YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 24 August 2014

TAZAMA PICHA JINSI MARIO BALOTELI ALIVYOPOKELEWA LIVERPOOL




Mario anakubalika: Balotelli alikutana na mashabiki née ya viwanja vya Melwood baada ya mazungumzo ya uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan
KLABU ya Liverpool imemuahidi maslahi mazuri Mario Balotelli ili kuhakikisha mshambuliaji huyo mtata anapiga mzigo wa uhakika Anfield.
Baada ya Liverpool kukubali kutoa Pauni Milioni 16 za ada ya uhamisho kwa AC Milan kumnunua nyota huyo, ilifanya kikao kizito na Mino Raiola, wakala wa mchezaji huyo, Balotelli alikwenda mjini Manchester jana kufanyiwa vipimo vya afya na baadaye akakutana uso kwa uso na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kwa mara ya kwanza. 
Mamia ya mashabiki wa Liverpool yalimlaki wakati anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi, Melwood na hakuna shaka atakapata mapokezi mazuri Anfield. 
Mshambuliaji huyo wa Italia atasaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya awe analipwa Pauni zisizopungua 85,000- au 90,000 kwa wiki. Lakini ameahidiwa marupurupu zaidi iwapo atafanya vizuri kazini. 


Balotelli akiondoka Melwood jana baada ya kukamilisha mazungumzo 




Mamia ya mashabiki yalijitokeza kumshangilia Balotelli


Hapa ni wakati Balotelli anawasili Melwood kwa mazungumzo

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg