YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday, 3 September 2018

TANZANIA KINARA KWA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa hoteli ya  Westin jijini Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Makampuni yapatayo 80 yalishiriki katika Kongamano hilo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B10.10.37%2BAM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni  wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki. 
 “Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”
 Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubiaKongamano la Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya  Winstin jijini Beijing nchini China.
 Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria  kwa dhati  kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.
 Amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania  inaongoza kwa kupokea  uwekezaji  katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.
 Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa  ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo  mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo  mkubwa katika  kujenga msingi imara wa viwanda.
 “Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza  mkakakati wetu wa kukuza  uchumi wa viwanda na biashara.”
 Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji  kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.
 Kuhusu uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017,  Waziri Mkuu amesema  umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda na utalii.
 Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesemakuna fursa nyingi kwenye sekta ya huduma hususan katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa kwa haraka nchini Tanzania. 

Pia kumekuwa na ukuaji na mageuzi ya haraka katika soko la TEHAMA nchini kwa miaka 10 iliyopita. “Soko la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano limekuwa kwa ongezeko la watumiaji, aina ya huduma zinazotolewa pamoja na kupanuka kwa eneo ambalo huduma hizo hutolewa.”
 Waziri Mkuu ameongeza kuwa, “Tanzania kuna fursa zisizo na ukomo katika eneo hili huku kukiwa na matarajio ya kukuwa kwa soko la kikanda.” 
 “Maeneo ya kuwekeza ni pamoja na utoaji wa huduma za simu hususan katika maeneo ya vijijini, utoaji na uendeshaji wa huduma za mtandao pamoja na ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mawasiliano. Tunawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo haya.”
 Amesema kwa wale ambao nia yao ni kuwekeza katika kilimo, Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na takribani hekta milioni 29.4 kwa ajili ya umwagiliaji.
  “Ninawakalibisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo cha biashara kwa mazao kama miwa, mpunga, ngano, kahawa, chai na mahindi. Tuna fursa kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari.”
WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B10.10.39%2BAM%2B%25281%2529Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania waliopo nchini China kuhudhudhuria Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018.
WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B10.09.16%2BAM%2B%25282%2529

WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B10.09.16%2BAM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China,mara baada ya kuzungumza nao leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.

WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B9.37.53%2BAM
Balozi wa Tanzani chini China, Mbelwa Kairuki akimtambulisha mmoja wa wafanyabiashara wa China kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza nao leo jijini Beijing, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili.
WhatsApp%2BImage%2B2018-09-02%2Bat%2B10.09.17%2BAM
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe akibadilishana kadi na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China.

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU UKATILI KWA RAIA NA WANAFUNZI.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelaani tukio lililofanywa na Mgambo wa Jiji la Dar es salaam akisema ni la kihuni, kishenzi na kinyama na halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani, watetezi wa haki za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Lugola alisema Serikali inalaani vikali tukio hilo ambalo lililotokea wiki iliyopita jijini humo, na kutokana na unyama huo tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa.

“Jeshi la Polisi tayari limewakamata wahusika kama Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni tarehe 31 Agosti, 2018 ilivyoeleza. Natumia fursa hii kuwakumbusha tena Mgambo wote kuwa makini katika utekelezaji wa maagizo wanayopewa na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu,” alisema Lugola.

Pia kutokana na tukio hilo, Lugola alisema anazitaka Mamlaka za Majiji, Manispaa na Halmashauri kufikiria kuanzisha Huduma ya Polisi Wasaidizi (Auxiliary Police) katika maeneo yao kwa mujibu wa Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322 ili kuepuka matukio ya uvunjifu wa haki za Binadamu kama tukio la Mgambo watatu  jinsi lilivyo tokea.

Aidha, Lugola pia alizungumzia kuhusu baadhi ya matukio mengine ambayo watu  wanajichukulia Sheria mkononi na kuwaadhibu kwa kuwapiga watu wengine kwa sababu mbalimbali.

Aliyataja matukio hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au wake kuwapiga waume zao, pia  wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali, pamoja na walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.

Pia Lugola aliwaonya baadhi ya Askari Polisi ambao wanatumia nguvu isiyo ya kadiri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.

“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalaani vikali matukio ya kujichukulia Sheria mkononi na kupitia kwenu Wanahabari nawataka Watanzania kufuata sheria za nchi kwa kuacha vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi. Vitendo hivi pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani vinaweza kuleta madhara kwa watu ambao hawana makosa na kuichonganisha Serikali na wananchi wake,” alisema Lugola.

Kutokana na matukio hayo, Lugola aliwataka wanandoa wanakumbushwa kutumia Dawati la Jinsia katika Vituo vya Polisi kote nchini ili kuwasilisha malalamiko yao ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa ili hatua stahiki zichukuliwe.

Pia aliwataka wananchi waendelee kuheshimu sheria za nchi na kuepuka kujichukulia unakuta mtu anapigwa hata haulizi anayepigwa amekosa nini nae anajiunga nao na kumpiga hali ambayo imesababisha majeraha, vilema vya kudumu na vifo kwa watu wasio na hatia.

Hata hivyo, Lugola aliwaonya walimu kwa kufanya matukio kujirudia kwa kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa na kuwapiga hovyo kiasi cha kusababisha maumivu makali, ulemavu na vifo.
 
“Natumia fursa hii kuwakumbusha Walimu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Adhabu kwa wanafunzi ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuepuka madhara yake, kuondoa hofu kwa wazazi na kufanya shule zetu kuwa mahali salama kwa watoto wetu,” alisema Lugola

"NIACHENI NIWATIE ADABU" MANENO YA FRED LOWASSA


Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa ameibukia katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Monduli na kuwataka aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Julius Kalanga na Isack Joseph maarufu Kadogoo, kukaa kimya kwani anawafahamu kuliko wanavyojifahamu.
Akizungumza kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea wa CHADEMA amesema, amelazimika kuwajibu vijana hao kutokana na kuendelea kumchafua Mzee Lowassa. “Kama kuwatia adabu hawa vijana niachieni mimi, ntawatia adabu ninawafahamu vizuri sana”
LOWASSA amesema “Kalanga si rizki ameharibu heshima yetu”

"NAMUUNGA MKONO RAISI". DIWANI KUTOKA CHADEMA


Diwani wa Kata ya Olasiti Alex Martin ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Udiwani katikaKata hiyo ikiwa imepita siku moja baada ya kujiuzulu Diwani wa kata ya Engutoto katika jimbo la Arusha mjini analoongoza Mbunge Godbless Lema CHADEMA.
Alex Martin amesema ameamua kuondoka CHADEMA sio kwamba na ugomvi na Chama ila ameamua kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

MAAJABU YA MBUZI TANZANIA


Umewahi kuwaza kumfuga mbuzi awe mlinzi wako? Kama ambavyo wengine hufuga mbwa ama wakati mwingine paka? Mzee Antony Mwandulami mkaazi wa Mkoa wa Njombe Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania anafuga mbuzi kama mlinzi wake. Anasema mbuzi huyo ambaye amefanya kazi kwake kwa miaka 19 sasa humpa taarifa juu ya kila mtu mbaya anayetaka kuja kwake na kumdhuru na ameweza kumnusuru dhidi ya majanga mbalimbali.

Thursday, 30 August 2018

KATIBU MKUU WA CCM DR. BASHIRU AUNGURUMA


August 30, 2018 Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ally amesema kuwa amemuita mmoja wa mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano aeleze kuhusu tuhuma za kumiliki ardhi ya ekari elfu moja (1,000) ili aeleze amezipataje.
Nilikuwa Morogoro akatajwa Waziri mmoja kuwa ana ekari elfu moja watu wanataka kujua amezipataje, na nitamuita anieleze amezipataje. Hatuwezi kuwa na viongozi ndani ya chama tunachokiita chama cha wanyonge alafu baadhi yetu tunapora ardhi ya wanyonge. Ni suala la kuchagua kati ya kuwa kiongozi wa CCM au kuwa mporaji wa ardhi.” –Dr. Bashiru Ally

DC MURO APATANISHA WACHUNGAJI NA MAASKOFU ARUMERU


Leo August 30 2018 Serikali imemaliza mgogoro wa Kanisa la African Mission Evangelism Church ( AMEC TANZANIA ) Arusha uliodumu kwa zaidi ya miaka 13.
Kumalizika kwa mgogoro huo kunatokana na viongozi wakuu wa kanisa hilo waliokuwa kwenye mgogoro kukubaliana kumaliza tofauti zao baada ya serikali kuamua kuingilia kati kulinusuru kanisa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amesema mgogoro huo haukuwa na tija kwa kanisa wala wananchi waliokuwa wakipata Huduma za kiroho na ulihatarisha amani na usalama kwa waumini wa kanisa.
Pia amesema mahusino mabovu ya serikali na kanisa hilo yamechangia kudhoofisha kanisa hilo Tanzania kwa zaidi ya miaka 13.
DC Muro amewapongeza viongozi wakuu wa kanisa hilo kwa kukubali kukaa katika Meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao, ambapo amewataka viongozi hao wakuu kufanya ibada ya pamoja ya toba ambayo itawahusisha waumini wote wa kanisa hilo.
Serikali ya Rais John Magufuli itayalinda makubaliano haya pamoja na kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yenu,”amesema.



MAKUNDI YA UEFA CHAMPIONS LIGUE HAYA HAPA


Staa zamani wa club ya Man United ya England ambaye anaichezea club ya Juventus ya Italia kwa sasa Cristiano Ronaldo atarudi kucheza katika nyasi za uwanja wa Old Trafford kwa mara ya nyingine tena  msimu huu wa 2018/19.
Cristiano Ronaldo ambaye aliondoka mara ya mwisho Old Trafford kama mchezaji wa Man United mwaka 2009 na kujiunga na club ya Real Madrid ya Hispania hivyo leo baada ya kuchezeshwa droo ya makundi na Man United kupangwa Kundi H na Juventus atarudi tena hapo.
Ronaldo atarudi Old Trafford kucheza mechi yake ya makundi akiwa na Juventus ambao amejiunga nayo msimu huu akitokea Real Madrid, hivyo kupangwa kwao Kundi H na timu za Man United, Valencia na Young Boys kutampa nafasi ya kucheza tena Old Trafford.

Makundi yote ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.

KWENYE MTANDAO WA TWITTER MBUNGE NAPE ANENA HAYA.


Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameandika katika ukurasa wake wa Twitter asubuhi ya leo August 31, 2018 “Barabara inapokua na shida, usikate tamaa na kuacha safari. Badili viatu na kusonga mbele!”
Alichoandika Nape wengi hawajafahamu ana maanisha nini? ila aliambatanisha na picha yenye maneno ya kizungu ambayo yeye aliyatafsiri katika caption.

Thursday, 23 August 2018

TRUMP AKANA TUHUMA DHIDI YAKE


kutoka kushoto: Michael Cohen, Donald Trump, Stormy Daniels na Karen McDougalHaki miliki ya picha
Image captionkutoka kushoto: Michael Cohen, Donald Trump, Stormy Daniels na Karen McDougal
Rais wa Marekani amekana vikali tuhuma za kuhusika kwake katika kutumia fedha wakati wa mikutano ya kampeni kuwalipa wanawake wawili ambao wanasadikiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Katika kesi iliyosikilizwa katika mahakama moja mjini New York mapema wiki hii , mwanasheria wa zamani wa rais Trump, Michael Cohen, amesema kuwa Trump alimpa maelekezo kutoa fedha kwa lengo kuu la kuwashawishi wanawake hao kukaa kimya wakati wa uchaguzi wa rais wa 2016.
Ingawa katika mahojiano na kituo cha runinga cha Fox News, Raisi Trump alitoa ufafanuzi kuwa malipo hayo yalitoka katika fedha zake binafsi na hazikuwa fedha za kampeni kama inavyodhaniwa.
Na kuarifu kuwa alikuja kutanabahi juu ya malipo hayo baadaye, ingawa hakubainisha kuwa miamala hiyo ilifanyika wakati gani.
Raisi Trump amekuwa akimshutumu bwana Cohen kwa kupika mambo dhidi yake kwa lengo la kupata huruma na kuepuka kifungo.
Ikulu ya white house, imesisitiza kuwa kuvunja sheria ya fedha za kampeni kwa Michael Cohen hakumaanishi kuwa basi Rais trump naye atawajibika, msemaji wa white house sarah sanders amekataa kusema ni lini Rais Trump alijua juu ya malipo ya wacheza filamu wawili wa ngono
''kama rais alivyosema katika matukio tofauti tofauti, hajafanya kitu chochote kibaya, hakukua na madai yoyote dhidi yake katika hili, na kwasababu tuu Michael Cohen amekiri makossa yake haimaanishi inamgusa rais''
Katika kukiri makosa yake siku ya jumanne bwana Cohen alisema kuwa ametumwa na Trump kufanya malipo hayo lakini white house imekataa madai haya.
Malipo yafanywayo kwa siri kwa niaba ya mwanasiasa ama mgombea yeyote yanaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa sheria za kampeni za nchini Marekani

MBUNGE BOBI WINE KUSOMEWA MASHITAKA LEO

Bobi Wine akiwa na wafuasi wake

Haki miliki ya picha
Image captionBobi Wine akiwa na wafuasi wake
Mbunge ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.
Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.
Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.
Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa.
Haki miliki ya picha
Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wanakataa kumtesa.
Anatarijiwa kufikishwa mahakamani juu ya madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria.
Waraka huo umeanzishwa na Rikki stain aliekua msimamizi wa zamani wa mawamuziki fella kuti ambae alikua mkosoaji mkubwa wa serikali ya Nigeria
Anasema kuwa likua akipigwa hata kwa kuzungumza.
Jeshi ambalo ndilo linamzuia Wine linasema kuwa hajateswa na Rais Yoweri Museveni ametupilia mbali madai hayo na kuzitaja kuwa habari za uongo.
Bobi WineHaki miliki ya picha
Image captionBobi Wine

Bobi Wine ni nani?

Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.
Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.
Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).