YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday, 20 August 2018

KINACHOPELEKEA WANAWAKE WASIOOLEWA KUPANGISHWA NYUMBA KWA SHIDA

Nigeria

Haki miliki ya picha
Wamiliki wengi wa nyumba za kupangisha nchini Nigeria wanawashuku wanawake ambao hawajaolewa kuwa wanajiuza miili yao na hivyo kuwapa wakati mgumu kupangisha nyumba zao.
Olufunmilola Ogungbile mwenye umri wa miaka 30 hakutegemea kwamba anaweza kulala sebuleni katika kiti cha rafiki yake kwa kipindi cha miezi mitano wakati anatafufa nyumba bila mafanikio katika mji wa Abeokuta huko kusini wa Nigeria licha ya kwamba ana kazi nzuri.
Olufunmilola alihama kutoka Lagos baada ya kupata kazi nzuri serikani ya kuwa meneja wa mradi .Pamoja na mafanikio ya kifedha ambayo dada huyo anayo lakini alikutana na changamoto kubwa ya kupata nyumba ya kuishi katikati ya mji au maeneo yaliyo karibu na masoko kwa sababu alikuwa hajaolewa.
"Swali la kwanza ambalo wapangishaji nyumba huwa wanauliza ni kama nimeolewa na ninapowajibu kwamba bado basi watauliza tena kwa nini?"
Na maswali hayo mara zote Bi. Ogungbile anadai kuwa huwa yanamshangaza sana.
"Kwanini kuolewa au kutoolewa kiwe kigezo cha kwanza mimi kupata sehemu ya kuishi?"Bi. Ogungbile aeleza.

Wanataka watu ambao wana heshima

ubaguziHaki miliki ya picha
Image captionUbaguzi wa wenye nyumba kwa wanawake wasioolewa uwapa wakati mgumu wanawake wengi wasioolewa
Bi. Ogungbile anasema ubaguzi wa namna hiyo umeenea sana
Bi. Ogungbile aliiambia BBC kwamba asilimia 99 ya wamiliki wa nyumba hawakutaka kunipangisha kwa sababu sijaolewa.
"Madalali wengi pamoja na wamiliki wa nyumba walinitaka nimpeleke mchumba wangu wakamuone"Walisema kwamba katika nyumba zao hawataki wanaume wawe wanaingia na kutoka ,wao wanataka mtu awe na heshima zake
Bi. Ogungbile anaamini kwamba changamoto ambazo amezipitia zinatokana na mila na desturi,watu wengi wanaamini kuwa mtu akiolewa ndio ana adabu na heshima.
OLUFUNMILOLA OGUNGBILEHaki miliki ya picha
Image captionBi. Ogungbile alipinga kumpeleka mpenzi wake kwa wenye nyumba ili kukemea huo ubaguzi
"Upande huu wa dunia kama haujaolewa basi wewe ni kahaba",aliongeza
Wakati Sylvia Oyinda yeye ni meneja masoko mjini Lagos anakubaliana na kuepo kwa ubaguzi huo ambao unawapa wakati mgumu wanawake kupangisha nyumba nchini Ngeria.
Bi Oyinda, mwenye umri wa miaka 31,yeye alikuwa amechumbiwa wakati anatafuta nyumba na wenye nyumba walikataa kumpangisha mpaka wamuone mchumba wake kwanza.
Kuna misemo mingi ambayo inawanyooshea vidole wanawake ambao hawajaolewa ya kudhaniwa kuwa kuna wanaume wazee ambao wanawalipia kodi ya nyumba ..kwa mfano nchini Tanzania wanawaita 'Sponsa','buzi' au 'danga'.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg