SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco, katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa ameibua tuhuma nzito dhidi ya Waziri Sitta na kumwita ni msaliti .
Amesema waziri Sitta alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM kama alivyoahidi wakati alipokutana na viongozi wa Chadema may 2010.
Amesema katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Dr Slaa anasema ameamua kutoa siri hiyo baada ya Sitta kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akisema kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Amekaririwa akisema “wenzake wametapatapa yeye sasa ameingia na amejiingiza kichwakichwa mahali asipopajua kwamba hatoki kwenye matope aliyoingia, kama Mbowe ni mchezesha disco Samwel Sitta anataka kuliambia nini taifa hili kwamba wacheza Disco ni wadhambi? ni wahalifu katika nchi hii? wacheza disco katika nchi hii ni wapiga kura, ni vijana.. nenda pale Bilicanas! kwa bahati mbaya kuna wazee ambao bado wanabehave kama vijana, kuna mawaziri wanakesha pale Bilicanas, Sitta haelewi na hana uzoefu”
Kwenye line nyingine Dkt Slaa amesema wakati Sitta akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka CCM ambao angehamia nao Chadema kabla ya bunge kuvunjwa lakini pamoja na kwamba Chadema iliahidi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.
Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza Chadema akidai hatojiunga na chama hicho mpaka atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.
Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu huku akikaririwa akitiririka zaidi kwa kusema “Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka,”
Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi na alizizima, ambapo kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi kunadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimboni kwake Urambo.
Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani Iringa wakisubiri kuanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko waliyoipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchini huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi. (stori imeandikwa na mwandishi Francis Godwin wa Iringa, support kazi yake pia kupitia francisgodwin.blogspot.com)
Unaweza kumsikiliza Dr Slaa hapo chini…..
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg