Mke wa rais wa Marekani Melania Trump anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika mwaka huu ingawa haijafahamika ni maeneo gani ya bara hilo ataweza kutembelea.
"Hii itakuwa safari yangu ya kwanza barani Afrika na shauku yangu kubwa ni kutoa mafunzo juu ya masuala yanayowahusu watoto na vilevile kujifunza juu ya utajiri wa utamaduni na historia ya bara hilo la Afrika" Melania alielezea.
Bi.Trump anatarajia kuangazia masuala ya kazi za kibinadamu na miradi ya maendeleo ambayo yaliwahi kufanywa katika mataifa mbalimbali
Rais Donald Trump ambaye aliwahi kukosolewa kwa kuzidharau baadhi ya mataifa ya Afrika licha ya kwamba alikana kuwa mbaguzi hatasafiri na mke wake kuja barani Afrika.
Rais Trump hajawahi kufanya safari ya Afrika tangu aingie ofisini mnamo januari 2016.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg