MAJIBU
ya vipimo vya afya vilivyofanyika juzi kwa mtoto Nasra Rashid (4),
aliyefichwa kwenye boksi mkoani Morogoro, kwa muda wa miaka minne,
yanatarajiwa kutolewa leo.Mtoto huyo awali alilazwa katika Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro ambako waliamua kumhamishia Muhimbili ambako alifanyiwa
vipimo mbalimbali kuchunguza afya yake.Wakati majibu hayo yakitarajiwa
kutolewa leo, madaktari wanaomungalia mtoto huyo wamemuanzishia lishe
maalumu ya maziwa, pamoja na dozi maalumu ya sindano ya kuzuia maumivu
kutokana na kulalamika maumivu ya kifua.Taarifa hiyo ilitolewa jana
jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Dosis Ishenda,
wakati akizungumza na Tanzania Daima.Alisema hali ya Nasra inaendelea
vizuri na kwamba vipimo vyote vya msingi vimeshachukuliwa na majibu yake
yatatolewa leo.“Hali yake inaendelea vizuri ingawa analalamika kuwa na
maumivu ya kifua, pia madakatari wamemuanzishia lishe maalumu ya maziwa
kwa ajili ya kumsaidia kupata nguvu,” alisema Ishenda.
Nasra, alifikishwa Muhimbili juzi saa saba usiku kutoka mkoani Morogoro baada ya hali yake kubadilika ghafla.Akiwa katika hospitali ya Muhimbili, alianza kupatiwa huduma za awali ikiwa ni pamoja na kupimwa uzito, damu na haja ndogo.Mei
21, mwaka huu, mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa
Kiwanja cha Ndege, Morogoro, alibainika kumficha mtoto wa marehemu mdogo
wake kwenye boksi kwa miaka minne, hali iliyowafanya wananchi
wamshambulie kwa kipigo kutokana na unyama aliomtendea.Siri
ya unyama huo iliibuliwa na majirani wa mtuhumiwa baada ya kutoa
taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo
kuhusu mtoto, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri
wa miezi tisa.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg