Vilabu shiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Septemba 2 ni siku ambayo mdhamini mkuu wa Ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 16, zitakazo shiriki Ligi Kuu msimu huu. Kupitia kwa meneja masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twissa wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya jumla ya Tsh 4,900,000 kwa kila timu, mbele ya Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura.
“Vodacom leo tuna furaha kubwa kukabidhi vifaa kwa ajili ya Ligi Kuu Vodacom ambayo itaanza Septemba 12 mwaka huu, tumesaini mkataba wa miaka mitatu ambao huu ndio wa kwanza, tumefurahi timu kuongezeka zimekuwa 16, hivyo kutakuwa na jumla ya mechi 240, tumetoa jezi soksi, shin guard, mipira”>>> Kelvin Twissa