CECAFA yajibu kwa kuifuta Dar es salaam Young Africans
posted 4 hours ago by admin
Mabingwa wa soka Tanzania bara Azam FC, watashiriki michuano ya kombe la Kagame mwaka huu, wakichukua nafasi ya Dar es salaam Young Africans ambayo imetimuliwa na CECAFA kufuatia azimio la kupeleka timu ya vijana lililotangazwa na kocha mkuu wa klabu hiyo mbrazil Marcio Maximo mwishoni mwa juma lililopita.
Katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA Nicolas Musonye, amesema wamefikia maamuzi ya kuiengua timu ya yanga kwenye michuano hiyo kutokana na maamuzi yao ya kutaka kupeleka kikosi cha vijana kuchukuliwa kama dharau.
Kufuatia maamuzi hayo Azam FC wanaingia katika kundi la kwanza la michuano hiyo ambalo lina timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Ratiba ya michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame inaonyesha Azam FC watacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport katika uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka huu.
Mchezo mwingine kwa siku hiyo utachezwa saa nane mchana kati ya mabingwa wa visiwani Zanzibar KMKM dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini.
Mchezo wa pili Azam FC watacheza mnamo Agosti 10 dhidi ya KMKM, kabla ya kuivaa Atlabara Agosti 12, halafu itamaliza makundi dhidi ya Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano hayo ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawad
|
Tuesday, 5 August 2014
KILICHOWAKUTA YANGA HIKI HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg