YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 28 July 2013

BONGO FLAVA NOMA:WAKENYA WAJA TANZANIA KUTAFUTA VIPAJI VYA KUIMBA KUVIPELEKA KWAO



Mmoja wa wasanii akifanya vitu vyake.
STUDIO ya Candy n’ Candy Records kutoka nchini Kenya, ilifanya ‘audition’ ya kusaka vipaji vya muziki kwa wasanii chipukizi Bongo wapatao 10.
Audition hiyo ilifanyika jana asubuhi katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar, ambapo wasanii wengi walijitokeza kuwania nafasi hizo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa studio hiyo, Bwana Joe Kairuki, alisema kuwa tayari walishaingia mkataba na wasanii wa Kibongo kama Top C na Mr. Nice na sasa wanatafuta wasanii wengine 10 ambao watafanya kazi na studio hiyo iliyopo nchini Kenya.
Baadhi ya wasanii waliofika kushiriki zoezi hilo la kusaka vipaji.
Timu ya majaji ikiwa kazini (kulia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, Joe Kairuki).
Top C (kulia) akiteta jambo na mwandishi

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg