0
Sunday, 10 March 2013
ZILIZONIFIKIA HIVI BASI LA KILIMANJARO EXPERIENCE LAPATA AJALI LEO ASUBUHI
Pichani juu na chini ni baadhi ya abiria wakiwa nje ya basi lao la Kilimanjaroo Express lenye namba za usajili T860 BVA walilokuwa wamepanda wakitokea jijini Dar kuelekea jijini Arusha mapema leo asubuhi,ajali hiyo imetokea eneo la Mombo ambapo chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni dereva wa basi hilo alikuwa akimkwepa muendesha baiskeli,matokeo yake basi hilo likakosa mwelekeo na kupinduka,aidha katika jali hiyo inaelezwa kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyepoteza maisha.(Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog)

TAARIFA KAMILI KUHUSU WALIOKAMATWA KWA KUMTUMIA MSG ZA MATUSI SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA
Kutokana na ile ishu ya watu kumtukana spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda baada ya namba yake kudaiwa kutajwa hadharani na viongozi wa Chadema, watu watatu wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kuhusika.
Hao watu ni kutoka mikoa ya Dodoma, Simiyu na Kilimanjaro ambapo wanatuhumiwa kutumia lugha chafu za matusi na uchochezi dhidi ya spika.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Assah Mwambene amesema wawili walikamatwa kwa tuhuma za kumtumia spika msg za matusi, mmoja aliebaki alikamatwa na DVD yenye picha ya kuhamasisha lugha za matusi kwa spika.
Mwezi uliopita spika Anne Makinda alipokea msg zisizopungua 400 kwenye simu yake ya mkononi pamoja na kupokea simu mbalimbali za matusi baada ya namba yake kudaiwa kutajwa hadharani kwenye mkutano wa CHADEMA.
Subscribe to:
Posts (Atom)