Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa, kushoto akimtoka beki wa Azam FC, Erasto Nyoni katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanya imeshinda 3-0.
Tuesday, 16 September 2014
AZAM FC YAKUBALI KICHAPO CHA GOLI 3 KWA 0 DHIDI YA YANGA
NSSF YADHAMINI MPAMBANO W SIMBA FC NA NDANDA FC
Baadhi ya mashabiki wakishudia mchezo huo.
Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa Mtwara, Bw. Daniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shirika la NSSF kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao ya NSSF yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo, mafao ya kuumia kazini na pension ya uzeeni
.
Kikosi cha Ndanda FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara
Kikosi cha Simba FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia mpango wake wa wakulima Scheme imedhamini mechi kati ya Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Timu ya Ndanda FC ya Mtwara. Akizungumzia mchezo huo uliofanyika jana mkoani Mtwara, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema mpango huo umelenga kuwasaidia wakulima mkoani humo.
Alisema kupitia mpango huo NSSF imejikita kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo. Aliongeza kuwa mpango huo unatoa mafao ya kuumia kazini, pamoja na pension ya uzeenipindi watakapofikisha umri wa miaka 55.
"..Hii ni kuisaidia serikali kujinasua na mzigo wa kulea wazee kwa kuwaingiza mapema kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili waanze kujiwekea kwa maisha yao ya baadae," alisema Bi. Chiume.
Mpango huo unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa nssf wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea. Akifafanua zaidi alisema wakulima mbalimbali mkoani Kigoma na wilayani Mbinga tayari wamenufaika kwa kupata mikopo zaidi ya bilioni 3.7 tangu mpango huu wa Wakulima Scheme uanzishwe.
"...Wakulima wote wanakaribishwa kutumia fursa hii kujiunga na NSSF."
Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza nlipia kwa mwaka mzima,miezi anayoweza lipa .lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.
NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne na mke au mume. Alieleza kuwa matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu kwa SHIB ya NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu. NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama zaidi ya 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani Mtwara na Lindi ambazo ni Tandahimba, Nanyumbu, Masasi, Nachingwea, Newala, Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa zao korosho.
aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu, pembejeo, zana mbali mbali za kilimo ili kujiinua kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans, Ofisi ya NSSF Mkoa wa mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion 1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasilia mali, wakulima na wafanyakazikwenye mkoa huo. Mpango huu wa Wakulima Scheme ulizinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete Mwezi Mei mwaka huu.
Bw. Dalali akitoa shukran kwa waandalizi wa ndanda day na wadhamin wa mpambano ambao ni NSSF kwa kuwezesha timu hizo kupambana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu hizo.Kwa mara ya mwisho timu ya Mtwara kucheza mpira ilikuwa ni miaka kumi iliyopita
DUNIA IMEKWISHA: MWANAMKE AWABAKA WATOTO WA KIUME WAWILI , AWALAZIMISHA WAMUINGILIE KIMWILI USIKU WA MANANE!
Vitendo vya ngono nchini Uganda vimesababisha maambukizi makubwa ya Ukimwi. Mwanamke wa miaka 37, aliyefahamika kwa jina moja la Adong anashikiliwa na Polisi huko mjini Gulu nchini Uganda kwa kosa la kuwaingilia watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 14 na 15 ambao vilevile ni wenye undugu na yeye!
Aliwaingilia watoto hao alipokwenda kuwatembelea wazazi wao na ndipo usiku akanyata na kuingia chumbani mwao na kuwashawishi bila aibu wamle uroda! Ilitokea baba yao aliwasikia wanae wakijadili juu ya "utamu" na ndipo akaiarifu polis nao hawakuzubaa na kumtia ndani. Akitiwa hatiani anaweza kufungwa miaka 7 au maisha! Mambo hayo! Taarifa zaidi tutawaletea tukizipata...!
TABORA WAPOKE ASKARI 75
.jpg)
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya Polisi. Kamanda aliwataka askari hao kufanya kazi kwa weledi katika utendaji kazi pamoja na Nidhamu ya hali ya juu.
.jpg)
Askari wapya wakimsikiliza Afande Suzan Kaganda alipowapokea mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi
.jpg)
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi. Picha na Fakih Abdul - mwandisi wa Polisi Tabora.
Ndugu waandishi wa habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-
KUPATIKANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA NA
PIKIPIKI ZA WIZI: Huko wilaya ya Igunga wamekamatwa watuhumiwa watatu:-
1. WILLY s/o MASHILINGI, 22 yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Kahama.
2. SITA
s/o JILUNGA, 38 yrs, msukuma, mkulima na mkazi wa Nzega.
3. YUSUPH
s/o MIHAYO, 24yrs, msukuma, mkulima wa mtaa wa Stoo.
4. GILALA
s/o BULEBA, 35yrs, msukuma, mkulima, mkazi wa Igunga mjini.
wakiwa na madawa ya
kulevya wanayoyatumiwa kulewesha watu kisha kuwapora pikipiki. Walipohojiwa
walikiri kuhusika na matukio mbali mbali ya wizi wa pikipiki na kuonesha
pikipiki mbili zenye namba T 892 CXB, T 522 CQZ, T.914 BUW na T.812 CGU
zote aina ya SANLG ambazo walizipora huko Puge wilaya
ya Nzega. Juhudi za kuwatafuta wamiliki halari wa pikipiki hizo zinaendelea.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA
BHANGI GUNIA MBILI:
Huko wilaya ya Nzega amekamatwa mtuhumiwa MABULA s/o
EZEKIEL, 23yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Ibologero akiwa na bhangi gunia
mbili. Mtuhumiwa baada ya mahojiano amekiri kuwa ni muuzaji na mtumiaji wa
bhangi.upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
AJALI YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU
NA KUSABABISHA VIFO:
Huko kijiji cha Ndono barabara ya Urambo
gari no. T607 BNV scania lorry iliyokuwa ikiendeshwa na FUMBA s/o JUMA, 45yrs,
Msambaa, mkazi wa DSM iligongana na pikipiki ya kubeba mizigo (Guta) REG no.
T153 CWJ SUNLG na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo ambao ni MAHONA
S/O MUSA WANDEZI, 30yrs, Msukuma, mkazi wa Intika dereva wa pikipiki, HIBHA S/O
LUCAS, 30yrs, msukuma, mkazi wa Ndono, MABULA S/O MATONGO, 35yrs, msukuma,
mkazi wa Intika chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki.
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA
KIFO:
Huko maeneo ya barabara kuu Nzega – Igunga katika kijiji cha Kitangili GARI
T.300 CWB Toyota Hiace ikiendeshwa na STANSLAUS S/O JOAKIM, 33yrs, Mchaga,
mkazi wa Nzega ilimgonga mtembea kwa miguu JOKU D/O MBEGESHEN, 32yrs, Msukuma, M/biashara,
mkazi wa Singida na kufa papo hapo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mtembea kwa
miguu kuvuka barabara bila tahadhali. Dereva amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza
vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia watumiaji wa barabara wafuate sheria za usalama barabarani.
SUZAN S. KAGANDA –ACP.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA TABORA.
Wednesday, 10 September 2014
RAIS KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa abiria atayekutwa na ugonjwa wa ebola mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid jinsi Tanzania ilivyojipanga kupambana na ugonjwa hatari wa ebola baada ya kukagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo ya namna ya kuhudumia abiria wakati wa ukaguzi wa wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madakrai na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jueb4: lius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma
NEWS ALERT: MOTO WATEKETEZA BWENI SHULE YA AFRICAN MUSLIM MJINI MOSHI HIVI SASA

Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya African Muslim iliyopo Laloleni manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto hivi sasa. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umeanza majira ya saa 2 za usiku huku chanzo chake bado hakijajulikana na ripota wetu Dixon Busagaga aliye eneo la tukio anafuatilia ajali hii na atatujulisha kila kitachojiri na kupatikana.
.jpg)
Kikosi cha zimamoto kimefanya jitihada za kuzima moto huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya maji.
JIJI LIMEINGILIWA SASA,UNAAMBIWA HUYU NDIYE MWANAFUNZI WA KIKE WA DARASA LA TANO TISHIO KWA UTAPELI JIJINI DAR
Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene (11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma.
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana nauli.Ilisemekana kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Dereva mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta.
“Mara kadhaa amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Jader Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye.
Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni.
Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Pia alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene.
Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia.
Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwa huku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia.
LORI LAPATA AJALI MBAYA MLIMA SEKENKE MKOANI SINGIDA

Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.
DEREVA wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.

Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.

Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni.

Malori mengine ya mizigo yakipita karibu na eneo la tukio.
Subscribe to:
Posts (Atom)











