Elizabeth Michael ,'Lulu'akilia kwa majonzi juu ya kaburi la Kanumba.
R.I.P Kanumba! Ikiwa imepita miaka miwili au siku 730 tangu aliyekuwa mwigizaji nambari wani Bongo, Steven Kanumba ‘The Great’ afariki dunia, aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiongoza kwa kumwaga machozi.Katika kumbukumbu ya marehemu Kanumba Aprili 7, mwaka huu, wadau na wasanii mbalimbali walikusanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar, alikozikwa staa huyo ambaye nyota yake iling’ara kimataifa.
SHUKRANI
Awali, kabla ya kwenda makaburini, mama Kanumba, Flora Mtegoa na baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali walihudhuria kwenye ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Temboni, Dar.
Lulu akikumbatiana na Mama Kanumba (katikati) wote wakiwa na majonzi.
Akihubiri katika ibada hiyo, mchungaji wa kanisa hilo, Ambikisye Lusekelo alimpongeza mama Kanumba kwa kukumbuka kumshukuru Mungu kwa kifo cha mwanaye, tofauti na watu wengine wanaofiwa na wapendwa wao kubaki wakilia tu majumbani au mitaani.Alisema wengine husahau kwamba maneno matakatifu yanasema washukuru kwa kila jambo na kufa ni lazima kwa kila binadamu kikubwa ni kila mmoja kujiweka tayari kwa kuwa karibu na Mungu.
Katika ibada hiyo, mastaa waliohudhuria walikuwa ni wachache akiwemo Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na Kajala Masanja.
MAMA KANUMBA KANISANI
Mama Kanumba alipopewa nafasi ya kuzungumza juu ya kifo cha mwanaye alisema:
“Namshukuru Mungu kwa kila jambo, siwezi kupingana na kazi yake kwa kumtwaa mwanangu mpendwa Kanumba. Nilikupenda sana mwanangu, inanipasa nitulie tu kwa sasa, maana hata kama nikilia sana naona kama najisumbua tu mwanangu. Zaidi ya yote, naona Mungu amevuna shambani mwake.”
Hotuba ya mama Kanumba iliibua simanzi nzito kwa watu waliokuwa katika ibada hiyo.
LULU AONGOZA MACHOZI MAKABURINI
Baada ya kufika makaburini, Lulu alionekana kuwa mwenye huzuni na alipofika tu alimkimbilia mama Kanumba na kumbusu huku wote wakilia kwa uchungu, baada ya hapo ndipo utaratibu wa kuingia sehemu lilipo kaburi la marehemu Kanumba ukafanyika.
Lulu alipofika kwenye kaburi, alipiga magoti huku akilia na kuanza kusali na baada ya hapo aliweka shada la maua na kuwasha mishumaa yote tofauti na ilivyokuwa mwaka jana ilipowashwa na wasanii tofauti.
Mwanadada huyo aliendelea kulia huku akiwa ameinamia juu ya kaburi hilo hadi watu wengine walipomaliza kuomba ndipo alipoenda kunyanyuliwa na msanii mwanzake, Flora Mvungi kisha akapelekwa pembeni.
MAMA KANUMBA, MAMA LULU HOI
Ni kweli uchungu wa mwana aujuae ni mama, Mama Kanumba alionekana akiwa hoi kwa kilio huku mama Lulu, Lucresia Karugila naye akionekana kusikitika kwa tukio hilo la kumbukumbu ya Kanumba.
WEMA AMKACHA KAJALA
Katika tukio hilo, Kajala alishiriki kwenye ibada kisha makaburini ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema kwamba Wema Isaac Sepetu amemkacha Kajala kwa kuhofia kupigana kwani kuna habari kwamba Kajala na timu yake walikuwa wamejipanga kwa lolote litakalotokea kwenye shughuli ndiyo maana Wema akaamua kukacha.
RAY, PATCHO MWAMBA, MWAKIFWAMBA WAINGIA MITINI
Inafahamika kuwa Vincent Kigosi ‘Ray’ alikuwa swahiba mkubwa wa marehemu Kanumba lakini hakuonekana kanisani wala makaburini jambo lililosababisha minong’ono kwa wadau.
Urafiki uliokuwepo kati yake na Patchou Mwamba ni mkubwa, kwanza alikuwa mbunifu wake wa mavazi lakini pia ndiye
Baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi katika picha ya pamoja na Mama Kanumba (wa pili kulia) na mama Lulu (kulia ).
aliyemwingizia kwenye tasnia ya filamu lakini hakuonekana kwenye tukio hilo muhimu.Bosi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba kama kiongozi anayehusika na wasanii wote wa filamu Tanzania, hakuonekana kanisani wala makaburini, achilia mbali listi nyingine ndefu ya mastaa wa filamu waliokuwa na uswahiba na marehemu Kanumba.
Kukosekana kwa watu kilishtua na kuwashangaza wengi kwani siyo jambo la kawaida na kubaki wakinong’ona wakisema wasanii hao hawajui kama siku moja nao watakufa.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ akizungumza makaburini hapo alimtaka mama Kanumba kuelewa kwamba watu waliohudhuria mahali hapo ndiyo ndugu zake kwani anayekujali wakati wa shida ndiye rafiki wa kweli.
Mchungaji Ambikisye Lusekelo akiongoza ibada ya shukrani iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Temboni, Dar.
Wasanii waliohudhuria kwenye kumbukumbu hiyo ni Mussa Issa ‘Cloud’, mzee Chilo, Salma Jabu ‘Nisha’ Salama Salmini ‘Sandra’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Dr. Cheni, Wastara Juma, Jacqueline Wolper, Flora Mvungi na Leah Richard ‘Lamata.’Mbali na kuhudhuria, mastaa wengi walitundika picha za marehemu Kanumba kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuweka maneno ya kumwombea staa huyo.
Kwa upande wake Lulu aliweka picha ya marehemu Kanumba akiwa anacheka kisha akaandika ujumbe wake, sehemu ya ujumbe huo ilisomeka:”…alikuwa zaidi ya mpenzi, mume, nitakukumbuka daima.”
Naye mwigizaji ambaye aliingia kwenye uigizaji kwa ushawishi wa marehemu Kanumba, Batuli aliandika: “Nimemisi tabasamu lako, kicheko chako, sauti yako…”
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg