Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA hivyo pambano hilo pamoja na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada ya wachezaji kama Alfonce Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac Chipindi katika pambano lao la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda ulingoni kwa kile walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji kumaliziwa pesa zao za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda ulingoni.
Nao mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni wakishinikiza kumaliziwa pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua taflani ukumbini hapoa huku mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika muda wa Cheka kupanda ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita muandaaji wa mapambano hayo ili kufika chumba alichokuwa Bondia mtanzania, Francis Cheka ili kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda ulingoni.
Alisikika Cheka akimuwakia muandaaji huyo kuwa, '' Nini Mmarekani hata angekuwa Mchina, nimalizie changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia lilichukua muda wa majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na wadau wa ngumi waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai mabondia, ndipo mabondia hapo wakapanda ulingoni.
Aidha katika pambano la raundi 10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la kuwania Ubingwa wa WBF wa Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa pointi 2 tu mpinzani wake Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa WBF wa Afrika.
Na katika pambano la Utito wa Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya Bondia Alfonce Mchumiatumbo na Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa kwa KO mpinzani wake katika raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha mikono juu kuashiria na wasaidizi wake kutupa taulo ulingoni kuashiria kushindwa kumalizia mchezo huo.
Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na Cheka, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
Waziri wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
Bondia Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mabondia hao wakiliana Timing.......
Cheka (kulia) na Phill wakichapana......
Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana
We subiri inakuja hiyooooo
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshuhudia mchezo huo.
Bondia Mada Maugo (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Thomas
Mashari kwa konde zito wakati wa pambano lao la raundi 10 la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBF, ambapo Mashali ameibuka mshindi kwa
Pointi dhidi ya Maugo.
Chanzo: Sufiani Mafoto Blog.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg