Friday, 19 December 2014
SKENDO: HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYEPOTEZA NYETI ZAKE MARA BAADA YA KUFAMANIWA AKILA URODA NA MUME WA MTU HUKO BUKOBA...!!
Thursday, 4 December 2014
Wednesday, 3 December 2014
MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HEKOPTA DAR ES SALAAM
Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.
Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake.
Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya
kupata hitlafu katika injili yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba, Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.SOURCE: Father Kidevu Blog
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.
Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
Heshima zikiendelea...
Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.
HABARI PICHAZ: MBUNGE ZITTO KABWE AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE!
Mh. Zitto Kabwe anayemfuatia ndiye mchumba ake huyo aitwaye Anna!
MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni.Utambulishio huo wa mchumba wa Zitto ulifanywa na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) wakati wa sherehe ya Harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex.
“Huyu wa kwanza anaitwa Anna anafanya kazi Ubalozi wa Ireland ni mchumba mtarajiwa wa Zitto Zuberi Kabwe, anayefuata kutoka kushoto kwa Anna wote mnamfahamu ndiyo Zitto mwenyewe na anayemfuata ni Mwalimu wangu wa chuo kikuu Kitila Mkumbo na mwisho ni mbunge mwenzangu David Silinde hao ndo walio nisindikiza,” alisema Kafulila.
Wednesday, 26 November 2014
WACHINA NOMA SANA: WATOA COPY YA RANGE ROVER KISHA KULIUZA KWA POUND 14,000 WAKATI ORIGINAL LA UINGEREZA LINAUZWA POUND 40,000 , TAZAMA SAKATA HILO HAPA PIA ORIGINAL NA COPY YAKE!
Na This Day Magazine
Hili Range Rover Evoque ambalo linauzwa Pound 40,000
Ukisikia Wachina balaa sasa hii ni moja wapo, Kiwanda Kimojawapo cha China kijulikanacho kwa jina la LandWind kimeibuka na Kutengeneza Range Rover Off-Roader X7 na kuliuza kwa bei Chee kabisa Pound 14,000 ambalo Linafanana kila kitu na Range Rover Jipya kutoka Uingeleza Linalokwenda kwa Jina la Range Rover Off-Roader ambalo wao waingeleza wanaliuza kwa Pound 40,000 ambapo tofauti yake ni Kubwa sana.
Swala hilo ambalo ni kinyume cha sheria litapelekea Kiwanda hicho kufunguliwa mashitaka kwa kosa hilo la kuiba ujuzi.
Kwa Mara ya kwanza wakati limeingia Dukani wapenzi wengi wa Magari walijua kabisa kuwa lile lilikuwa ni Range Rover evoque kutoka uingeleza ambalo ndilo 'Latest Model' kwa kuwa lilifanana kila kitu , lakini ukweli ni Kwamba Lilikuwa sio bali ni Copy yake tuu ambayo wachina walichakachua
Sasa Hili ni Lile la kichina ambalo limezinduliwa wiki iliyopita na Kampuni ya Landwind huko Guangzhou Ni Range Rover X7 na Bei yake ni poa kabisa Pound 14,000 tuu
Je Mdau unaona kuna tofauti yoyote kati ya Magari hayo?
SAKATA LA MFANYABIASHARA MAARUFU DAR KUHUSU DAWA ZA KULEVYA LACHUKUA SURA MPYA!
Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji(mwenye suti), akiwa chini ya ulinzi.
Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo.
HALI tete, siku chache baada ya
mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.
mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake zimeanza kuchunguzwa.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo
TAARIFA YA KUSIKITISHA!!! WATU SITA WAPIGWA RISASI NA RAIA WA KIGENI ZANZIBAR
Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao katika matukio tofauti Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi Salum Msangi amewataja watuhumiwa hao ambao watafukishwa mahakamani kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria ni Artur Miarka ambaye alikutwa na bunduki na risasi aina ya Shotgun.
Aidha Kamishna Msangi ametoa wiki moja kwa wageni wakiwemo wawekezaji na wazalendo ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya jeshi hilo kuanza oparesheni maalum ya kuzisaka silaha kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu kuwa na silaha Zanzibar.
Hili ni tukio la Nne katika kipindi kifupi kwa jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu wenye silaha na wengine kukutwa na mabomu kisiwani Zanzibar hali inayowafanya wananchi wengi wahoji hali ya usalama na vipi silaha hizo zinapita bila ya kugundulika
Aidha Kamishna Msangi ametoa wiki moja kwa wageni wakiwemo wawekezaji na wazalendo ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya jeshi hilo kuanza oparesheni maalum ya kuzisaka silaha kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu kuwa na silaha Zanzibar.
Hili ni tukio la Nne katika kipindi kifupi kwa jeshi la polisi kufanikiwa kuwakamata watu wenye silaha na wengine kukutwa na mabomu kisiwani Zanzibar hali inayowafanya wananchi wengi wahoji hali ya usalama na vipi silaha hizo zinapita bila ya kugundulika
Tuesday, 25 November 2014
MASKINI MSICHANA HUYU AFANYIWA KITU MBAYA KATIKA UCHOCHORO HADI KUPOTEZA FAHAMU
Huyu ni msichana ambaye alikutwa katika uchocholo wa club za bar usiku kati ya galax majira ya asubuhi saa 12 akiwa hajitabuhi
Baadhi ya wanachi wakijaribu kumuongalia bint huyo akiwa ana fahamu huku akiwa katika kichocholo huku nguo zake zikiwa zimechanwa na watu wasifamika mjini kahama.
Askari polisi wa kituo cha polis kahama thomas munyongo akijaribu kumtabua msichana huyo na bila mafanikio na kuomba msanda katika kituo cha polisi .
Baadhi ya watu wakijaribu kumtambua msichana huyo .
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Baadhi ya wanachi wakimchukuwa binti huyo kwenda kwenye gari ya polisi na kupelekwa hospital ya wilaya ya kahama .
Hakiwa katika gari la polisi huku akiwa hana fahamu
Msichana akiwa hospital ya wilaya kahama daktali akijaribu kumkangua kama yuko hai .
Hivi ndivyo msichana alipochukuliwa kupelekwa hospital ya wilaya kahama kwa uchunguzi zaidi
Baadhi ya askari polisi wamtoa msichana ndani ya gari ya polisi baada ya kumfikisha hospital ya wilaya kahama
.
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya alipinga marufuku biashara ya ngono katika wilaya yake. kutokana wasichana wengi kufanya biashara hiyo haramu .
Aidha wilaya kahama imekuwa ni sehemu kubwa kwa wasichana kuingia katika biashara ya ukahaba jambo ambalo linafanya wasichana wengi kubakwa na kutupwa katika mitalo ya maji au manyumba yasio kwisha
MTOTO ALIYEPEWA KIPIGO CHA KUFA MTU KUTOKA KWA HOUSE GIRL HUKO UGANDA, AFYA YAKE INAENDELEA VIZURI.
AISEE HII HATARI SANA ...UNAAMBIWA HUYU MTOTO ATUMIWA KUMWIBA MTOTO MWENZAKE, AKAMATWA... MTAA WAFUNGWA KWA TIMBWILI LA MTOT
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi.
Kamanda akimbana mtoto huyo kwa maswali. “Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi. “Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha Polisi.Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments: