YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday, 10 March 2014

PICHA:MFAHAMU PASTA ANAYEHUBIRI KANISANI AKIWA NA NYOKA SHINGONI.


Pasta anayejulikana kuhubiri akiwa amemweka nyoka shingoni ameaga dunia. Pasta Jamie Coots anayeamini kuwa kinga hutoka kwa mungu aliweza kupoteza maisha yake baada nyoka huyo wa sumu kumuuma akiwa akihubiria mbele ya maumini.
Ilikuwaje hadi pasta huyo kuhubiri na nyoka mgongoni?

Kupitia andiko la Marko 16:15-18, pasta huyo anaamini kuwa Yesu aliweza kuwaambia wakristo wote kuwa wanaweza kushika nyoka na hatawaumiza wala kuwadhuru bora tu uwe umebarikiwa na mungu mwenyewe.

Pasta huyo wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name aliumwa na nyoka huyo mbele ya kanisa lake na ilimbidi kukimbizwa hadi nyumbani kwake bila kupelekwa hospitalini.

Wauguzi walipowasili nyumbani kwake waliweza kufukuzwa huku pasta huyo akiwa na imani kuwa mungu atamtibu ugonjwa wake, jambo ambalo halikufanyika. 

ABANIKWA KAMA NYAMA CHOMA NI BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA


Ezekiel Kaganga

Ezekiel Kaganga (29) mkazi wa Mjimwema Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga baada ya kubanikwa kwenye moto kama kuku akituhumiwa kuiba pikipiki (bodaboda).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amewataja watu wawili wakihusishwa na tukio hilo la kinyama.
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni ni Alex Ludago (28) na Steven Michael (29) wote wakazi wa MET mjini Mafinga.
Akisimulia jinsi tukio lilivyokuwa katika wodi namba tano ambako amelazwa Kaganga alisema anafahamiana na watuhumiwa hao na kabla ya tukio hilo Januari 7, mwaka huu walikuwa pamoja wakinywa bia katika moja ya maduka ya kuuzia pombe mjini Mafinga.
Alisema Januari 8 mwaka huu alipokea taarifa katika duka hilo la pombe lililopo katika eneo la mashine ya mpunga kwamba kuna pikipiki ilipotea katika mazingira ya kutatanisha baada ya yeye kuondoka katika eneo hilo siku iliyopita.
Katika majibu yake kwa mmoja wa watuhumiwa hao alisema hajui lolote kuhusu kupotea kwa pikipiki hiyo.
Anavyoonekana majereha ya mgongoni
 “Jamaa hao hawakuridhishwa na majibu yangu na Ijumaa ya  Januari 12 alikamatwa na Polisi akihusishwa na tukio hilo na akatoka Januari 17,” alisema.
Alisema baada ya kutoka Polisi alikaa siku tatu uraiani na ndipo alipokamatwa na vijana hao na kupelekwa katika msitu wa Lumwago nje kidogo ya mji wa Mafinga.
Katika msitu huo alifungwa kamba, kupigwa viboko na baadaye alining’inizwa juu ya mti huku moto ukiwa umechomwa chini yake.
Sehemu ya miguu yake
“Nilibanikwa kama kuku, moto ukiwa chini mie nikiwa nimefungwa juu ya miti; niliachwa hapo kwa siku mbili,” alisema.
Alisema baada ya siku mbili alihamishwa kutoka katika msitu huo na kupelekwa eneo la machijio mapya na kumwagiwa mafuta ya taa ili achomwe na moto na kundi la watu wanaokadiriwa kuwa saba.
“Nikiwa mahututi walinichukua na kunipeleka kituo cha Polisi kabla sijaletwa hapa hospitalini nako endelea kupata matibabu,” alisema.
Aliyata maeneo ambayo ameungua sana kuwa ni mgongoni, makalioni, mikononi, ubavuni, miguuni na shingoni.
Kaka wa Kaganga, Aizaki Kaganga alisema “mdogo wangu anaendelea kupata matibabu, na hali yake sio mbaya sana japokuwa hawezi kutembea.”
Alisema alipokea taarifa ya kupotea kwa mdogo wake  kuhusishwa na tukio hilo na akawaahidi watuhumiwa wamsubiri  arudi kutoka safarini Arusha ili alipe pikipiki hiyo.
“Hata hivyo vijana hao hawakuwa na subira hiyo na badala yake wakamfanyia unyama waliofanya,” alisema.
Kamanda Mungi alisema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na kuwasaka watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII INATISHA HEBU ANGALIA PICHA YA KIJANA ALIYECHOMWA MOTO


PICHA_3_6bed3.jpg

Sunday, 9 March 2014

SIKILIZA TAHARIFA ZA MAGAZETI YA LEO TAREHE 10/3/2014 LIVE

on_air11Kwa kutumia teknolojia ya kisasa nimekurekodia magazeti haya yakisomwa na kuchambuliwa  Redioni kwako mtu wangu wa nguvu,hivyo kama ulimis kwa bahati mbaya waweza kuyasikiliza hapa,Sikiliza kupitia 104.4 Clouds Fm Dodoma.
Bonyeza play kusikiliza.

Use

AKIWA STUDIO YA RADIO MAARUFU:SHOGA ANAEJIITA ANTI SUZY AVAMIWA NA KUPEWA KICHAPO NUSU YA KUFA


 
BAADA ya shoga maarufu jijini Dar es Salaam, Ibrahimu
Mohamed ‘Anti Suzy’ (25), kutoboa siri kwenye vyombo vya habari jinsi watoto wa kiume wanavyoharibiwa na wanaume na kueleza namna alivyobwagiwa mtoto wa mwaka amtunze, mwanamume aliyembwagia mtoto ameibuka na kumjeruhi kwa visu akitaka kumuua.

Mwanamume huyo mwenye mke, awali alikuwa akiishi na Anti Suzy kama mume na mke eneo la Jangwani, baada ya kumkimbia mkewe na alikorofishana na shoga huyo baada ya kumfanyia fujo na kumuibia.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo jana nyumbani kwake, ‘Anti Suzy’ aliyejitangaza kuwa ni muathirika wa Virusi Vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 10 sasa, alisema mwanamume huyo alikuwa akimsumbua warudiane, lakini yeye alikataa na kumtaka aishi na mkewe na kutunza watoto badala ya kumng’ang’ania.

“Nilimwambia simtaki, vituko alivyonifanyia ukiacha kuniletea mtoto wa mwaka na nusu wa kike nimlee hapa nyumbani, alikuwa akinipiga, kunitukana na aliniibia vitu vyangu vyote. Kwanza nilishamwambia nimeathirika na Ukimwi ananifuata nini?” Alihoji shoga huyo.

“Jana (juzi) alinipigia simu akinitaka turidiane nikamwambia asinifuate kwanza nimeshaenda kwenye vyombo vya habari.”

Alisema alimwambia hivyo ili asimfuate, lakini baada ya kumweleza hayo, alimvamia nyumbani juzi kati ya saa nne na tano asubuhi akiwa na panga na visu akimtishia kumuua kama hawatarudiana na kama ataendelea kwenda kwenye vyombo vya habari kumuanika mambo yake.

“Nilikimbilia ndani na yeye akanifuata humo, akarusha panga anikate shingoni huku akisema ataniua, nikakwepa, lakini likanijeruhi shingo, kama haitoshi akachukua kisu alichokuwa nacho akanikata vidole.

“Damu ikaanza kutoka nyingi, alivyoona hivyo akanikaba kooni ili aninyonge, majirani waliposikia nakoroma, wakavunja mlango na kuniokoa,” alidai Anti Suzy.

Shoga huyo aliyeanza vitendo hivyo akiwa mkoani Mwanza, alisema aliamua yeye na mama mwenye nyumba kwenda Kituo Kidogo cha Polisi Jangwani kutoa taarifa na kupewa hati yenye namba MS/RB/10695/2011.

Alisema baada ya kwenda Polisi, aliandika maelezo na kutoa vielelezo likiwemo panga na kisu alivyovitumia kumjeruhi na aliandikiwa hati ya matibabu (PF3) na kwenda Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.

Polisi katika Kituo cha Jangwani walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini walisema mlalamikaji alijitaja kwa jina la kike ambalo ni Suzana Mohamed na tayari taarifa za suala hilo zimepelekwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa hatua za juu zaidi. Mkuu wa Kituo cha Msimbazi hakuwa tayari kutoa taarifa kuhusu suala hilo.

Aidha, Muuguzi aliyekuwa zamu juzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ambaye hakupenda kutaja jina gazetini, pia alithibitisha kumhudumia mgonjwa, Suzana Mohamed (25) mkazi wa Jangwani aliyejeruhiwa shingo na vidole kwa kukatwa na visu akiwa na PF3.

Mama mwenye nyumba anakoishi ‘Anti Suzy,’ Manju Machu maarufu kama Bi Manju, alithibitisha jana kutokea kwa tafrani hiyo iliyosababisha mpangaji wake huyo akimbie kunusuru maisha yake.

“Alikuja hapa huyo mwanamume akamvamia akitaka kumuua, alikuwa na panga na kisu, tuliingilia maana alikuwa anasema lazima amuue, nikasema akimuulia hapa kwangu na mimi nitakuwa matatani, na nchi hii ina sheria, kama una kosa na mtu polisi si ipo? Sisi tulimpeleka huyu Polisi kutoa taarifa” alisema Machu.

Majirani wa Mohamed ‘Anti Suzy’ nao walithibitisha jana kushuhudia vurugu hizo na kumshauri shoga huyo kurudi kwao Mwanza ikiwa vitisho vitaendelea.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mohamed alifanya mahojiano na gazeti la Habari Leo na kueleza namna vigogo aliowataja kwa jina la mapedejee wanavyowatumia wao kwa gharama yoyote, wawatafutie watoto wadogo walioko shuleni na mitaani akiwataka wazazi, serikali na jamii kuwa macho na watoto hasa wa kiume.

Aidha, pia aliwaonya wanaume wasimfuate kwa kuwa yeye ni mwathirika wa Ukimwi na kwamba mashoga kama yeye wameathirika na ugonjwa huo. Usikose makala maalumu ya mahojiano ya ana kwa ana baina ya gazeti la Habari Leo na Mohamed “Anti Suzy” katika gazeti hilo keshokutwa Jumatano.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 10/3/2014 YA HABARI,UDAKU,MATUKIO,MICHEZO NA BURUDANI


 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.