTALII?

Yuster Nyakachara
Muigizaji huyu ana vituko?! Yani anatoka kwa staili anayotaka...!

Tuesday, 24 December 2013

MAITI YA DENTI WA CHUO CHA BIASHARA CBE YAZUA KASHESHE

KWELI dunia ina mambo! Kijana Abel Dafe 21, (pichani) mkazi wa Kayenze, Mwaloni jijini Mwanza amezua sintofahamu ya aina yake baada ya kudaiwa kufariki dunia na maiti yake kuzikwa wiki chache zilizopita na baadaye kuonekana akiwa hai, bali denti wa Chuo cha Biashara (CBE) Tawi la Mwanza ndiye akidaiwa kufa.

Desemba 2, mwaka huu, Abel alidaiwa kufa maji akiogelea katika Ziwa Victoria na mwili wake kuthibitishwa na mjomba’ake, mwili ukapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kabla ya kusafirishwa Sengerema kwa maziko Desemba 4.

Akizungumza na waandishi wetu juzi, mtu wa karibu wa Abel aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel alisema baada ya kumaliza mazishi, familia ilirudi Kayenze, Lakini yeye Desemba 17  mwaka huu ghafla alionana na Abel akiwa mzima wa afya maeneo ya Mwaloni.

Alisema alimuweka chini ya ulinzi na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kayenze na kutoa taarifa kwa ndugu waliokuwa Sengerema ambao walifika na kujionea marehemu akiwa hai!
Kituoni hapo, Abel alikataa katakata kuwa yeye hakufa alikuwa kwenye misele yake ila alipoteza simu ndiyo maana hakuwa na mawasiliano na nduguze.

Ndugu hawakuyaamini mwaelezo hayo, wakati mwingine walitaka asiwakaribie maana ni mzimu, lakini wakiwa katika maswali mengi juu ya Abel yupi aliyezikwa, walipata taarifa kituoni hapo kuwa maiti waliyemzika Sengerema anaitwa Manyama Chimwejo na nduguze  wamepatikana.

Polisi wakaitaka familia hiyo ya Abel kukaa na familia ya Manyama kujadili hatima, kama watafukua maiti hiyo na kwenda kumzika upya Kigoma au watamwacha hukohuko Sengerema alipozikwa awali.

Akizungumza kwa simanzi, Abel (aliyedhaniwa kufa) alisema ndugu zake wanachojua waliyemzika ndiye Abel bali amefufuka.

Ndugu zangu hawaamini kama mimi ni mzima hivyo napata tabu sana kwa kuwa kila mtu ananipigia simu kuniuliza. Mimi sikufa, nilikuwa nyumbani kwangu, tatizo lilikuwa ni mawasiliano, nilipoteza simu,” alisema Abel.

Kwa upande wa pili, kaka wa marehemu aliyejitokeza kudai maiti ya mdogo wake aliyezikwa kimakosa aliyejitambulisha kwa jina la Christopher Chimwejo alimtaja Manyama Chimwejo (20) kuwa kweli alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Tawi la Mwanza mwaka wa kwanza na alifika kuishi naye mapema mwezi huu baada ya chuo kufungwa.

Alisema Manyama alitoweka nyumbani kwake ghafla maeneo ya Mwaloni na baada ya hapo hakumuona tena jambo lililomfanya atoe taarifa polisi.

Hata hivyo, sakata hilo lilimalizika Desemba 21, mwaka huu katika Kituo cha Polisi Kirumba D ambapo pande zote mbili zilikutana na kukubaliana kuacha kaburi la marehemu Manyama liendelee kuwa Sengerema licha ya kwamba familia hiyo haiamini kama mwanafunzi huyo alifariki dunia.

Hapa kuna kitu, sisi hatujafiwa na ndugu yetu, tumechezewa. Kama ndugu yenu aliyekufa amerudi hata ndugu yetu pia atarudi tu, ngojeni kwanza tukatambike kwetu Kigoma,” alisema kaka huyo wa marehemu

SAMAHANI KWA PICHA ZA KUTISHA...MCHAWI APIGWA HADI KUFA MBEZI NI BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”.
“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”.
 
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

 Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

 “Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo. Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema. 
 
“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali.

Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

 Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa